JKU na POLISI: Lipi lina hadhi kubwa zaidi Zanzibar?

Amini amini nakwambia, ni rahisi kuwakuta vijana wa Scout wakiwa karibu na uwanja wa Gwaride kwenye maadhimisho ya Kitaifa kama Muungano na Uhuru kuliko hao migambo wa visiwani
OK sawa Mkuu kwani unajua Hata kuna mambo yanayohusu Muungano na yasiyohusu Muungano?
Unajua kama Zanzibar nalo ni Taifa?
Unajua kuwa Waziri wa Afya wa Tanzania Hana sauti Akiwa zanzibar?
 
Maelezo yameshiba asante.
 
Mkuu, Jeshi la nchi yoyote huwa liko attached na State. Je, Zanzibar ni State? (Rejea definition ya State iliyotolewa na Montevideo Convention on The Rights and Duties of State ya Mwaka 1939).
Kama sio State, je, hao JKU wanawekwa kundi gani?
Umeshawahi kusikia kuna Jeshi la Palestine? Umewahi kujiuliza kwanini wanaitwa Wanamgambo wa Kipalestina?
Mkuu Paschal yupo sahihi kabisa, jaribu kujiongezea maarifa zaidi kuhusu State ndiyo utajua kwanini hao JKU amewaweka kundi hilo
 
Rejea Ibara ya 147 ya Katiba ya JMT na uache kukariri maneno ya vijiwe vya kahawa.
 
JUTZ = Jeshi la Uhifadhi Tanzania. Nadhani lina miaka isiyozidi 3.
Liko vizuri.
 
OK sawa Mkuu kwani unajua Hata kuna mambo yanayohusu Muungano na yasiyohusu Muungano?
Unajua kama Zanzibar nalo ni Taifa?
Unajua kuwa Waziri wa Afya wa Tanzania Hana sauti Akiwa zanzibar?
Najua hilo, je, unadhani Ulinzi na Usalama sio jambo la Muungano pia?
Unachopaswa kujua ni kwamba Zanzibar sio State ndiyo maana sio member wa United Nations
 
Habari ministrant
Naifahamu Vizuri Montevideo convention on rights and duties of the state ya mwaka 1939..
Nitaichambua only Article 1 kwa ajili ya kuthibitisha kuwa zanzibar ni state..

Article 1

"The state as a person of international law should possess the folowing qualifications:
(a) a permanent population [people]
(b) a defined teritory; [land]
(c) government; [Serikali]
(d) capacity to enter into relations with the other states...


Nitaanza na Kudeclare kwamba zanziba ni Nchi..
Turudi katika Katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar..

ibara ya kwanza ya Katiba hiyo na ibara ya Pili inaonyesha Declaration ya Teritory na Kujideclare kuwa Yenyewe ni state..
nita quote

"Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar."

Ibara ya Pili..


"Zanzibar ni miongoni mwa Nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."


Vipi zanzibar imedeclare kuhusu People au permanent Population..
Yes and its Cited in ibara ya 6 ya katiba ya Zanzibar ibara ndogo ya 1 na 2

"6.(1) Kutakuwa na Mzanzibari ambaye upatikanaji wake, upoteaji wake na urudishwaji wake atakuwa kama alivyoainishwa katika Sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

(2) Kila Mzanzibari, kwa misingi ya Katiba hii, ataweza kufaidi haki na fursa zote anazostahiki Mzanzibari, na atapaswa kutekeleza wajibu, majukumu na dhamana za Mzanzibari kama ilivyo kwenye Katiba hii au kwenye Sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi."



Vipi kuhusu Goverment yaani Serikali Je zanzibar ina Serkali?
Offcuze yes,
Cited on Katiba ya Zanzibar ibara ya 26, ibara ya 51 na ibara ya 52..



Bila kusahau kwamba zanzibar Ina..
Bunge
Baraza la mawaziri
Mahakama
Serikali
Jaji mkuu
e.t.c.


So kwa Montevideo convention on rights and duties of the state ya mwaka 1939..
Zanzibar Inkidhi vigezo vya kuwa State so Do the Army and millitary?

Kumbuka pia Kuwa katiba yao ina nguvu ya kisheria kabla ya kujibu..
 
Najua hilo, je, unadhani Ulinzi na Usalama sio jambo la Muungano pia?
Unachopaswa kujua ni kwamba Zanzibar sio State ndiyo maana sio member wa United Nations
Kwahyo mkuu We umeona kikubwa Ili kuwa state ni lazma Awe member wa UN ,Los angels Ni State je ni member wa UN?
New York ni state Je ni member wa UN?..

Kwa kifupi

Tanganyika was a Member of the United Nations from 14 December 1961 and Zanzibar was a Member from 16 December 1963. Following the ratification on 26 April 1964 of Articles of Union between Tanganyika and Zanzibar, the United Republic of Tanganyika and Zanzibar continued as a single Member, changing its name to the United Republic of Tanzania on 1 November 1964.
 
Nilikuwa nakusubiri kwenye kipengele D Mkuu, naona umeshapata jibu sasa. Kwamba Zanzibar haina sifa ya State ndiyo maana hatuioni kwenye mawanda ya siasa za Kimataifa kama Membership kuwa mwanachama wa jumuiya za kimataifa kama AU, UN, pia haina mamlaka ya Dola ya kufungua Ubalozi kwenye Taifa lingine lolote.
Kama kiumbe hai kina sifa kuu saba kuwa na sifa Sita bado unakuwa haujafuzu kuwa kiumbe hai.
Mfano mzuri gari hatuwezi kuliita kiumbe hai kwakuwa lina uwezo wa kujongea, kuhisi, na nyinginezo ila kwa kukosa sifa mbili kuu za kiumbe hai, gari halijakidhi vigezo vya kuitwa kiumbe hai
 
Unadhani haijawa member kwa bahati mbaya, au kwakuwa tayari Soveregnty yake imemezwa na Muungano?
Kwanini jitihada za kujiunga na OIC ziligonga mwamba? Acha kukaza fuvu bro
 
Washauri wote wa mgambo ni wajeshi wa JWTZ, bado mgambo ni mgambo na jeshi ni jeshi. CDF akistaafu akaajiriwa ultimate security, hakuigeuzi ultimate security kugeuka jeshi kwasababu inaongozwa na general!. Most mercenaries ni trained soldiers, hakuwafanyi wawe jeshi. Hivyo KMKM na JKU ni migambo hata ikiongozwa na ma general wa jeshi.
P
 
Jkt maafisa wote ni jwtz,hivyo jkt au jku ni jwtza,na kama itatokea vita wote wanaingia uwanjani bila kujali wewe ni jkt su jku au jwtz,huu ndio ukweli kwa lugha rahisi jkt au jku vyote ni kitengo mdani ya jwtz
 
Tofauti ni kubwa sana, even kimafunzo mgambo wana light training, tofauti na full military members. na kuna vitu zaidi wanatofautiana
Tofauti ni status tuu, kuna migambo who are better trained kuliko wajeshi wetu!.
P
 
Rejea Comment #70..
Zanzibar na Tanganyika Vilinyanganywa viti Umoja wa mataifa na Kupewa Taifa moja lililoitwa United Republic of Tanganyika and Zanzibar ambayo baadaye ilibadiliishwa na kuwa United republic of Tanzania..

Kwakuwa Viliungana vikabaki.kuwa Nchi moja yenye nchi mbili zilizoungana..

Zanzibar wamejaribu kuandika barua Nyingi sana kuomba kiti chao kurudi Au Na UN ila imeshindikana..

Hata kama unaangalia mpira Utagundua juzi kati Timu ya Taifa ya Zanzibar walibeba bango La kudai Kiti kwenye Jumuia za kimataifa...
 
Jkt maafisa wote ni jwtz,hivyo jkt au jku ni jwtza,na kama itatokea vita wote wanaingia uwanjani bila kujali wewe ni jkt su jku au jwtz,huu ndio ukweli kwa lugha rahisi jkt au jku vyote ni kitengo mdani ya jwtz
JKT ni jeshi, JKU ni jeshi usu!.
P
 
Kinachofanya wawe jeshi ni Sheria na Katiba ma umiliki chini Ya dola na yes wanao kwa.Katiba na Sheria zao..
Kwanini Unashindwa kujua na wakati wewe ni.Wakili?
 
Unafurahisha Sana kwa majibu haya Mkuu!
NIlikuomba unijibu Kwa Kutumia combat officers Na insignia Utifautishe unakuja kitofautisha na biyu vya ajabu?
Unanijibu kwa ultimate security Really?
Msomi wa sheria?
Mgambo Sio jeshi na wala sio waajiriwa..
Ila JKU ni waajiriwa Unajua tifauti?
 
Jeshi ni lugha tu but si jeshi kitaalam. Wangekuwa jeshi kamili wasingekuwepo chini ya wizara ya mambo ya ndani, hata kisheria hawana power kama waliyonayo jeshi la wananchi ambalo ndio main military.
wewe uko busy kufuta maziwa kwenye carpet na tambala lenye mkojo,yaani afadhali hata mayala alikuwa karibu na uhalisia.

kama polisi haipaswi kuitwa jeshi,si sababu ipo chini ya wizara,mbona jwtz iko chini ya wizara!!!au ulitaka polisi iwepo wizara ya ulinzi ndipo ukubali kwamba ni jeshi??

neno jeshi ndani ya polisi limewekaa kiusalama,vingine hatuwezi kuwaambia vyote hapa ila ni ile ile mbinu kama ya kikosi 577kj mgulani,hizo namba zimewekwa kimkakati,maandazi kama nyinyi hamuwezi elewa mtaanza kuhoji hoji hovyo namba 1 na 25 viko wapi?

baadae jeshi leti la ulinzi litakapofikia hatua fulani basi hatutaona hii police force,au prison force.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…