TANZIA GE2025 Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Aliyewahi kuwa Spika na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia, leo Agosti 6, 2025, taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson imeeleza kuwa msiba umetokea Dodoma

Dkt. Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

WASIFU MDOGO WA JOB NDUGAI
Alizaliwa Januari 21, 1963 na kupata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)

Amekuwa Mbunge wa Kongwa kwa miaka 25 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Katika uongozi wake wa bunge, mambo kadhaa yameibua mjadala mkubwa ikiwemo sakata la wabunge 19 wa CHADEMA wanaodaiwa kuvuliwa uanachama wao, na kuhojiwa kwa baadhi ya wabunge akiwemo Josephat Gwajima na Jerry Muro kwa madai ya kushusha hadhi na heshima ya bunge.

Suala jingine ni kumtaka mmoja wa wabunge aliyedai amevaa nguo zisizo za staha kutoka ndani ya ukumbi wa bunge. Uamuzi huo ulikosolewa vikali, wakosoaji wakieleza kwamba vazi la mbunge huyo halikuwa na tatizo. Karibuni, amezua mjadala tena kwa kusema Tanzania haitakiwi kukopa ili kufadhili miradi ya maendeleo.

Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
Yule Nabii kijana wiki iliyopita alitoa unabii wa nchi na moja ya mambo aliyoyatabiri ni kuhusu mjumbe aliyetumwa Dodoma akiwa na chupa yenye sumu ikimlenga kiongozi mstaafu wa ngazi za juu. Na akasema viongozi wawe makini. Je ndiyo hii alikuwa akitabiri?
 
Hapa ndio nataka kuamini hata j8m aliuwawa, hakikuwa kifo cha kibinadamu.
J8pm aliuawa hiyo ni confirmed 💯 %, na ndiyo maana kuuana hakutakuwa na mwisho maana yake watu wamejaa visasi balaa. Kama unakumbuka kuna uzi mdau mmoja aliwahi tahadharisha kuwa rais aliyepo madarakani akifa nchi inaweza kuwa kwenye hali ya tahadhari mpaka miaka 50, lengo ni kujitafuta nani alimuua na nani alihusika. Ndiyo maana tunaamini wauaji wa Dkt Magufuli watakuja kujulikana wengine watauawa kwa risasi wengine kufungwa maana watu wa usalama sidhani kama watakubali hii aibu ya karne. Ndiyo maana mi nikiangalia sasa hili kundi lililoshiriki kumuua Dkt Magufuli lazima liwe na mkono wa chuma ili watu wa Falsafa ya Dkt Magufuli kama Waziri Mkuu, na makamu wa rais Dkt Mpango wawe nje kabisa ya utawala maana wanaamini wanaweza lipiza kisasi wakishika madaraka na ndiyo maana hata ndugai kwenye u spika alikuwa tishio ndiyo maana wamemuwahisha. Polepole naye ajiandae na akina Gwajiboy hili kundi huenda linawatafuta kuwaua
 
Tuliwaambia hapa, yajayo yanafurahisha ,na Bado August Ina mengi
Chawa mjiandae na Bado wengi wataondoka

Aliyewahi kuwa Spika na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia, leo Agosti 6, 2025, taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson imeeleza kuwa msiba umetokea Dodoma

Dkt. Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

WASIFU MDOGO WA JOB NDUGAI
Alizaliwa Januari 21, 1963 na kupata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)

Amekuwa Mbunge wa Kongwa kwa miaka 25 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Katika uongozi wake wa bunge, mambo kadhaa yameibua mjadala mkubwa ikiwemo sakata la wabunge 19 wa CHADEMA wanaodaiwa kuvuliwa uanachama wao, na kuhojiwa kwa baadhi ya wabunge akiwemo Josephat Gwajima na Jerry Muro kwa madai ya kushusha hadhi na heshima ya bunge.

Suala jingine ni kumtaka mmoja wa wabunge aliyedai amevaa nguo zisizo za staha kutoka ndani ya ukumbi wa bunge. Uamuzi huo ulikosolewa vikali, wakosoaji wakieleza kwamba vazi la mbunge huyo halikuwa na tatizo. Karibuni, amezua mjadala tena kwa kusema Tanzania haitakiwi kukopa ili kufadhili miradi ya maendeleo.

Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
 
Afadhali amefariki dunia. Huyu ni mmoja ya waliochangia kuharibu demokrasia ya nchi hii.
Gongo huwwaa unatumia?

Unaanzaje kufurahia kifo cha binadamu mwenzako mkuu ilihali hata wewe u marehemu wa badaye?
 
RIP Ndugai
Msalimie Magufuli kama mtaonana.
Mwambie Lisu bado yupo anashuhudia tu vifo vya watesi wake akiwa jela na zile haki zake za kibunge bado hawajampa
 
nadharia ya kijinga jinga ni huyu kauawa vita vya madaraka maana angerudi bungeni angeweza kushinda u spika halafu akaisumbua serikali iliyoko kwa madaraka. Na ukumbuke ndiye alipangwa kuwa presida baada ya jpm kwa katiba ya makamu hawezi kwa kupindua meza (kwa mujibu wa umbea wa foma cdf), mpango ulipogoma wakatafuta platfomu akajichanganya akaandikishwa barua ya kujihudhuru (alitaka kugoma malecela akamfuata akamuambia watakuua achia u spika-hii aliwahi share yeye mwenyewe marehemu ndugai), maana yake wale waliotaka kumuua akiwa spika endapo angekataa ndiyo hao hao waliommaliza now ili asije shindania u spika
Kuna shombo la hawala kwa gharama ya inachokitaka

Uaminifu ndio udhaifu
 
Yule Nabii kijana wiki iliyopita alitoa unabii wa nchi na moja ya mambo aliyoyatabiri ni kuhusu mjumbe aliyetumwa Dodoma akiwa na chupa yenye sumu ikimlenga kiongozi mstaafu wa ngazi za juu. Na akasema viongozi wawe makini. Je ndiyo hii alikuwa akitabiri?
Ni kweli alisema hivyo
 
Halafu Mzee Malecela na uzee wake uliokithiri yupo Hai

Daah
 
Huyu kwanza tujue alikua team gani? Zile mbili wahuni au Itifaki ya chama wakina polepole kuna mtu alitabiri uchaguzi ukifika kuna vigogo wengi wataondoka Tunaomba ule Uzi
 
Back
Top Bottom