Mwaka huu Jeshi la Ethiopia limeanzisha kiwanda cha kutengeneza ndege vita zisizotumia rubani kwa shughuli za ulinzi wa ndani na biashara.
Picha hizi hapa👇
View attachment 3324765View attachment 3324766
Haya yakifanyika nchini Ethiopia huku Tanzania hapo jana Mkuu wa Majeshi kazindua mradi wa kuponda kokoto wa Jeshi. Picha hizi hapa👇
View attachment 3324767
Tukisema hii nchi tulirogwa na aliyeturoga alishakufa tueleweni jamani.
Walaaniwe CCM kwa ujinga waliotupa Watanzania!
Mwalimu Nyerere alianzisha Kiwanda cha Magari Cha NYUMBU pale Kibaha .
Kile kiwanda kilikua sawa na kiwanda Cha TATA kule India .
Leo hii India wanatengeneza Semi za TATA na mabasi na magari ya aina zote .
Kiwanda Cha NYUMBU bado kiko kwenye Maonyesho ya viwanja vya 77.
Mkapa alipoingia aliuza kila kitu na kupandisha mishahara ya wakurugenzi na mameneja ,majaji,Wakuu wa vyombo vya dola ,wabunge ,Mawaziri ,Makatibu bila kuzalisha chochote ili watumike kisiasa katika kukitumikia Chama cha mapinduzi .
Jeshi leo nalo linatumiwa na kuambiwa jiamdaeni kuwadhibiti wapinzani mwana ni mwaka wa siasa .
Matokeo yake Jeshi linaandaa vijana wa kupiga watu kwa mateke na vituko vya bunduki na hata risasi . Watawala wanatumia pesa nyingi kuzuia demokrasia na kuua utaalam mpaka majeshini.
Leo hata hawezi tena kutumia Intelijensia ya ukweli kwa sababu atashughulikiwa na CCM . Yaani kwa mfano Angetokea Polisi mmoja akasema hawa Chadema tumewakamata basi tuwapeleke kituoni na kuwafungulia kesi za kufanya fujo badala ya kuwapiga na kuwaua au kuwavunja miguu ,bila shaka angegeuka kuwa adui wa CCM kama yule aliyekua analazimishwa aseme CCM hoye kwenye mikutano ya CCM .
CCM unajenga taifa la hovyo kila sekta matokeo yake tunakua na wanajeshi wa kuchimba kokoto na kuafagia barabara kwa maufagio ya kununua china .
Watanunua mpaka Uniform China wakati wangeweza kuanzisha kiwanda cha hata kushona uniform zao wenyewe na kuajiri watu . Kutengeneza Buti , Kofia , Mikanda , n.k.
Lakini Jeshi linaagiza kila kitu nje halafu wamekubali kupiga makofi Bandari na viwanja vya ndege vikauzwa kwa Watesi wetu na wakoloni wetu wa Marekani na Dubai . Siku Marekani na china zikiamua kuivamia Afrika Mashariki na Kongo wakamtumia Kagame basi Kuwadi wa kutoa siri za jeshi atakua ni DP world .Samia atakua amepumzika zake au yupo huko ahera akiwa kwenye mito ya pombe .
Uzalendo ni Jambo kubwa sana.
Traore anayoyafanya leo Nyerere aliyaona na akina Musuguri na Akina Mayunga waliokua na Elimu ya kawaida leo tuna Majenerali waliotembea karibu dunia nzima na wenye Elimu kubwa sana lakini wanakoseshwa na watawala raia wasio na huruma wala uzalendo wanaowaza kuiba na kuficha pesa za zao Ughaibuni na watoto wao kufanya biashara .
Wanasiasa mishahara mara mia ya mishahara ya wanajeshi na mapolisi wanaotoa maisha yao kwa ajili ya nchi.
Waacheni CCM kama ni kushindwa washindwe kama ni kushinda washinde kwa haki ili waone kuwa Hii nchi ni ya watu wote sio ya wanasiasa peke yao . Jeshi libaki kulinda mipaka ya nchi wanasiasa wabaki kusimamia maendeleo na wakishindwa kutimiza ahadi zaao wajue watajibeba wenyewe bila mbeleko na watakosa kura .
Yaani Jeshi likae pembeni Ili Bunge lichangamke kwa kuwa na wabunge wenye kupigania maslahi ya umma .
Leo hii eti serikali inauza bandari kwa kuwapeleka Wabunge na waandishi na wasanii Dubai kutembea .Je,waliona mkataba huo au ni ili waupitishe kwa fadhila za kukaribishwa na kupewa viwanja Dubai ?
Jeshi ni Chombo kinachopaswa kujitenge kabisa na dhulma maana ni chombo kinachotajwa katika Biblia .
Mungu ni Mungu wa Majeshi .
Sio Mungu wa wanasiasa .Wanasiasa ni watu janja janja tu ndio maana wengi ni waabuddu mashetani na wanaoishi kwa makafara ya kuua watu wema kwa kuwsingizia kuwa ni adui wa Amani .