John Heche anafaa kuwa Katibu Mkuu CHADEMA Taifa, John Mnyika ni dhaifu sana

Kama kuwa nonaligned means kutokuipinga CHADEMA basi kweli nitakuwa aligned!

Swali ni hili: Nani amewahi kuwa KM katika Kambi ya Upinzani, ambaye ni more effective kuliko Dr. Slaa?
Jibu. Define effectiveness.

Amandla...
 
Messaging consistency.

Tangu aondoke Dr. Slaa, imekuwa vigumu sana kujua CHADEMA inasimamia kitu gani.
Mabadiliko ya kisera ambayo wamegundua hayatatokea bila Katiba Mpya. Wanataka watu wawe na uhuru wa kutoa maoni yao na kuhoji serikali yao. Aidha, wanataka uchumi unaoongozwa na sekta binafsi.

Amandla...
 
Wewe lidogi la ccm lakini umenena, Mnyika hana hamasa wala mvuto, ni mpayukaji.
Kuweka rekodi sawa, Mashinji ndiye katibu dhaifu kuwahi kutokea.
 
Mabadiliko ya kisera ambayo wamegundua hayatatokea bila Katiba Mpya. Wanataka watu wawe na uhuru wa kutoa maoni yao na kuhoji serikali yao. Aidha, wanataka uchumi unaoongozwa na sekta binafsi.

Amandla...

Katiba Mpya inayokubalika na CHADEMA? Obviously, CHADEMA is delusional.

Let’s be realistic here! CHADEMA wanapata wapi tumaini la kupata aina ya katiba wanayoitaka ilihali hawana kura za kutosha kwenye Bunge la Kawaida na Bunge Maalumu la Katiba linaloweza kuitishwa?

It’s impossible! Sana sana watapiga billions za pesa ya walipakodi kisha wasusie vikao vya Bunge kama walivyofanya 2015. Je, kweli sisi walipakodi wa Tanzania ndiyo tunataka hii biashara kichaa?
 
Unatumia nguvu nyingi kubadilisha mwenendo wa huu uzi, uzi umetoa maoni ya mabadiliko ya uongozi wa juu wa CDM. Kitu ambacho kundi dogo ndani ya CDM ambalo ni la kaskazini wanapinga vikali.

Ungekuwa wa maana kama ungeweza kutufafanulia CDM itaendeleaje bila Mbowe kuwepo madarakani? Maamuzi ya na mwekeko wa chama utatolewa na nani. Kusema fulani ni mjinga au ni propaganda hakujibu hoja ya Mbowe is not CDM's future.
 
Katiba iliyokuwepo ni ya TANU na CCM. Chadema wanachodai ni Katiba itakayopata baraka na wananchi sio wabunge.
Na kuhusu uwakilishi wao bungeni hawatakubali ipitishwe na bunge ambalo hawana imani nalo.
Wapinzani walitoka katika bunge la Katiba baada ya CCM kutaka kuibadilisha ifanane na hii ya sasa.
Let's be honest. The only reason CCM hawataki Katiba Mpya ni kwa sababu wanajua pakiwa na level playing ground wataondoka. Na Chadema wameonyeshwa katika miaka 6 hii jinsi Katiba iliyopo inakipa chama tawala uwezo wa kufanya lolote watakalo bila repercussions zozote. Kwa hiyo it is insanity kutegemea mpinzani yeyote anayejitambua atakubali kuingia katika uchaguzi wowote chini ya Katiba iliyopo.

Mpira upo kwenu, mtangaze kuwa tumekuwa de facto one party state na tuachane na charade za uchaguzi, badala yake tukubaliane tu kuwa Mwenyekiti wa Chama Tawala ndie Rais wa nchi yetu. Sidhani kama hii scenario mtaipenda ndio maana mmechukua extraordinary measures kuhakikisha kuwa bungeni kuna wabunge wasio wenu.

Btw, nani amesema ni lazima kuwa na Bunge la Katiba ili tupate Katiba Mpya?

Amandla...
 
Swali lako halina maana. Miezi 9 iliyopita wengi tuliamini Bawacha bila Halima Mdee haiwezekani. Mbowe asipokuwepo atapatikana mwingine na chama kitaendelea kuwepo.

Amandla...
 
Swali lako halina maana. Miezi 9 iliyopita wengi tuliamini Bawacha bila Halima Mdee haiwezekani. Mbowe asipokuwepo atapatikana mwingine na chama kitaendelea kuwepo.

Amandla...
Mbowe sio Halima Mdee, Halima hajawahi kuwa mwenyekiti wa halmashauri kuu au kamati kuu au hata vikao vikuu vya kitaifa vya chama. Haja wahi kupitisha ajenda yoyote au bajeti yoyote ya chama. Je hivyo vikao nani anakaimu hivi sasa? Na kama mbowe akiwa ndani zaidi ya mwaka, kaimu ana nguvu ya kubadilisha mwelekeo wa chama au kuja na ajenda mapya?
 
Nilimwona jana nje ya mahakama Kisutu akaulizwa mbele ya TV camera za dunia, unasemaje kuhusu waliokamatwa leo nje ya mahakama, akasema cha msingi ni kuhimizana tuje tena kesho.

Angekuwa Heche hapo angewavua nguo Kamanda Sirro, Muriro na Mama yao
 
huelewi nini hapo sasa? heche ni kiongozi shupavu mbali sana ukilinganisha na hiko kimnyika. ila mbowe a.k.a mr haambiliki hataki mtu wa kum-challenge. ndo maana akakaweka hako kajamaa ka "ndio mzee". mimi sio fan kabisa wa chadema hii ya akina mbowe ila nikiweka ushabiki wangu pembeni heche ilimfaa sana hiyo nafasi, mwengine labda msigwa. hawa wangeweza kuitendea haki hiyo nafasi.
 

Cdm ingekuwa imepoteza mwelekeo, serekali kupitia maagizo ya ccm isingetumia nguvu ya vyombo vya dola kufanya haya wanayoyafanya sasa. Sidhani kama unaongelea cdm, labda unazungumzia TLP au UDP.
 
Wote ni viongozi. Sasa hivi Chadema inaongozwa na Makamu Mwenyekiti. Na kwa nini kiongozi mpya abadilishe muelekeo wa chama chake wakati atatokea ndani ya chama hicho hicho? Mbona Rais Samia Hassan hajabadilisha muelekeo wa chama chake na serikali yake? Kwa nini iwe tofauti kwa Chadema? Mbowe sio Mwenyekiti wa kwanzs wa Chadema. Alipokea chama kwa mwengine na yeye atapokelewa hivyo hivyo.

Amandla...
 
Mnyika amekuwa Naibu katibu mkuu chini ya Dk Slaa na Mashinji kipindi hicho Heche akiwa mwenyekiti wa BaVICHA wewe huoni hiyo ilikuwa succession plan nzuri.?

By the way mimi pendekezo langu toka 2019 ilikuwa Marcos Albanie ila kwa muda sasa hajihusishi na active politics but he is a nice pick.
 

Mkuu, Katiba Mpya haitapatikana kwa azimio la CC ya CHADEMA. Process ya kufanya mabadiliko ya Katiba inasimamiwa na Bunge la JMT kupitia sheria ya Bunge inayotungwa kwa ajili hiyo.

CHADEMA wamepata wapi kura Bungeni za kuwawezesha kutunga sheria itakayosimamia mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwa namna wanayotakata wao? Ndiyo maana nakuambia CHADEMA watapiga pesa kisha wasepe bila Katiba Mpya kupatikana, kama walivyofanya 2015!

BTW, kweli sikubaliani na CHADEMA katika maeneo mengi, lakini mimi sio CCM wala Serikali ya CCM. Naona unanijibu kama vile unaijibu CCM au Serikali ya CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…