Jitahidi sana usiwe sehemu/sababu ya ndoa za rafiki zako kuvunjika

Hii story inafundisha sana mkuu. Asante brother
 
Niliwahi kupata bahati ya kuujua mchepuko wa uncle kwa mbinu zangu flaflani, kutokana na uncle kuniamini sana alikua ananiagiza nipeleke na pia kuchukua baadhi ya vitu.

Ubaya ni kwamba uncle alinogewa na ile side chick hadi akajisahau mkewe akaanza kuhisi hilo jambo na akaanza kumfanyia upelelezi kimyakimya ili amjue huyo mla mali yake...

Uncle naye akagundua anafatiliwa akaanza kukwepa mitego hasa ya kwenye simu.. Mie ndo nilimwekea password na hilo hata mkewe alikua anajua

Kufupisha stori ni kwamba, nilikuja kugombana na mke wa uncle kwa kunilazimisha nimpeleke anapoishi mwizi wake, pia alishaplan kwamba akishamjua mwizi wake na akawa na ushahidi kamili basi kinachofata ni kuomba talaka na kumwachia uncle wanae

Nilikaribia kumpeleka ila nikakumbuka maisha niliyokulia mie alafu wale madogo ndo waje waishi kama mie dah!. Roho ilinisuta sana nikaghairi kufanya hivyo, kilichotokea hasira zake zikahamia kwangu na mie ndo nikawa adui wa familia yake

Huenda nilifanya ujinga sijui, lakini pia nahisi kama wangeachana nadhani leo hii wale madogo wangekua wanarandaranda ovyo
... Familia ya uncle inaendelea kuishi hadi leo... Mtetezi wa familia nipo nazunguka tu sina mwelekeo wowote NAAMKA.. NAKULA.. NALEWA... NALALA hiyo ndo ratiba yangu 4N's
 
Nimemiss mastory yako ya kivita
 
Daaah kama movie vile ila ndio maisha halisi uliyoyapitia. Pole sana mzee baba. Hiyo ndio ilikupa changamoto na kukukomaza kiume...
 
Mkuu, ulifanya uamuzi wa maana sana wa kutokuvunja ndoa ya uncle wako la sivyo laana ya hao watoto ingekuandama mpaka kufa kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…