John Heche: Magufuli aliniahidi kunipa nafasi ya Uwaziri kama ningekubali kuhamia CCM

Dah!......
 
Heche anafanya upumbavu tuu, Sasa mtu alishakufa angenyamaza tuu hakuna namna ya kuthibisha au kukanusha. Yeye anagombea mwakani hilo ndo la msingi.
Hawa wanaomuongelea mtume Hadi sasa kwani kafufuka? Kila siku tunasikia habari za kina Nyerere, Mandela, Mkapa, Mwinyi nk, kwani wao wako hai?
 
hii haiko sawa hata kidogo
upinzani mbinu mnazotumia ni za kitoto onnyesheni ukomavu walau
 
Hivi ni Vitu vya kawaida tu katika uwanja wa Siasa. Hiyo kwa king-eleza inaitwa political maneuvering

Yakujiuliza, Kwani Hayat Rais Magufuli alivunja sheria gani? Yeyote ile?

Heche anatafuta kiki tu kutaka kuonyesha kwamba alikuwa anahongwa(rushwa), wakati kiuhalisia sera za Hayat Rais hazikupishana sana na zile za J.Heche. Wote walikuea wakipigania Rasilimali za Mtanzania.
 
Heche anafaa kuwa Mwenyekiti wa CDM baada ya Mbowe
 
Usiamini kila kitu kinachosemwa na wanasiasa. Yaani kusema tu hivyo tayari umeamini kuwa Heche alikuwa approached kuhamia Ccm. Bado safari yetu kama taifa ni ndefu sana
 
Magu alitaka wafanya kazi ndio maana ukiangalia wabunge wake wakuteuliwa ndo walipewa vyeo kuliko wale wa muda mrefu hivyo sio jambo baya aliona unaweza kazi akataka kukuteua ila hawez kutoa nje ya mfumo sasa
 
Heche anafanya upumbavu tuu, Sasa mtu alishakufa angenyamaza tuu hakuna namna ya kuthibisha au kukanusha. Yeye anagombea mwakani hilo ndo la msingi.
Ukinyamaza wewe inatosha, waache wenye uwezo wa kusema maovu ya Magufuli wayaseme. Kusema kuwa tuwaache waliokufa wapumzike kwa vile wamekufa ni hoja dhaifu. Hata ukifa lazima tukosoe matendo yako maovu.

Mbona hujajiuliza kwa nini Mkapa au Mwinyi hawaandikwi humu? Ni kwa vile walitenda yaliyo mema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…