Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
Habari zenu waungwana wa humu JamiiForums.
Jamani nyie waungwana, katika haya maisha jitahidi sana usiwe sehemu/sababu ya ndoa za rafiki zako kuvunjika.
Hivi utasijikiaje ukiwaona watoto wanazurura mitaani baada ya wazazi wao kuachana kwa sababu ya uchonganishi wako?
Kama ndoa inavunjika kisha mke na mume wanatengana, basi waachane kwa sababu zao wenyewe na sio kwa kuwa kuna mkono wako wewe rafiki. It's not fair at all. Ninarudia tena sio sahihi kabisa.
Nyie vijana mliozaliwa juzi juzi, kuna msemo mmoja wakongwe waliwahi kusema ya kwamba, wapiganapo mafahari wawili siku zote zinazoumia ni nyasi. The same applies to the marriage. Once couple break up, it's the kids who suffer the most.
Jenga picha upo Kariakoo katika shughuli zako halafu unakutana na mtoto wa rafiki yako ambaye kwao walikuwa na hali nzuri tu ya kimaisha ila sasa anauza maji ya chupa yale ya 500 kwa sababu alishindwa kuendelea na kidato cha pili kwa sababu baba na mama waliachana kwa umbea ambao wewe uliupeleka.
Unapeleka umbea unaojua fika kwamba utavunja ndoa za watu wa sababu gani? Kwanini unakuwa na roho ya ibilisi namna hiyo? Au kwa kuwa rafiki yako anafanya kazi Bank fulani kubwa kama Mkurugenzi hivyo unahisi ukimpa habari ya kuwa mkewe anachepuka ndio atakupenda sana na kukusaidia kupata kazi?
Au unahisi kwa kumwambia rafiki yako kuwa mkewe ameshika mimba ambayo yeye rafiki yako sio "biological father" ndio atakupenda sana na kukununulia beers mbili tatu kila weekend? Yaaani unavunja ndoa ya watu kisa beers? Kwani ungekaa kimya ungepata hasara gani?
Kama imeandikwa kuwa utapata kazi nzuri basi Mungu atakupa tu siku yako ikifika na sio kuingilia ndoa za watu kisha kuwaweka watoto katika mateso ambayo hayakustahili. Kwani kama suala ni beers, usipokunywa utakufa?
Mbona kuna watu hawanywi beers na bado wanaishi maisha mazuri sana. Basi hata kama unataka Beers kwanini usinunue kwa pesa zako mpaka unaleta ugomvi ndani ya familia za watu wengine?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.