TANZIA GE2025 Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

TANZIA GE2025 Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kama hivyo ndivyo, wale watu waliomfukuza kwenye kiti cha uspika na kutaka kumuua iwapo angekaidi kuondoka, unadhani angegombea uspika tena awamu hii wangeshindwa kummaliza?

What is the difference? Aliona kugombea uspika wakati huu ni salama? Obviously NOT, haikuwa salama kabisa ndio maana wamemfyekelea mbali.

Kwanini hakulijua hilo? Siamini kama alikuwa mjinga kiasi hicho?

Probably he was blinded by some false assurances and promises?
Sure nadhani kundi lake la sukuma gang limezidiwa
 
Sana maisha mafupi dear
Enzi kile kigrocery pale makaburini kino kwa mzee maende sahv breakpoint,ndugai alikuwa anasogea sana wao wanatokea pale ndani mwembe jini kwenye zile ofisi,nkajuana naye na wkt huo nafanya clearing vijana wa mjini wkt huo tunatamba,nshamtolea gari zake kadhaa,mara ehh kawa mb mara spika 😄

Kifo kiboko ya mwanadam kweli

Ova
Dah tupo saa hz breaking point njoo ununue generator
 
Lissu yeye ataishi milele?
Hatoishi milel,ila dunia haitomuandika kwa uovu kama maccm yanavyoandikwa humu ikifa,angalia post tu za mitandaoni uone ndugai anavyoandikwa kwa uovu alioutenda.
 

Aliyewahi kuwa Spika na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia, leo Agosti 6, 2025, taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson imeeleza kuwa msiba umetokea Dodoma

Dkt. Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

WASIFU MDOGO WA JOB NDUGAI
Alizaliwa Januari 21, 1963 na kupata elimu ya msingi kutoka Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1991-1997. Alianza elimu ya Sekondari ya Kibaha mwaka 1978-1981 na kumalizia Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia 1982-1984.

Amesoma Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka kuanzia mwaka 1986-1988, kisha Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1989-1993).

Amesoma Post Graduate kutoka Chuo cha Kilimo nchini Norway kuanzia 1994-1995 na kusoma Shahada ya Umahiri kutoka chuo hicho (1995-1996).

Safari yake ya elimu iliishia Eastern and Southern African Management Institute ambapo alisoma Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (2005-2008)

Amekuwa Mbunge wa Kongwa kwa miaka 25 sasa (tangu mwaka 2000) na ameshika nafasi mbalimbali ndani ya kamati za bunge.

Alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge Novemba 17, 2015 baada ya kupata kura 254 kati ya 365, na mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA akipata kura 109, huku kura mbili zikiharibika. Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge tangu mwaka 2010.

Katika uongozi wake wa bunge, mambo kadhaa yameibua mjadala mkubwa ikiwemo sakata la wabunge 19 wa CHADEMA wanaodaiwa kuvuliwa uanachama wao, na kuhojiwa kwa baadhi ya wabunge akiwemo Josephat Gwajima na Jerry Muro kwa madai ya kushusha hadhi na heshima ya bunge.

Suala jingine ni kumtaka mmoja wa wabunge aliyedai amevaa nguo zisizo za staha kutoka ndani ya ukumbi wa bunge. Uamuzi huo ulikosolewa vikali, wakosoaji wakieleza kwamba vazi la mbunge huyo halikuwa na tatizo. Karibuni, amezua mjadala tena kwa kusema Tanzania haitakiwi kukopa ili kufadhili miradi ya maendeleo.

Mbali na ubunge, amefanya kazi sehemu nyinginezo ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Pori la Akiba Selous na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Januari 6, 2022 amejiuzulu nafasi ya Uspika kutokana na sababu binafsi na kwa hiari yake.

Ndugai ni mume wa Fatuma Mganga.
Bunge limevunjwa. Spika wa bunge katoka wapi?
 
Mwendo umeumaliza,Pumzika unapostahili Ndungai.Tuacheni kufuru kifo tumeumbiwa wanadam.Siku yako ikifika utaondoka tu.Hakuna atakayeishi milele.Punguzeni maneno makali kwa mwendazake.
 
Back
Top Bottom