Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama unapokea maoni na kufanyia kazi basi tunakuomba ufanye yafuatayo.Hii ya kugeuza simu uweze kusoma sijaipata bado. Labda uniambie inakuwaje, au umeweka auto rotate. Na usomaje wake ni kuscroll right tu. Na kama ulifika chapter fulani, unaweza kuiclick kwenye yaliyomo na itakupeleka moja kwa moja.
Nashukuru kwa maoni yako.Kama unapokea maoni na kufanyia kazi basi tunakuomba ufanye yafuatayo.
1. Simu ina kazi nyingi, kuitumia muda mrefu kaa kusoma vitabu online inaingiliana na mambo mengi, mara msg, mara call mara video call n.k
2. Ukifungua kitabu baadhi ya maandishi yanakatwa eidha chini au juu...ina poteza mtiririko kwa msomaji.
3. Unaweza ruhusu file sharing, ili mtu ahamishie kwenye pc au email for easy perusing
4. Uruhusu kitabu kifunguliwe kwa njia mbali mbali yan ile option ya open with.... iwepo.
5. Binafsi nimependa kitabu cha babilon...
Ila napata shida kukifaidi tokana na changamoto nilizosema hapo juu
Sent using Jamii Forums mobile app
Kww bajeti yetu kwa sasa bado kutengeneza app ya IOS. Ila tutaitengeneza huko mbeleni.Sisi wa iPhone tunaipataje?
Ukiweza tunaomba utuwekee zaidi vitabu vilivyotafsiriwa vya manguli kama kiyosaki, Robert Greene etc.Jisomee hadithi ya Alladini na taa ya ajabu bure ndani ya maktaba app(by pictuss). Ingia playstore uinstall.View attachment 1850154
Mwanzo tuliweka ya kusubscribe kwa Tsh 6,000 kwa mwaka lakini sasa imekuwa bure.Nimepitia reviews nimeona kuna mtu anauliza kuhusu njia ya kulipia na wewe huku unasema ni bure
Nashukuru kama imekufaa mkuu. Vitabu tunajitahidi kuweka. Kila mwezi tunaweka vitabu. Wiki hii tunatarajia kuweka vitabu viwili.Mkuu ubarikiwe Sana,hakika hii app imenipa company ya kutosha,nimeburudika kweli
Ila nilikuwa Nina ombi mmoja Kama inawezekana ku update library ingependeza kutuongezea vitabu vingine
Lakini pia ungejaribu ku categories vitabu mfano kitabu Cha tajiri wa babeli kukichanganya na kitabu Cha naluetesha au alladin Nona sio sawa,
Kuna vitabu vyenye kuelimisha na vingine kuburudisha...na vingine ambavyo Ni hadithi za picha(mfano nyati akamuambia Simba twende tukanywe maji)
Kwa hayo you're naomba nikupongeze Tena kwa kazi uliyoifanya ya kutuletea collection ya vitabu..tupunguze ujinga na kuongeza maarifa
Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
Jan Fedha Mrefu - Long John SilverKisiwa chenye Hazina. Hadithi hii ya The Treasure Island unaweza isoma bure ndani ya Maktaba app by pictuss. Install kutoka playstore na ujisomee.
View attachment 1842693
Born a leader.Jan Fedha Mrefu - Long John Silver
Mkuu hongera sana, kwa kweli ni wazo zuri sana, nimepakua app na ku download baadhi ya vitabu, ni app nzuri na vitabu vinapatikana kwa kb chache, ombi langu ongezeni vitabu hata vile vya Europe na Amerika huwa ni vizuri sana isipokuwa mvitafsiri kwa kiswahili ili kuleta maana ya app hii, pia ningeomba muongeze kitabu cha Wagagagigikoko kile cha Abunuwasi na Lizabeta.Sasa ndani ya App yetu ya maktaba unaweza kujisomea vitabu vyote vilivyomo bure kabisa. Ingia playstore na install Maktaba by pictuss APP.
Unaweza kusoma vitabu hata ukiwa offline.
View attachment 1842690
Vitabu vilivyopo mpaka sasa.
1. Hekaya za Abunuwasi na hadithi zingine
2. Machimbo ya mfalme Sulemani
3. Hadithi ya Allan Quatermain
4. Kisiwa chenye hazina
5. Alibaba na wezi arobaini
6. Alladini na taa ya ajabu
7. Safari saba za Sinbad
8. Tajiri wa Babeli: Tafsiri ya kitabu The richest man in Babylon chake George Cleason
9. Sanaa ya vita: Tafsiri ya kitabu The art of war cha Sun Tzu
10. Kiongozi: Tafsiri ya kitabu The Prince cha Niccolo Machiavelli
11. Nalutuesha: Cha Pete McGregor
12. Jasiri katika Africa: Chake J. C. Chande
13. Kusadikika: Cha Shaaban Robert
14. Kufikirika: Cha Shaaban Robert
15. Adili na nduguze: Cha shaaban Robert
16. Vazi jipya la mfalme: Tafsiri ya kitabu Emperor's new clothes
17. Wasifu wa Siti binti Saad cha Shaaban Robert
18. Ifahamu pombe
19. Mtu aliyepanda miti: Tafsiri ya kitabu cha Jean Giono, kilichotafsiriwa na Mara Consult
20. Kaburi la wanaume: Ally Mbetu
21. Sura ya mtu roho ya shetani: Ally Mbetu
22. Shamba la wanyama: Tafsiri ya kitabu The animal farm
23. Nchi ya wasioona: Tafsiri ya kitabu The country of the blind
24. Someni kwa furaha, kitabu cha Tatu, cha muandishi Alfonso Loogman.