Jionee tofauti ya Miradi kati ya Jeshi la Ethiopia na Jeshi la Tanzania

Jionee tofauti ya Miradi kati ya Jeshi la Ethiopia na Jeshi la Tanzania

Kuna jaamaa alisema Uniform, ikiwemo 🥾 wanatakiwa kupewa kila mwaka ,lakini inaweza kupitab miaka miwili , wa tatu wanapata, hela inaandikiwa na inaliwa na wakubwa.
Askari wanajishonea wenyewe zile , na bood low quality wanapewa ulivaa mwezi zimefumuka, mpaka mgao mwingine baada ya miaka miwili.

Kwa ajili hiyo wengine wanajinunulia Boots za quality wenyewe.
Huyo ndo aende battle ground na watoto wa KAGAME???🤔🤔

Kuingia mzigo mpya kila kambi lazima wachache wanatoka kujifunza silaha waende refresher course kujifunza silaha mpya.

Hamna wanaonde refresher course kwa sababu hamna mzigo mpya.

Uganda Rwanda wako mbali sana kwa weapons na mafunzo nchinalimbal.

China, urusi, Israel, Marekani, Ujerumani.

Madam hii nimeipenda sana.Siku ikitokea MBILINGE Kagame ndani ya week tu Biashara inaisha!!

Kajaza Mamluki kibao kwenye idara nyingi!! Rejea Cornel Solomba wa Pangawe aliyetoroka akarudi Kwao Rwanda, mtaalamu wa IT Pangawe!!

Tuna akina Solomba wangapi ambao hatuwajui??

Tuko uchi utupu kwa RWANDA, pale Congo alikuwa anatupa salamu kuwa sisi ni weupe!

Askari wa bongo wanarudi Congo anapekuliwa airport utazani MWIZI wa kuku???
Tukae kwa kutulia tusimchokoze KAGAME, tutakuja kulia 😭😭

Halafu serikali (CCM)ipo busy na MIPANGO YA KUIBA KURA na ushindi hewa wa kishindo asilimia 90%🤔🤔🤔
 
Kwa sasa (Mei 2025), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania (CDF) ni Jenerali Jacob John Mkunda. Aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan tarehe 29 Juni 2022, akichukua nafasi ya Jenerali Venance Mabeyo aliyestaafu baada ya kufikia umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria [1] .

Wasifu wa Jenerali Jacob John Mkunda

- Elimu ya Awali: Alisoma katika Shule ya Sekondari ya Ruvu, ambapo alishiriki katika timu ya mpira wa miguu na shughuli za uongozi wa wanafunzi [2] .

- Kazi ya Kijeshi: Kabla ya kuteuliwa kuwa CDF, Jenerali Mkunda alikuwa Mkuu wa Operesheni na Mafunzo katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Mnamo Februari 2020, akiwa na cheo cha Brigedia, aliongoza Kikosi cha 202 cha Magharibi katika mkoa wa Katavi katika operesheni ya kudhibiti shughuli za waasi katika makazi ya wakimbizi, ambapo silaha kadhaa zilinaswa na watu kadhaa kukamatwa [2] .

- Uongozi wa JWTZ: Tangu kuchukua nafasi ya uongozi, Jenerali Mkunda amesisitiza umuhimu wa uwekezaji mkubwa wa serikali katika kuimarisha uwezo wa JWTZ, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya kisasa na kuboresha mafunzo ya kijeshi [3] .




Mmeona CV yake msimlaumu buree.
 
Tukisema hii nchi tulirogwa na aliyeturoga alishakufa tueleweni jamani.

Walaaniwe CCM kwa ujinga waliotupa Watanzania!
Kuna wakati CCM ilikuwa makini. Nyumbu (magari) yalitengenezwa na wanajeshi hao hao; na mambo mengine kadhaa ya muhimu sana kwa nchi hii.
Ni busara kuwa tunatenganisha CCM hizi ambazo ni tofauti sana.

Ninacho kubaliana na wewe kwa asili mia mia moja. Hii CCM ya sasa ni bure kabisa, ni hasara kubwa kwa nchi hii. Kama hatutaweza kuiondoa au kuibadili haraka, nchi hii itageuka na kuwa ya kuonea aibu kubwa.

Naona hapa utakuwa umempa wazo mama; kesho au keshokutwa utasikia Kafulila amewapata wawekezaji wa mradi huo.
Rais huyu haamini kamwe, kwamba kuna jambo linaloweza kufanywa na waTanzania wenyewe; hasa na taasisi kama hizi za jeshi. Ni ajabu kuwa hajawahi kusikia wachina wanavyofanya mambo kama haya, na sasa Ethiopia nao wanathubutu.
Nchi za kiafrika zitakazo pata maendeleo ya haraka ni zile zenye uthubutu, na kujiamini kuwa wanaweza kufanya jambo, na wakajipanga kweli kukifanya.

Tanzania tulishawahi sana kuwa na uthubutu. Kawaulize wale wazee wa TRC, waliokuwa wakifufua mabehewa ya reli enzi zao.

Hasara ya kuwa na viongozi kama Samia tutaijutia sana.
 
Kwanini kile kiwanda cha kutengeneza magari chapa NYUMBU pale Kibaha kilichoanzishwaga na Nyerere kikiwa chini ya JWTZ hawahawa kimeishiaga wapi...?

Kipo au nacho kwishinei kilishafisadiwa na ma - CCM na kukimaliza kabisa..?

Aidha pale pale Kibaha kulikuwa na kiwanda kingine pia kilichokuwa kina - assemble magari aina ya SCANIA kikijulikana kama Tanzania Automobile Manufacturer Company LTD (TAMCO), nacho kiliishiaga wapi..?

Kipo au au nacho kwa sbb ya sera mbovu za CCM, kimekwishinei kwa kufisadiwa na hawa nzi wa kijani kukimaliza..?
Viwanda Vyote Vipo Ila Sasa Unaposikia Ubongo Kids Wanaimba 0 Nini ? Wanajibu Maana Yake Hakuna Kitu
Pale Hakuna Linaloendelea Lenye Tija
 
Mbwembwe zao Sasa kwenye sikukuu za krismasi mwaka mpya pasaka na idd😁😁😁
 
Mwaka huu Jeshi la Ethiopia limeanzisha kiwanda cha kutengeneza ndege vita zisizotumia rubani kwa shughuli za ulinzi wa ndani na biashara.

Picha hizi hapa👇
View attachment 3324765View attachment 3324766

Haya yakifanyika nchini Ethiopia huku Tanzania hapo jana Mkuu wa Majeshi kazindua mradi wa kuponda kokoto wa Jeshi. Picha hizi hapa👇
View attachment 3324767

Tukisema hii nchi tulirogwa na aliyeturoga alishakufa tueleweni jamani.

Walaaniwe CCM kwa ujinga waliotupa Watanzania!
Mbona hata sie ipo ya SumaJKT
 
Kuna wakati CCM ilikuwa makini. Nyumbu (magari) yalitengenezwa na wanajeshi hao hao; na mambo mengine kadhaa ya muhimu sana kwa nchi hii.
Ni busara kuwa tunatenganisha CCM hizi ambazo ni tofauti sana.

Ninacho kubaliana na wewe kwa asili mia mia moja. Hii CCM ya sasa ni bure kabisa, ni hasara kubwa kwa nchi hii. Kama hatutaweza kuiondoa au kuibadili haraka, nchi hii itageuka na kuwa ya kuonea aibu kubwa.

Naona hapa utakuwa umempa wazo mama; kesho au keshokutwa utasikia Kafulila amewapata wawekezaji wa mradi huo.
Rais huyu haamini kamwe, kwamba kuna jambo linaloweza kufanywa na waTanzania wenyewe; hasa na taasisi kama hizi za jeshi. Ni ajabu kuwa hajawahi kusikia wachina wanavyofanya mambo kama haya, na sasa Ethiopia nao wanathubutu.
Nchi za kiafrika zitakazo pata maendeleo ya haraka ni zile zenye uthubutu, na kujiamini kuwa wanaweza kufanya jambo, na wakajipanga kweli kukifanya.

Tanzania tulishawahi sana kuwa na uthubutu. Kawaulize wale wazee wa TRC, waliokuwa wakifufua mabehewa ya reli enzi zao.

Hasara ya kuwa na viongozi kama Samia tutaijutia sana.

Unachokiona sasa ni athari za chini kwa chini zilizosababishwa na CCM toka awamu ya pili.
Kunyanyuka kutoka hapa tunahitaji miaka mingine mingi sana mbele na viongozi wapya wenye maono.

Toka vyama vingi viingie akili ya CCM na Serikali ni kuwa kwenye defensive mode, hapa hakuna tena akili zaidi ya kufikiria kushinda uchaguzi na kunyamazisha watu.
 
Mwaka huu Jeshi la Ethiopia limeanzisha kiwanda cha kutengeneza ndege vita zisizotumia rubani kwa shughuli za ulinzi wa ndani na biashara.

Picha hizi hapa👇
View attachment 3324765View attachment 3324766

Haya yakifanyika nchini Ethiopia huku Tanzania hapo jana Mkuu wa Majeshi kazindua mradi wa kuponda kokoto wa Jeshi. Picha hizi hapa👇
View attachment 3324767

Tukisema hii nchi tulirogwa na aliyeturoga alishakufa tueleweni jamani.

Walaaniwe CCM kwa ujinga waliotupa Watanzania!
Jeshi letu linafanya vitu kimya kimya sio lazima litangaze.
 
Back
Top Bottom