Kumetokea malumbano makali kati ya John Heche [M/Kiti - CHADEMA - kanda ya Serengeti] na Dr W. P. Slaa [Former GS wa CHADEMA] huko club house moja usiku wa kuamkia leo..
Msingi wa malumbano ni hoja ya Dr Slaa aliyowahi kuiibua na kuripotiwa hapa kuhusu UTEKAJI, KUPOTEA KWA WATU na KUPIGWA RISASI 37 kwa Tundu Lissu Septemba, 2017..
Hoja ni kina nani wanahusika?
Dr. SLaa katika maelezo yake, kwa mbaaali [japo jana amekanusha na kudai ameeleweka vibaya] ameonesha kuwa hiyo yaweza kuwa ni INSIDE JOB ya CHADEMA wenyewe kuwa WANAJITEKA, WANAPOTEZA NA na KUJIPIGA RISASI wenyewe kwa wenyewe.
Kwa kujaribu kuthibitisha hili, Dr Slaa anatoa mfano wa M/Kiti wa CHADEMA (W) fulani miaka hiyo kutekwa na kupigwa kisha kutupwa porini akiwa mahututi na watekaji hao wanaamini kubwa amekufa..
Few hours later, victim huyo alipata fahamu na baadaye taarifa kumfukia GS Dr Slaa by then. Kwa maelezo ya Dr Slaa, kitambo kidogo baadaye mmoja wa walinzi wa chama chao [Red Brigade] alijitokeza mbele ya Dr Slaa na kukiri kuwa yeye ni mmoja waliohusika kumteka m/kiti huyo.
Sasa mpaka hapo ndipo John Heche, ame - react na kumpinga vikali Dr Slaa. Na akathubutu kumwita his former Party GS kuwa mwongo. Anamuona Dr Slaa ni kama mtu aliye kwenye confusion ya aina fulani hivi. Anauliza yeye kama GS ikawaje kwa miaka zaidi ya 15 sasa anyamazie jinai hiyo na kuisema leo..?
Kwa ku - react shutuma za John Heche, Dr Slaa akajibu kuwa, hajaeleweka na watu wanapotosha kwa makusudi na mantiki ya hoja yake kwa sababu hajasema kuwa CHADEMA wanajiteka, kujipoteza na kupigwa risasi kwa TL ni INSIDE JOB ya CHADEMA yenyewe..!
Dr Slaa, akarejea tena kwenye tukio la M/Kiti wake wa CHADEMA (W) kutekwa. Akasema yeye kama GS kisheria siyo jukumu lake kushughulikia jinai kama ile. Anasema, yeye alipopata taarifa hiyo kazi yake ilikuwa ni kuipeleka polisi na ndivyo alivyofanya..
Anaendelea kusema kuwa hadi leo, hajui uchunguzi wa polisi kwa tukio hilo uliishia wapi kwa sababu mpaka anatoka ofisini, hakuwahi kuitwa polisi wala kuitwa kuwa shahidi ktk mahakama yoyote kwa kesi hiyo...!!
MAONI YANGU:
Baada ya kauli hii ya jana ya Dr Slaa, kidogo mimi ilinifungua macho na ufahamu wangu. Nikaanza kumwelewa Dr Slaa. Kumbe ni kweli kabisa kuwa hakuwa na maana ya CHADEMA huwa wanajiteka, kujipoteza wenyewe na kwamba, ndiyo walimpiga risasi TL mwaka 2017..!
KUMBE TUSEMEJE SASA..?
✓ Hii ni vita ya kisiasa ya siku zote kati ya CCM na CHADEMA..
✓ Bahati mbaya sana, baadhi ya maafisa wa UWT na Polisi wamekubali kuzichafua taasisi hizi muhimu kwa amani na utulivu wa taifa hili kwa kushiriki ktk michezo hii michafu ya kisiasa ya wanasiasa. Victim mkuu wa mchezo huu mchafu basically ni CHADEMA huku CCM ikidhani inanufaika..
✓ Hawa UWT na POLISI kwa kuagizwa na kutumwa na wanasiasa walio serikali, hutengeneza matukio ya kijinai kwa jina la CHADEMA ili ku - tarnish image ya chama hiki na baadaye waki - incriminate na kisha wapate sbb ya kukifuta. Tukio la juzi kati hapa la kesi ya M/Kiti wa CHADEMA Taifa ndg Freeman Mbowe iliyojifuta yenyewe kwa kukosekana ushahidi ni mfano halisi na rahisi kabisa wa kesi ya kutengenezwa na baadhi wa maafisa wa UWT na POLISI..
✓ Kwa sababu, hebu tujiulize swali hili la msingi, kwamba, kama hizi ni INSIDE JOB ya CHADEMA, ni sababu gani inayowafanya polisi wasiingie huko CHADEMA, wakachunguza na kuwatambua wahusika na kisha kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria iwapo kweli hawa huwa wanajiteka, kujipoteza na ndiyo walihusika kumpiga mwenzao Tundu Lissu risasi mwaka 2017..?
✓ Kwanini tukio la M/Kiti wa CHADEMA (w) anayetolewa kama reference example na Dr Slaa ripoti yake kwa zaidi ya miaka 15 imefichwa, hazitolewi hadharani na polisi ili kuthibitisha kuwa CHADEMA walimteka na kumpiga mtu wao wenyewe?
✓ Je polisi, wanaiogopa CHADEMA? Je, CHADEMA hawachunguziki wala kukamatika?
KAMA MAMBO YAKO HIVI, TATIZO LIKO WAPI SASA..?
✓ Tusimung'unye maneno, "Pandora box ☑️ ", ndiyo inafunguliwa taratibu na akina Dr Slaa. Tatizo liko kwenye serikali kupitia idara za UWT na POLISI. Hawa, baadhi ya maafisa wake wanalipwa na wanasiasa wa chama tawala kuliharibu taifa hili kwa kushiriki siasa chafu za CCM...
✓ SAMAKI mmoja akioza, kikawaida uozo huo huambukizwa box au tenga lote la samaki wote huonekana wameoza. Idara za UWT na POLISI zimeoza na ni lazima mabadiliko ya kimfumo na kisheria ufanyike ili kulinusuru taifa hilikuishia kwenye machafuko...!
Sasa namwelewa Dr Slaa. Mfano wake ule, alikuwa anajaribu kutuonesha tatizo liko wapi..