John Heche anafaa kuwa Katibu Mkuu CHADEMA Taifa, John Mnyika ni dhaifu sana

mkitaka chama kife, mpeni Heche uongozi wa juu. Mkurupukaji yule. na elimu hana. Mnyika ndo anafaa kuwa mwenyekiti ajae. Unafikiri wasomi watakubali kuwa chini ya Heche? Heche aendelee kuwa mpiga debe wa chama.
 
Mnyika ni dhaifu ajawahi kutana na mkono wa dikteta,Heche ni mwanaume wa mapambano
 

Ccm sio chama cha siasa, kimevaa koti la dola. Leo hii ccm ikipoteza dola Kaburi lake litakuwa pembeni ya la KANU ya Kenya. Serekali inaendeshwa kwa kodi za nchi, kwa bahati mbaya serekali ndio mnaifanya ni ccm.
 
mkitaka chama kife, mpeni Heche uongozi wa juu. Mkurupukaji yule. na elimu hana. Mnyika ndo anafaa kuwa mwenyekiti ajae. Unafikiri wasomi watakubali kuwa chini ya Heche? Heche aendelee kuwa mpiga debe wa chama.
unamuogopa
 
shallow reasoning, bila polisi CCM ni kama karatasi! Hao ndio unasema CDM itachukua miaka 100? CCM inasimama kwa nguvu za polisi, siyo UMMA!
Nadhani polisi itakuwepo ata miaka 200 ijayo labda jeshi Hilo litungiwe Sheria ya kufutwa na Bunge la JMT lenye wabunge Zaid ya 90% wa CCM
 

Toka wakati wa uchaguzi nilisema kuwa Mnyika amepooza sana, hafai kwenye nafasi ya katibu Mkuu. Nilipendekeza Marcus Albanie apatiwe nafasi hiyo, na mwenyekiti wa chama awe John Heche.
 
Nadhani Mdee alifaa kwenye hiyo nafasi, tukiacha madhaifu yake mengine
 
Paka anamshauri Panya jinsi ya kujikinga dhidi ya maadui zake
 
Kwani Magufuli asingekufa Samia angekuwa mwenyekiti sasa hivi ?

Lini CCM imeacha kutumia mabavu iliyokuwa inayatumia chini ya Magu ?
Mnayoyafanya CDM kwa sasa msingeweza kufanya kipindi cha Magufuli, ila sidhani kama ni jambo baya pia, Mahakama iachiwe ifanye kazi yake, Mbowe kama hana makosa ataachiwa, utawala huu hautamuonea mtu, BTW CDM kwa sasa badilini ajenda zenu, Samia ni mtu poa sana kuwasaidia kujenga chama chenu kiwe chama cha upinzani wa kudumu, hizi siasa za piga nikupige hazitowafikisha popote
 
ubunge mtamu sana, baada ya kupigwa chini sasaivi anatafuta kazi. siasa hizi kumbe watu ukiona wana hasira wanaleta fujo nchini ni kwamba wanatafuta kula.
 
Ccm sio chama cha siasa, kimevaa koti la dola. Leo hii ccm ikipoteza dola Kaburi lake litakuwa pembeni ya la KANU ya Kenya. Serekali inaendeshwa kwa kodi za nchi, kwa bahati mbaya serekali ndio mnaifanya ni ccm.
Unahitaji elimu ya siasa. Kazi ya chama cha siasa ni kupata ridhaa ya wananchi na kuwawakilisha kwenye mijadala ya kitaifa. CDM ilicheza karata mbaya tokea 2018 ilipoamua kuanza kususia chaguzi kwa kisingizo cha eti CCM inatengeneza matokeo, mbona huko nyuma mlikuwa mnashida. Inawezekana vipi leo hii CDM inaibuka na kusema inawakilisha wananchi ambao hajawapa dhamana ya kuwakilisha? Hata kukutana na Mama, ni kwa hisani yake tuu maana hawawezi kusema tunapeleka malalamiko ya wananchi ambao hajawapa ridhaa yayote.
 
CCM, Mkuu.
Nielimishe kwa kunitajia achievements za Dr. Slaa na kwa nini anastahili hiyo title unayompa.

Amandla...

Mimi tangu multiparty system ilipoanza nilikoma kuwa mwanachama wa CCM na nikabaki bila affiliation na chama chochote.

Swali nililokuuliza hujalijibu, Mkuu!
 
Mawazo yangu ni kua sioni kama Chadema ni chama cha Upinzani Tanzania. Isipokua Nakiona Kama Kikundi Cha Wanaharakati Chenye Mlengo Wa Kugain Popularity. Nimesema Ni Mawazo Yangu Tafadhali.
 
Mimi tangu multiparty system ilipoanza nilikoma kuwa mwanachama wa CCM na nikabaki bila affiliation na chama chochote.

Swali nililokuuliza hujalijibu, Mkuu!
Nyie ndio non aligned mliokuwa aligned?
Swali gani hilo Mkuu. Nikumbushe.

Amandla...
 
Mimi tangu multiparty system ilipoanza nilikoma kuwa mwanachama wa CCM na nikabaki bila affiliation na chama chochote.

Swali nililokuuliza hujalijibu, Mkuu!
Nilikuuliza unitajie vitu vinavyokufanya uamini kuwa alikuwa effective ili tutumie kigezo kimoja kuwapima.

Amandla...
 

Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu. Naona unazungumza inavyotakiwa kuwa na sio ilivyo. Hiyo kupata nguvu ya kuongea kutoka kwa wananchi ni iwapo uchaguzi unaheshimiwa, na sio yale maagizo aliyotoa Magufuli kwenye uchaguzi. Huko nyuma unapozungumza ccm walikuwa wanapita zaidi ya 30% bila kupingwa? Huko nyuma ulikuwa unakuta Karatasi la kura rais aliye madarakani jina lake linakuwa juu bila kufuata alphabet za chama? Huyo mama hana hisani yoyote anatoa maana anajua fika hakukuwa na uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…