Jinsi ya kupika maharage kwa njia rahisi bila kutumia gharama kubwa

Kuna vitu umechanganya hapa asee, sikuelewi kabisa.
Nieleweshe zaidi hapa

Zoezi hili lifanyike masaa 5-8 kabla ya muda unaotaka kuyaunga, njia hii niliitumia sana miaka ya ubachera nikiwa na jiko la mchina lile la mafuta, ambalo likiingiza hewa linalipuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hapo kwenye jiko nifafanulie plZzzz
Miaka ya 1980 tulikuwa tunatumia majiko ya mafuta ya taa kutoka nchini China, majiko haya yalikuwa na utambi ambao unachomekwa kwenye mirija kwenda juu na chini utambi unabaki unaning'inia kwenye sufulia ya jiko.

Hicho kisufulia ndicho kinatumika kuwekea mafuta ya taa, so kwa haraka haraka unaweza kuweka mafuta na kufunga kwa haraka, bahati mbaya ukiwasha na kuendelea kupika linajaa gesi, soon unasikia bust ya maana.
 
Nieleweshe zaidi hapa

Zoezi hili lifanyike masaa 5-8 kabla ya muda unaotaka kuyaunga,
Chemsha maji na weka ndani ya thermos pamoja na maharagwe kwa masaa 5 mpaka 8, masaa hayo inategemea na muda wako wa kazi na kupika.

Unaweza kuyaweka jioni na kesho asubuhi kabla ya kwenda kazini unayaunga kwa nazi, kitunguu na pilipili mbuzi kisha unakula kwa chapati na chai ya maziwa 😛!.
 
Umewazungusha sana, njia rahisi ni chukua maharage yako, yaloeke kwenye maji ya baridi tuu kwa masaa 6-7 yatakuwa yashavimba=kulainika.

Then baada ya hapo unayainjika kwa dakika 20-30, yanakuwa tayari kwa kuliwa. Na quality yake inabaki palepale.

NB: Ukiyaloeka kwa masaa zaidi ya 24, utakuta yashaota. Hizi techniques tunaiga toka vijijini tulikotokea ambapo mvua ikiwahi kunyesha na ikakukuta hujapanda, basi unachofanya unaloeka mbegu zako kwa siku moja, baada ya saa 24 zinakuwa zishaota ndio unazipanda. Ukipanda leo kesho yake unakuta zimeshachomoza.

Unforgetable
 
Umewazungusha sana, njia rahisi ni chukua maharage yako, yaloeke kwenye maji ya baridi tuu kwa masaa 6-7 yatakuwa yashavimba=kulainika
Njia hiyo ni tofauti kabisa na hii ya maji moto.
Maji baridi unaloweka na hutapata ile supu ya kuunga ila ukiweka kwenye maji ya moto ni njia ya kupika bila kuunga.

Ukiyatoa kwenye thermos unaunga moja kwa moja hauchemshi tena.

Heading Inasema: "Njia rahisi ya kupika maharagwe pasi garama kubwa"
 
Umewazungusha sana, njia rahisi ni chukua maharage yako, yaloeke kwenye maji ya baridi tuu kwa masaa 6-7 yatakuwa yashavimba=kulainika.

Then baada ya hapo unayainjika kwa dakika 20-30, yanakuwa tayari kwa kuliwa. Na quality yake inabaki palepale.

NB: Ukiyaloeka kwa masaa zaidi ya 24, utakuta yashaota. Hizi techniques tunaiga toka vijijini tulikotokea ambapo mvua ikiwahi kunyesha na ikakukuta hujapanda, basi unachofanya unaloeka mbegu zako kwa siku moja, baada ya saa 24 zinakuwa zishaota ndio unazipanda. Ukipanda leo kesho yake unakuta zimeshachomoza.

Unforgetable
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njia hiyo ni tofauti kabisa na hii ya maji moto.
Maji baridi unaloweka na hutapata ile supu ya kuunga ila ukiweka kwenye maji ya moto ni njia ya kupika bila kuunga.

Ukiyatoa kwenye thermos unaunga moja kwa moja hauchemshi tena.

Heading Inasema: "Njia rahisi ya kupika maharagwe pasi garama kubwa"
Najaribu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya 1980 tulikuwa tunatumia majiko ya mafuta ya taa kutoka nchini China, majiko haya yalikuwa na utambi ambao unachomekwa kwenye mirija kwenda juu na chini utambi unabaki unaning'inia kwenye sufulia ya jiko.

Hicho kisufulia ndicho kinatumika kuwekea mafuta ya taa, so kwa haraka haraka unaweza kuweka mafuta na kufunga kwa haraka, bahati mbaya ukiwasha na kuendelea kupika linajaa gesi, soon unasikia bust ya maana.
yalikua ya kijani mkuu!? au nna kumbukumbu mbovu.
 
Baada Ya Maharage kuiva.. Chambua mchele vizuri uoshe kisha mwga maji yote. Tia katika mfuko wa rambo kulingana na kiasi cha mchele wako.

weka mchele wote kwenye mfuko weka mafuta yakupikia na chumvi funga mfuko wako vizuri, tafuta sufuria kubwa jaza maji yakiwa na mfuko wenye mchele wako.. acha maji mpaka yatokote kwa dakika tatu tano flani.

Ukiipiua utakua umepata maji yakuogea kwa mikoa yenye baridi huku ukila wali maharage matata kabisa.

NB. Nilikua nakula wali bwenini bila kujua naupikaje maana hakukua na jiko mi ni mwendo wa heater na ndoo ya maji tuu huku arage likiiva kwa njia ya mtoa uzi huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chemsha maji na weka ndani ya thermos pamoja na maharagwe kwa masaa 5 mpaka 8, masaa hayo inategemea na muda wako wa kazi na kupika.

Unaweza kuyaweka jioni na kesho asubuhi kabla ya kwenda kazini unayaunga kwa nazi, kitunguu na pilipili mbuzi kisha unakula kwa chapati na chai ya maziwa 😛!.
Kishuleshule ilikua baada ya uji wa saa nne natia harage... mpaka saa moja limeshaiva japo sio kama lakupikwa.
Kuunga nilikua nina vitunguu nilivyovikaanga nyumbani kabisa. Ukivichanganya na harage acha kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maharagwe ya kijani sijawahi kuonana nayo, miaka hiyo yaliyokuwa yanapatikana ni rangi nyekundu nk
nauliza mkuu majiko hayo ya kichina sio maharagwe.

siku clarify vzuri swali langu sorry.
 
Back
Top Bottom