mbotoro kivoi
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 2,018
- 3,009
Rest in peace
Aisee?! Ni jukumu la Serikali kujua kila ndugu wa matehemu wako wapi kila dakika ili ahabarihswe?! Kweli?Mimi nauliza kwa Nini familia zao upata taarifa za vifo vya ndugu zao kupitia mitandaoni?
Ndugu wa ndungai aliyeshinda nae kutwa nzima na jioni akasafiri kwenda Dodoma anasema jamaa alikuwa poa kabisa haumwi chochote waliwasiliana mpaka jioni lakini kujua km aliumwa saa ngapi na aliumwa Nini hajui KIMSINGI hapa mwili uchunguzwe
Ili pia lilitokea kwa familia ya Hayati Magufuli kwa Nini he awa viongozi wakiumwa ndugu zao hawaitwi mpk wafe?
Lissu wameshtukia yupo deathrow mpaka sasa nyumbu wamemtelekeza mahakamani anajitetea mwenyeweMangula Familia yake ilistukia tu kalazwa ICU
Walioko hapo kwa ndugai Twambieni kuna tukio kubwa
🙏🏽
Britanicca
Shule ya Msingi 1991-1997? Halafu UDSM mwaka gani?1989-1993?
Aliyewahi kuwa Spika na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia, leo Agosti 6, 2025, taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson imeeleza kuwa msiba umetokea Dodoma
Dkt. Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
WASIFU MDOGO WA JOB NDUGAI
Alizaliwa Januari 21, 1963 na kupata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.
Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).
Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).
Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)
Amekuwa Mbunge wa Kongwa kwa miaka 25 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.
Alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.
Katika uongozi wake wa bunge, mambo kadhaa yameibua mjadala mkubwa ikiwemo sakata la wabunge 19 wa CHADEMA wanaodaiwa kuvuliwa uanachama wao, na kuhojiwa kwa baadhi ya wabunge akiwemo Josephat Gwajima na Jerry Muro kwa madai ya kushusha hadhi na heshima ya bunge.
Suala jingine ni kumtaka mmoja wa wabunge aliyedai amevaa nguo zisizo za staha kutoka ndani ya ukumbi wa bunge. Uamuzi huo ulikosolewa vikali, wakosoaji wakieleza kwamba vazi la mbunge huyo halikuwa na tatizo. Karibuni, amezua mjadala tena kwa kusema Tanzania haitakiwi kukopa ili kufadhili miradi ya maendeleo.
Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).
Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.
Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
Na yeye aliepata idhini ya matibabu toka bungeni ndo kaondoka na wamemuacha walie mnyima matibabu ili afe..
kudadeki kifo kiboko...
Kifo ni kifo tu, msituletee vijidrama na taharukiWapumbavu sana hawa baadhi ya hawa wajinga wa Chadema kwahiyo kifo ni adhabu? Hapo ndipo Chadema wanakosa credibility kabisa
Aliyekuwa Spika wa Bunge la JMT, Job Ndugai hatunaye tena duniani.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi na kuwapa faraja ndugu, jamaa , taifa, na marafiki wote wakati huu wa msiba. Amina
Hata mhusika anaweza kusikia stori kuhusu maisha yake ambapo yeye mwenyewe hajawahi kupitia kabisa.Hahaha 😂 raha ya JF, aisee ukiwa kiongozi nadhani JF ni muhimu sana ili ujue mitizamo ya watu hata ukiwa rais naona ni jukwaa muhimu yaani hapa unaweza sikia story ambazo hakuna anayeweza kukuambia.