John Heche amjibu Saada: Wazanzibari wanaoishi Tanganyika nao wanyimwe matibabu?

John Heche amjibu Saada: Wazanzibari wanaoishi Tanganyika nao wanyimwe matibabu?

Mambo yanazidi kuwa mengi.... Wazanzibari ni wabaguzi sana. Hawataki tumiliki ardhi Zanzibar, hawataki tufanyekazi Zanzibar, hawataki tutibiwe Zanzibar na mengine yanakuja soon.

Anaandika John Heche Makamu Mkiti Chadema.
==============

Huyu Saada Mkuya Salum amekua mbunge na waziri wa fedha huku bara.

Maneno muhimu kutoka kwako:

Unaelekeza mtu akienda hospital akitoa kitambulisho cha Taifa asitibiwe mpaka atoe cha Mzanzibari!!!! Ni mtu gani anaweza kuwa na kitambulisho cha Mtanzania lakini hana cha Mzanzibari?

Bila shaka ni mtu kutoka Tanganyika.

Umesema hatuna uwezo wa kutibu watu milioni 60 ambayo hiyo ni idadi ya Watanzania ambao wengi ni Watanganyika.

Je kuna siku wote wamevuka kuja kutafuta matibabu huko?

1. Saada unaweza kuwambia watu deni la Taifa ambalo kila mwezi tunalipa karibia trilioni moja na kadhaa ni kiasi gani kinatoka kwenye makusanyo ya Zanzibar?

2. Serikali za mitaa sio suala la muungano kwa katiba yetu,

Je unajua kuna wakurugenzi wa halmashauri za miji na majiji wameteueliwa kutoka Zanzibar huku Tanganyika?

Unajua kuna MADC wengi tu wameteueliwa kutoka Zanzibar wako huku bara?

Umefuatilia kwenye idara za madini, utaliii na wizara nyingi ambazo sio za Muungano kuna wakuu wa idara wangapi, wakurugenzi wa idara na maafisa wangapi kutoka Zanzibar?

Unataka Watanganyika wanaoishi huko wabaguliwe na wasipewe matibabu kwasababu ya kukosa kitambulisho cha Mzanzibari hata kama ana matibabu kadi ambayo ni sawa na bima ya afya….

Je Wazanzibari wanaoishi huku Tanganyika na wana bima za afya za NHIF nao wanyimwe matibabu?

Huyu ni waziri wa pili ndani ya mda mfupi kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya Watanzania wengine na..

Hakuna kauli yeyote kutoka kwa aliewateua, kwahiyo huu ndio msimamo wa ccm na ndio msimamo wa wateuzi wao.

Nani anaewatuma hawa kusema haya? Maana sio bahati mbaya… nani anaewatuma kuwabagua Watanganyika? := John Heche Makamu Mkiti CHADEMA.
Kumtetea bibi wa PhD ni kazi sana.
 
Heche hata Zanzibar haijui, anakwenda mchana anarudi na ndege ya jioni. Hajui hata maisha ya Wazanzibari. 55 % ya masheha zanzibar inawezekana ni Watanganyika.
Mabolozi wa nyumba 10 inawezekana 60% ni ya Watanganyika.
Wanaomiliki mashamba inawezekana 20% ni watanganyika.
Kinachowasumbua wengi humu ni UDINI.
Hahaaa we jamaa kila siku unazidi kuonesha uhalisia wako. Umekuwa wa kwanza kuleta udini ktk maandishi yako halafu unamlaumu mtu mwingine. Kikubwa watu Sasa hivi wengi hasa vijana wamesoma na kuelewa huu ujinga wenu wa miaka mingi jinsi mlivyokuwa mnawechezea wazee wetu na hilo tishio lenu la udini hivi udini vile now we see your true colours.
 
Wanakuwaje watanganyika wakati wana vitambulisho vya ukaazi wa zanzibar, means ni wazenj. Au wewe unazungumzia asili yao?

Ukisema ufate asili tuu kuhalalisha utanganyika ndani ya zanzibar unafeli sana, maana hata katika nchi tunazopakana nazo Kuna wamasai ni wakenya, wamakonde ni wamsumbiji, wahaya ni wanyarwanda nk.

Ukishakuwa na kitambulisha Cha ukaazi wa zanzibar wewe sio mtanganyika hata kama babu zako walitoka mkuranga kama rais mwinyi.
iweje wajitenge wakati wakiwa Tanganyika hawatengwi wanapewa haki sawa na watanganyika
 
Heche hata Zanzibar haijui, anakwenda mchana anarudi na ndege ya jioni. Hajui hata maisha ya Wazanzibari. 55 % ya masheha zanzibar inawezekana ni Watanganyika.
Mabolozi wa nyumba 10 inawezekana 60% ni ya Watanganyika.
Wanaomiliki mashamba inawezekana 20% ni watanganyika.
Kinachowasumbua wengi humu ni UDINI.
Uchoyo ubinafsi cha watanganyika ni cha wote lakini cha mzanzibar ni chake binafsi hayo ndiyo maajabu na ujinga mkubwa pato kubwa la Tanganyika ndilo linailea kuilisha Zanzibar lakini wakishashiba wanaanza ubaguzi
 
iweje wajitenge wakati wakiwa Tanganyika hawatengwi wanapewa haki sawa na watanganyika
Wakiwa Tanganyika hawabaguliwi lakini wakiwa Zanzibar wanakuwa wabaguzi kama Africa kusini, sasa wanang’ang’aniza ajila mahotelini wapewe wao wakati wamiliki wa Mahoteli wanaangalia utashi wao wanajua wazanzibar siyo smart idara hizo hawajui kazi ni wavivu na wabishi sana
 
Heche hata Zanzibar haijui, anakwenda mchana anarudi na ndege ya jioni. Hajui hata maisha ya Wazanzibari. 55 % ya masheha zanzibar inawezekana ni Watanganyika.
Mabolozi wa nyumba 10 inawezekana 60% ni ya Watanganyika.
Wanaomiliki mashamba inawezekana 20% ni watanganyika.
Kinachowasumbua wengi humu ni UDINI.
Ficha ujinga wako.
 
mimi ni mtanzania, sina vyama kwani uchaguzi ulishaisha,na yaliyopita si ndwele sasa tunaganga yaliyopo. Mimi nahoji as mtanzania ambaye naona kabisa kuwa hizi kauli zinatugawa watanzania. Mambo ya vyama nawaachia wakereketwa waliomo ndani ya vyama. Hili suala linawagusa watanzania wote,wazanzibar,watanganyika,wana ccm,wanachadema,wasukuma,wapemba,wanamwanza wanadaslam na yeyote yule anayeitwa mtanzania.
Aliyeanza ubaguzi ni mzanzibar na aliyemjibu kutaa huo ubaguzi ni Mtanganyika sasa hapo shida ipo wapi? Wewe kataa ubaguzi wa kijinga ndipo utaonekana mungwana
 
Hizi kauli toka kwa viongozi waandamizi wa Taifa la Zanzibar siyo za bahati mbaya, ukweli ni kuwa hawa watu wamejiandaa ifikapo 2030 mwenzao akimaliza term yake huku Tanganyika na muungano unakoma. Kauli hizi zina baraka zote za Mwenzao anayetawala huku bara na kipindi hiki tutashuhudia Zanzibar ikijengeka kwa kasi ya ajabu kwa kodi za Watanganyika, Yote haya wameyataka wahafidhina wa CCM waliokataa muundo wa serikali tatu sasa hizi serikali mbili ndiyo zimetoa mwanya kwa wazenji kututawala kila nyanja , hata Waziri wa Fedha kuteuliwa Mzanzibari ni katika mkakati wao. Watanganyika tujitafakari jee CCM inatutendea haki kutuwekea Rais asiye wa damu yetu Watanganyika?
Cha mzanzibar ni chake lakini cha Mtanganyika ni cha wote
 
Huo ndiyo ujumbe wa Samia, jana meli ya mafuta imetoka moja kwa moja toka Oman muda mfupi tu mafuta yatauzwa sh. 2000 kwa lita moja, Samia ni shetani na jambazi wa Tanganyika
 
Heche hata Zanzibar haijui, anakwenda mchana anarudi na ndege ya jioni. Hajui hata maisha ya Wazanzibari. 55 % ya masheha zanzibar inawezekana ni Watanganyika.
Mabolozi wa nyumba 10 inawezekana 60% ni ya Watanganyika.
Wanaomiliki mashamba inawezekana 20% ni watanganyika.
Kinachowasumbua wengi humu ni UDINI.
Wewe nae ndio mjinga kbs kwanza unaongea mamb ya kuhisi tu, eti inawezekana inawezekana inawezekana my foot!! Njoo na facts ya kutetea hoja yako!
 
Back
Top Bottom