Jitahidi sana usiwe sehemu/sababu ya ndoa za rafiki zako kuvunjika

Jitahidi sana usiwe sehemu/sababu ya ndoa za rafiki zako kuvunjika

Nilikuwa kwenye wakati mgumu baada ya kuona shem ana mpango wa kumuua tajiri yangu pindi amalizapo kujenga nyumba yao. Wana watoto watatu mwanamke ni rika langu nikaanza vurugu za kuanza kumtaka kimapenzi huyu mke wa tajiri alianza kushangaa huyu mfanyakazi wetu anautoa wapi ujasiri wa kunitongoza! Nilikomaa naye mpanga akanifungulia duka lake, nilikuwa nikimrecord audio mara zote tunapogegedana kama ushahidi na njia ya kumzuia kutekeleza lengo lake la kumuua tajiri bila kumwambia ya kuwa siri yako ya kutaka kumuua tajiri yangu naijuia.
Kwa huyu tajiri yangu mimi nilikuwa ndio msimamizi wa ujenzi wa nyumba yao,nilikuwa naharibu vitu mbalimbali na vyengine kuvichukua ili kuzuia nyumba hiyo kukamilika(hapa nilikuwa na risk sana) lkn nashukuru Mungu niliweza kufanya hivi kwa muda wa miaka mitatu bila tajiri kubaini kuwa mimi ndiye muharibifu wa mipango yake. Sasa walivyopata mtoto wa nne ikabidi nimtafute mganga Washawasha nikampanga jinsi ya kumrubuni tajiri siku nitakayokwenda naye kwake ili nianze kurudisha vitu kidogokidogo na nianze kumtisha huyu mke wetu😍(mke wa tajiri) Basi nikamshawishi tajiri na mkewe twende kwa mganga, how come material ya ujenzi yanapotea kizembezembe pale site kwake na ikiwezekana tuisindike nyumba.
Tulifika kwa mganga huyu fix ( Washawasha ) akafanya mambo yake kama nilivyompanga na tukapewa baadhi ya dawa za kwenda kutupa baharini na masharti mengine ambayo wao waliogopa kufanya mi nikasema nitafanya,tukaondoka zetu.
Basi kila siku nikawa narudisha vitu usiku kidogokidogo mara leo box la tiles,kesho roll la wire n.k mpaka nilipomaliza kurudisha vitu nilivyochukua. Tajiri alifurahi sana na tukaenda kumpoza na cha juu mganga( Washawasha ) kwa kazi yake nzuri.
Baada ya hapo nikaanza kumwambia mke wetu(mke wa tajiri) ya kuwa mganga ameniambia siri za mpango wake wa kutaka kumuua tajiri,kwahiyo amenituma na amenisihi nikwambie achana na mpango huo kwa kuwa hautofanikiwa kwa lolote. Alishtuka sana,nikamwambia yule mganga ni kiboko si umeona wezi walivyokuwa wakirudisha mali zenu. Aliniomba sana nisimwambie mumewe kuhusu hilo,nami nikamkubalia.
Nikawa nimelimaliza suala hilo ovu la huyo mwanamke bila kuwatenganisha na penzi lao.
Nalog off
Hii story inafundisha sana mkuu. Asante brother
 
Niliwahi kupata bahati ya kuujua mchepuko wa uncle kwa mbinu zangu flaflani, kutokana na uncle kuniamini sana alikua ananiagiza nipeleke na pia kuchukua baadhi ya vitu.

Ubaya ni kwamba uncle alinogewa na ile side chick hadi akajisahau mkewe akaanza kuhisi hilo jambo na akaanza kumfanyia upelelezi kimyakimya ili amjue huyo mla mali yake...

Uncle naye akagundua anafatiliwa akaanza kukwepa mitego hasa ya kwenye simu.. Mie ndo nilimwekea password na hilo hata mkewe alikua anajua

Kufupisha stori ni kwamba, nilikuja kugombana na mke wa uncle kwa kunilazimisha nimpeleke anapoishi mwizi wake, pia alishaplan kwamba akishamjua mwizi wake na akawa na ushahidi kamili basi kinachofata ni kuomba talaka na kumwachia uncle wanae

Nilikaribia kumpeleka ila nikakumbuka maisha niliyokulia mie alafu wale madogo ndo waje waishi kama mie dah!. Roho ilinisuta sana nikaghairi kufanya hivyo, kilichotokea hasira zake zikahamia kwangu na mie ndo nikawa adui wa familia yake

Huenda nilifanya ujinga sijui, lakini pia nahisi kama wangeachana nadhani leo hii wale madogo wangekua wanarandaranda ovyo
... Familia ya uncle inaendelea kuishi hadi leo... Mtetezi wa familia nipo nazunguka tu sina mwelekeo wowote NAAMKA.. NAKULA.. NALEWA... NALALA hiyo ndo ratiba yangu 4N's
 
Habari zenu waungwana wa humu jamiiforums.

Jamani nyie waungwana, katika haya maisha jitahidi sana usiwe sehemu/sababu ya ndoa za rafiki zako kuvunjika. Hivi utasijikiaje ukiwaona watoto wanazurura mitaani baada ya wazazi wao kuachana?

Kama ndoa inavunjika kisha mke na mume wanatengana, basi waachane kwa sababu zao wenyewe na sio kwa kuwa kuna mkono wako wewe rafiki. It's not fair at all. Ninarudia tena sio sahihi kabisa.

Nyie vijana mliozaliwa juzi juzi, kuna msemo mmoja wakongwe waliwahi kusema ya kwamba, wapiganapo mafahari wawili siku zote zinazoumia ni nyasi. The same applies to the marriage. Once couple break up, it's the kids who suffer the most.

Jenga picha upo Kariakoo katika shughuli zako alafu unakutana na mtoto wa rafiki yako ambaye kwao walikuwa na hali nzuri tu ya kimaisha ila sasa anauza maji ya chupa yale ya 500 kwa sababu alishindwa kuendelea na kidato cha pili kwa sababu baba na mama waliachana kwa umbea ambao wewe uliupeleka.

Unapeleka umbea unaojua fika kwamba utavunja ndoa za watu wa sababu gani? Kwanini unakuwa na roho ya ibilisi namna hiyo? Au kwa kuwa rafiki yako anafanya kazi Bank fulani kubwa kama Mkurugenzi hivyo unahisi ukimpa habari ya kuwa mkewe anachepuka ndio atakupenda sana na kukusaidia kupata kazi?

Au unahisi kwa kumwambia rafiki yako kuwa mkewe ameshika mimba ambayo yeye rafiki yako sio "biological father" ndio atakupenda sana na kukununulia beers mbili tatu kila weekend? Yaaani unavunja ndoa ya watu kisa beers? Kwani ungekaa kimya ungepata hasara gani?

Kama imeandikwa kuwa utapata kazi nzuri basi Mungu atakupa tu siku yako ikifika na sio kuingilia ndoa za watu kisha kuwaweka watoto katika mateso ambayo hayakustahili. Kwani kama suala ni beers, usipokunywa utakufa?

Mbona kuna watu hawanywi beers na bado wanaishi maisha mazuri sana. Basi hata kama unataka Beers kwanini usinunue kwa pesa zako mpaka unaleta ugomvi ndani ya familia za watu wengine?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Nimemiss mastory yako ya kivita
 
Niliwahi kupata bahati ya kuujua mchepuko wa uncle kwa mbinu zangu flaflani, kutokana na uncle kuniamini sana alikua ananiagiza nipeleke na pia kuchukua baadhi ya vitu.
Ubaya ni kwamba uncle alinogewa na ile side chick hadi akajisahau mkewe akaanza kuhisi hilo jambo na akaanza kumfanyia upelelezi kimyakimya ili amjue huyo mla mali yake...
Uncle naye akagundua anafatiliwa akaanza kukwepa mitego hasa ya kwenye simu.. Mie ndo nilimwekea password na hilo hata mkewe alikua anajua
Kufupisha stori ni kwamba, nilikuja kugombana na mke wa uncle kwa kunilazimisha nimpeleke anapoishi mwizi wake, pia alishaplan kwamba akishamjua mwizi wake na akawa na ushahidi kamili basi kinachofata ni kuomba talaka na kumwachia uncle wanae
Daaah kama movie vile ila ndio maisha halisi uliyoyapitia. Pole sana mzee baba. Hiyo ndio ilikupa changamoto na kukukomaza kiume...
 
Niliwahi kupata bahati ya kuujua mchepuko wa uncle kwa mbinu zangu flaflani, kutokana na uncle kuniamini sana alikua ananiagiza nipeleke na pia kuchukua baadhi ya vitu.
Ubaya ni kwamba uncle alinogewa na ile side chick hadi akajisahau mkewe akaanza kuhisi hilo jambo na akaanza kumfanyia upelelezi kimyakimya ili amjue huyo mla mali yake...
Uncle naye akagundua anafatiliwa akaanza kukwepa mitego hasa ya kwenye simu.. Mie ndo nilimwekea password na hilo hata mkewe alikua anajua
Kufupisha stori ni kwamba, nilikuja kugombana na mke wa uncle kwa kunilazimisha nimpeleke anapoishi mwizi wake, pia alishaplan kwamba akishamjua mwizi wake na akawa na ushahidi kamili basi kinachofata ni kuomba talaka na kumwachia uncle wanae
Nilikaribia kumpeleka ila nikakumbuka maisha niliyokulia mie alafu wale madogo ndo waje waishi kama mie dah!. Roho ilinisuta sana nikaghairi kufanya hivyo, kilichotokea hasira zake zikahamia kwangu na mie ndo nikawa adui wa familia yake
Huenda nilifanya ujinga sijui, lakini pia nahisi kama wangeachana nadhani leo hii wale madogo wangekua wanarandaranda ovyo
... Familia ya uncle inaendelea kuishi hadi leo... Mtetezi wa familia nipo nazunguka tu sina mwelekeo wowote NAAMKA.. NAKULA.. NALEWA... NALALA hiyo ndo ratiba yangu 4N's
Mkuu, ulifanya uamuzi wa maana sana wa kutokuvunja ndoa ya uncle wako la sivyo laana ya hao watoto ingekuandama mpaka kufa kwako.
 
Back
Top Bottom