Jirani anajenga Msingi wa ukuta katikati ya jiwe la mpaka la manispaa, Sheria ya Ardhi inaruhusu hii?

Kapata mseleleko hana gharama tena
Tena hapo amwambie aweke msingi wa mawe sio tofari. Amshauri na jirani wa upande wa pili nae aweke ukuta ili yeye aje amalizie kuzoba nyuma na mbele tu
 
Huku nimeomba ushauri kwa kuuliza kwanza kwa wataalamu na wazoefu.

Kabla sijaenda kusema kokote ama kufungua kesi?

Toa jibu ama ushauri kama yupo sahihi ama anakosea
Kweli hata zile mita mbili kila upande wa kiwanja kuachwa hajaacha
 
Hiyo Sheria utekelezaji wake unahitaji busara kama si kuitazama vizuri, maana Kuna baadhi ya maeneo, hivyo vichochoro vinavyozaliwa baada ya watu kujenga kuta zao, huwavutia sana vibaka na wavuta bangi, mwisho wa siku mtajuta kuwatengenezea ofisi.
 
Hairuhusiwi
 
Huku nimeomba ushauri kwa kuuliza kwanza kwa wataalamu na wazoefu.

Kabla sijaenda kusema kokote ama kufungua kesi?

Toa jibu ama ushauri kama yupo sahihi ama anakosea
...Sasa tukupe Ushauri Gani Hapo. Wee Sema ulitaka TU kutujulisha kwamba una kiwanja!
Nikuulize wewe swali la kawaida Hapo la kutumia TU Akili... Jirani akamua kujenga Hapo, Maji ya Mvua ya Bati lake yataangukia Wapi???[emoji35]
 
Yes amemsaidia upande mmoja..........Kuna wengine wana bahati anasaidiwa pande tatu zote yeye anabakiza kufunga mbele tu na kuweka geti....Ukinunua viwanja vya kupimwa ndio advantages zake hizo.
....Akiamua Kujenga Fensi....akiamua ndio atakapojenga nyumba yake ya Kuishi, je??
 
Huo ndio ushauri! Hapo juu, jamaa hawajui chochote, badala ya kupiga kimya, wao wameamua kujivua nguo!
 
Ingekuwa ndio hivyo nyumba zote zingekuwa zina vichochoro pande zote ndio hicho unamaanisha?
 
...Sasa tukupe Ushauri Gani Hapo. Wee Sema ulitaka TU kutujulisha kwamba una kiwanja!
Nikuulize wewe swali la kawaida Hapo la kutumia TU Akili... Jirani akamua kujenga Hapo, Maji ya Mvua ya Bati lake yataangukia Wapi???[emoji35]

Punguza makasiriko mzee mbona kiwanja kitu cha kawaida tuu, mpe ushauri bila kumtolea maneno ya shombo, ukizingatia ID za humu nyingi ni feki wala hata hatufahamiani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…