Jitu alilolichukua kutoka huko nje na kuliteua ni nani hasa?

Jitu alilolichukua kutoka huko nje na kuliteua ni nani hasa?

Mama leo amechukia na kuamua kufunguka kwa codes.
Kwa haraka haraka, inavyoonekana kuna mtu, huenda ni maarufu au mzoefu ambaye alimuamini kutokana na exposure aliyeipata kimataifa kiasi cha kuamua kumteua idara fulani nyeti, ghafla mtu huyo amegeuka kuwa mwiba mkali wa kuiumiza serikali yake vibaya kwa 'kuchomoa betri'.

Hilo jitu ni nani hasa?
Je, bado lipo ndani ya mamlaka za kiserikali?
Siku za hivi karibuni anaonekana kuchukia sana.
 
Mama leo amechukia na kuamua kufunguka kwa codes.
Kwa haraka haraka, inavyoonekana kuna mtu, huenda ni maarufu au mzoefu ambaye alimuamini kutokana na exposure aliyeipata kimataifa kiasi cha kuamua kumteua idara fulani nyeti, ghafla mtu huyo amegeuka kuwa mwiba mkali wa kuiumiza serikali yake vibaya kwa 'kuchomoa betri'.

Hilo jitu ni nani hasa?
Je, bado lipo ndani ya mamlaka za kiserikali?
Yeye si anateua kwa kuangalia dini 😅 😅 😅 😅 😅 😅
 
Itakuwa yule kigogo wa Twitter aliyeinyesha serikali enzi za jiwe..!!
Yule mbona alikua palepale ikulu tangu enzi za Magufuli, na hajaondoka. Na yule shida yake kubwa na Magufuli ilikua ni kukatwa jina lake na kupitishwa jamaa fulani kwenye kinyang'anyiro cha ubunge.

Kwasasa ni mtiifu sana kwa mama, na ananeemeka na yanayoendelea.
 
Alikaa kwa bahati mbaya haikuwa nafasi yake, wacha aendelee kujua na kuaibika. Unajua Mkuu kama nafasi ulipata kwa haki zote huwezi kuwa na itikadi za mipasho na kwenda kujipendekeza kwa Mashehe misikitini ili wapate kukusemea na wanaokusemea nao ni full mipasho.

Trump ni jasiri na anajiamini kwa sababu nafasi alipata kwa haki hakubebwa. Na anawanyoosha kweli maraisi uchwara hasa hawa wa Kiafrika.
Katika uongozi hakuna kukaa kwa bahati mbaya. Kuna thorough vetting.

Ukisema alikaa kwa bahati mbaya maana yake hapo hamna vetting.

Halafu hujajibu hoja yangu. Anayesemwa nani?

Nchi haitakiwi kuendeshwa kwa mipasho na vineno vya vijembe kama taarab.
 
alisoma Marekani na alienda na mkewe na wakawa wanaishi kwenye appartment ipo ghorofa ya 58 wakati huo mimi naishi Colorado wakazembea mtoto wao mdogo wa umri wa mwaka mmoja alidondoka kutoka dirishani hadi chini ila aliokolewa na zima moto na toka siku hiyo walimnyanga,'nya mtoto huyo
Heshima, mkuu 'fimboyaukwaju'.
Wasira kaamua mwenyewe kuharibu jina lake kwenye historia ya nchi hii kwa kukubali kujiunga na utawala huu unaofanya kila juhudi ya kuliangamiza taifa hili.
Sijui nini hasa kimemfanya akubali nafasi ya kutumika kama kikaratasi cha chooni tu; huku akiharibu kila kitu alichokwisha kifanya kujijengea heshima.
Kwa umri huo, bado anatafuta pesa; ya nini? Pesa ambayo unajuwa ni ya kuchangia kuhujumu taifa lake!
 
Ni kama vile ulikuwa akilini mwangu.
Kila nikijaribu kuwaza tofauti ngoma inakataa kabisa.
Nahisi hili kombola ametumiwa kipara.
Ile timu ya mtu 3 ni hatari sana. Baba yao mzee wa canada🍁
Mmoja ndie kigogo aliemtesa JPM, mwingine hutumiwa kama chambo, wa mwisho ana ego ya hatari.
 
Lakini mtu huyo kama anaibua uovu, tatizo liko wapi? Mbona kama hakuna malengo mazuri kabisa ya kuiongoza hii nchi kwa uadilifu? Rais anachukia waziwazi mtu anayetoa uovu? Ni message gani inatumwa kwa wabadhilifu? Waendelee kula, watu wazuri watashughulikiwa?
 
Mama leo amechukia na kuamua kufunguka kwa codes.
Kwa haraka haraka, inavyoonekana kuna mtu, huenda ni maarufu au mzoefu ambaye alimuamini kutokana na exposure aliyeipata kimataifa kiasi cha kuamua kumteua idara fulani nyeti, ghafla mtu huyo amegeuka kuwa mwiba mkali wa kuiumiza serikali yake vibaya kwa 'kuchomoa betri'.

Hilo jitu ni nani hasa?
Je, bado lipo ndani ya mamlaka za kiserikali?
Mchungaji Gwajiboy
 
Aisee kwamba wazalendo Watanganyika wanaowafikishia wananchi mipango miovu ya Siri ndo wanaitwa mijitu? Huyu SSH kama hajaanza dawa apewe!
Yani hapo ndio inasikitisha sana. Taarifa zilizotolewa ni nzuri au mbaya kwa maslahi ya taifa? Mbona kama anaonyesha waziwazi kuwa hana nia njema na taifa? Kwa nini akasirike hayo maovu kutoka? Kwa nini aone anakuwa yeye targeted, bila ya kuangalia maslahi ya taifa? Matamshi yake huwa yanamuaibisha sana na kumuonyesha wazi kuwa hana lengo zuri na sisi.
 
Back
Top Bottom