John Heche vs Dkt. Slaa: Je, ni kweli utekaji, kupotea kwa watu na kupigwa risasi Tundu Lissu Septemba, 2017 ni 'INSIDE JOB' ya CHADEMA wenyewe?

Pangueni hoja zake!

Kwanini hamtaki kujibu hoja zake badala yake mnashambulia maisha yake binfsi
Labda uwe punguani pekee ndio utaamini maneno ya slaa, punguani ujibiwa kipunguani.
Kwa akili yako tu,slaa anamaanisha chadema ipo juu ya Sheria
 
Ni malumbano makali kati ya John Heche [M/Kiti - CHADEMA - kanda ya Serengeti] na Dr W. P. Slaa [Former GS wa CHADEMA] huko club house moja usiku wa kuamkia leo Alhamisi trh 28/4/2022..

Msingi wa malumbano hayo ni hoja ya Dr Slaa aliyowahi kuiibua na kuripotiwa hapa hapa JF kuhusu UTEKAJI, KUPOTEA KWA WATU na KUPIGWA RISASI 37 kwa Tundu Lissu Septemba, 2017..

Hoja inayoleta majadala ni kina nani wanahusika na jinai hii ya kupoteza na kuua watu kwa style mbalimbali? Na ni kina nani hasa walihusika na jaribio la kuuwawa kwa risasi Tundu Lissu mwaka 2017? Nini wajibu wa polisi? Kwanini haya yanatokea nao wakiwepo tu?

Dr. SLaa katika maelezo yake, kwa mbaaali [japo jana amekanusha na kudai alieleweka vibaya] ameonesha kuwa hiyo yaweza kuwa ni INSIDE JOB ya CHADEMA, kwamba ni wenyewe WANAJITEKA, KUPOTEZANA na KUJIPIGA RISASI wenyewe kwa wenyewe. Na obviously, ndiyo walimpiga risasi Tundu Lissu mwaka 2017..!

Kuthibitisha hili, Dr Slaa anatoa mfano wa M/Kiti wa CHADEMA (w) fulani miaka hiyo, kwamba, alitekwa na kupigwa kisha kutupwa porini akiwa mahututi na watekaji hao wakaamini kuwa amekufa..

Lakini few hours later, victim huyo alipata fahamu na baadaye taarifa kumfikia yeye Dr Slaa by then akiwa ndiye GS..

Kwa maelezo ya Dr Slaa kwa niaba ya chama, alitoka public na kulaani tukio hilo. Lakini kitambo kidogo baadaye mmoja wa walinzi wa chama chao [Red Brigade] alimwendea Dr Slaa na kukiri kuwa yeye ni mmoja waliohusika kumteka m/kiti huyo..!!

Sasa mpaka hapo ndipo John Heche, aka - react na kumpinga vikali Dr Slaa. Heche akamwita his former Party GS kuwa huo ni uongo na anamuona Dr Slaa ni kama mtu aliye kwenye confusion ya aina fulani hivi..

Heche akamuuliza Dr Slaa, kuwa, kama ni kweli, yeye akiwa kama GS wa chama by then, ikawaje kwa miaka zaidi ya 15 sasa anyamazie jinai hiyo na kuisema leo..?

Dr Slaa akajibu tuhuma hizo za Heche kwa kusema, ni wazi kuwa hajaeleweka na watu wanapotosha kwa makusudi mantiki ya hoja yake kwa sababu hajasema kuwa CHADEMA wanajiteka, kujipoteza. Na hajasema kuwa, kupigwa risasi kwa Tundu Lissu ni INSIDE JOB ya CHADEMA yenyewe..!

Dr Slaa, akarejea tena kwenye tukio la M/Kiti wake wa CHADEMA (W) kutekwa. Akasema yeye kama GS kisheria siyo jukumu lake kushughulikia jinai kama ile. Anasema, yeye alipopata taarifa hiyo kazi yake ilikuwa ni kuipeleka polisi na ndivyo alivyofanya..

Dr Slaa akaendelea kujitetea kwa kusema kuwa hadi leo, hajui uchunguzi wa polisi kuhusu tukio hilo uliishia wapi kwa sababu mpaka anatoka CHADEMA, hakuwahi kuitwa polisi wala kuitwa kuwa shahidi ktk mahakama yoyote kwa kesi hiyo...!!

MAONI YANGU:

Baada ya kauli hii ya jana ya Dr Slaa, kidogo mimi ilinifungua macho na ufahamu wangu. Nikaanza kumwelewa Dr Slaa. Kumbe ni kweli kabisa kuwa hakuwa na maana ya CHADEMA huwa wanajiteka, kujipoteza wenyewe na kwamba, ndiyo walimpiga risasi TL mwaka 2017..!

Ni wazi kuwa kumbe Dr Slaa alikuwa anatufungua ufahamu na akili zetu ili kujua tatizo la haya mambo liko wapi. Kwamba, kiini cha tatizo la kupotea, kutekwa watu liko ndani ya serikali kupitia TANPOL na UWT wakichezeshwa mchezo mchafu wa kisiasa na wanasiasa watawala wa CCM kwa maslahi ya kisiasa..!!

KUMBE TUSEMEJE SASA..?

✓ Hii ni vita ya kisiasa ya siku zote kati ya CCM na CHADEMA..

✓ Bahati mbaya sana, baadhi ya maafisa wa UWT na Polisi wamekubali kuzichafua taasisi hizi muhimu kwa gharama ya amani na utulivu wa taifa hili kwa kushiriki ktk michezo hii michafu ya kisiasa ya wanasiasa. Victim mkuu wa mchezo huu mchafu basically ni CHADEMA huku CCM ikidhani inanufaika..

✓ Hawa UWT na POLISI kwa kuagizwa na kutumwa na wanasiasa walio serikalini, hutengeneza matukio ya kijinai kwa jina la CHADEMA ili ku - tarnish image ya chama hiki na baadaye waki - incriminate na kisha wapate sbb ya kukifuta. Tukio la juzi kati hapa la kesi ya M/Kiti wa CHADEMA Taifa ndg Freeman Mbowe iliyojifuta yenyewe kwa kukosekana ushahidi ni mfano halisi na rahisi kabisa wa kesi ya kutengenezwa na baadhi wa maafisa wa UWT na POLISI..

✓ Kwa sababu, hebu tujiulize swali hili la msingi, kwamba, kama hizi ni INSIDE JOB ya CHADEMA, ni sababu gani inayowafanya polisi wasiingie huko CHADEMA, wakachunguza na kuwatambua wahusika na kisha kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria iwapo kweli hawa huwa wanajiteka, kujipoteza na ndiyo walihusika kumpiga mwenzao Tundu Lissu risasi mwaka 2017..?

✓ Kwanini tukio la M/Kiti wa CHADEMA (w) anayetolewa kama reference na Dr Slaa ripoti yake kwa zaidi ya miaka 15 imefichwa, hazitolewi hadharani na polisi ili kuthibitisha kuwa CHADEMA walimteka na kumpiga mtu wao wenyewe?

✓ Je polisi, wanaiogopa CHADEMA? Je, CHADEMA hawachunguziki wala kukamatika?

KAMA MAMBO YAKO HIVI, TATIZO LIKO WAPI SASA..?

✓ Tusimung'unye maneno, "Pandora box ☑️ ", ndiyo inafunguliwa taratibu na akina Dr Slaa. Tatizo liko kwenye serikali kupitia idara za UWT na POLISI. Hawa, baadhi ya maafisa wake wanalipwa na wanasiasa wa chama tawala kuliharibu taifa hili kwa kushiriki siasa chafu za CCM...

✓ SAMAKI mmoja akioza, kikawaida uozo huo huambukiza box au tenga lote na samaki wote huonekana wameoza. Idara za UWT na POLISI zimeoza na ni lazima mabadiliko ya kimfumo na kisheria ufanyike ili kulinusuru taifa hili kuishia kwenye machafuko...!

Sasa namwelewa Dr Slaa na mfano wake ule. Kumbe alikuwa anajaribu kutuonesha tatizo liko wapi. Yeye siyo tatizo kwa kusema haya. Na wala CHADEMA siyo tatizo hata kidogo.
Hebu pitia link hiyo hapo chini. Ndipo utagundua Slaa kasema uongo au ukwel Joseph Yona Mwenyekiti wa chadema wilaya Temeke na Mjumbe wa Baraza kuu aliyetwkwa ameeleza waliomteka. Halafu wewe unaleta poroja ana assumptions wakati kuna facts!!!
Nawashauri vijana mkae kimya msimbagaze huyo Slaa.
Alikuwa SG CHADEMA
Anajua mengi ya chadema enzi zake kuliko yeyote humu jukwaani msimfanye akalazimika kujitetea ataropoka sana
 
Sasa namwelewa Dr Slaa na mfano wake ule. Kumbe alikuwa anajaribu kutuonesha tatizo liko wapi. Yeye siyo tatizo kwa kusema haya. Na wala CHADEMA siyo tatizo hata kidogo..
Ni kwa nini Slaa anafurahia Lissu kuuwawa? Why anapenda mauaji?
 
Magufuli na ubabe wake wote akitumia vyombo vyake ameshindwa kuia au kuichafua chadema sasa Dr slaa ataweza.
Walikuwepo wenye nguvu kina Dr Kaburu wakafa wao sembuse huyu aliyekuja juzi juzi tu.
 
Hebu pitia link hiyo hapo chini. Ndipo utagundua Slaa kasema uongo au ukwel Joseph Yona Mwenyekiti wa chadema wilaya Temeke na Mjumbe wa Baraza kuu aliyetwkwa ameeleza waliomteka. Halafu wewe unaleta poroja ana assumptions wakati kuna facts!!!
Nawashauri vijana mkae kimya msimbagaze huyo Slaa.
Alikuwa SG CHADEMA
Anajua mengi ya chadema enzi zake kuliko yeyote humu jukwaani msimfanye akalazimika kujitetea ataropoka sana
Kwann alikaa kimya miaka 20
 
Kumtumia Yona Joseph ni matumizi mabaya ya akili na muda. Hata hivyo, itoshe kusema kwamba Dk Slaa mwenyewe ameanza kuyakana anayonukuliwa kuyasema kuhusu Chadema. It is wasting of time kumwamini mtu mwenye njaa anayeamini njaa yake inaweza kuondoka kwa kuchafua wenzake!
 
Kumbe unamjua Joseph Yona..
Kwanini wastage of time?
Hakutekwa?
Hakupigwa?
Hakuwataja chadema?
Maelezo yake ni uongo?

Why
 
Pascal wacha hizo mjomba unajua kabisa kuwa kitumbua kinachozungumzwa hapa ni kile katikati ya mapaja,au hujastua kile kinywaji cheru pendwa cha Yohana Mtembezi hivyo bado hujakaa sawa?
Muelewe pascal sio kama hajaelewa ni technic ya kuchokoza mjadala uwe mpana , sarcasm
 
huku ni kuchafua watu, nimeishi Sweden, kule hawali vitumbua, wanakula mikate tuu, kitendo cha kumsingizia mke wa Dr. Slaa, mama yetu Josephine Mushumbusi kuwa anafanya kazi ya kuuza vitumbua Sweden, ni kutaka kumchafua tuu, and soon tutasikia kuwa daktari kaanza tena kushindia mihogo!.
P
Pasco acha ujanja bwana! Nani kasema anauza vitumbua? Jamaa kasema "kitumbua" sasa nini huelewi? Au unatilia mkazo hoja kisayansi nini?
Ila tunatambua Dr ni rafiki yako tokea zile enzi zetu za Jambo forums ambapo wengi humu walikuwa wananyonya
 
Wangefanya CHADEMA na walivyokuwa wanawindwa na Magufuli ni lazima wangeshastakiwa na Chama kufutwa. Chadema hawahusiki ila wasiojukikana na Mimi siwajui. Huyu Prof. Mihogo Slaa vihela vya Ubalozi vimemlewesha.
 
Itachikua muda Sana kupata watu wenye kufikiri mantiki
Tatizo la Kuwa bias katika kufikiri na kutoa hukumu litatutafuna Kwa muda mrefu Sana.
Katika hoja hii hakuna ubishi kwamba Kuna matukio ya udhalimu yamekuwa yakitokea kwenye vyama,Serikalini na kwenye jamii.

Sehemu inayotakiwa kufanyiwa utafiti wa kina ni je,katika mipango ya kutekeleza uovu inaratibiwa na taasisi yote au ni kundi dogo katika taasisi husika lililowekwa maalumu Kwa KAZI husika?

Viongozi wa taasisi wanaporatibu umafia wanashirikisha taasisi yote?

Kama jibu ni hapana je,kitendo kiovu kinakuwa kosa la taasisi yote au ni Wale WACHACHE ambao wametumia koti la taasisi kutekeleza mambo ambayo siyo makusudio ya kitaasisi.

Mfano KAZI za Polisi au vyama vya kisiasa vimeainishwa kwenye sheria hivyo kama itatokea kundi dogo limekiuka sheria na taratibu hizo basi KUWEPO na mechanism ya kuwachomoa waliokiuka sheria wao kama wao kama ilivyo Kwa wahalifu wengine.

Kwa mujibu wa Circumstancial evidence CHACHA wangwe,Tundu Lisu NK Kuna makundi kutoka taasisi wametekeleza uhalifu Kwa mwanvuli wa taasisi na wamejificha ndani ya taasisi kujustify uovu wao.

Uhalifu ni uhalifu tu hakuna taasisi inayoweza Kuwa na Common intension ya kuua Bali watu kadhaa wanaweza kufanya hivyo na kujifanya wamepewa baraka na taasisi.

Hapo ni pagumu Sana itachukua muda mrefu kupaelewa kwasasa wacha tuendelee kuwaficha waovu mmoja akiharibu wote wanastahili lawama.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Matola hiyo sio "Inshumata" bali inaitwa Shuntama, nasikia ni kiboko sana. Babu kama Slaa lazima imtoe akili na kubwabwaja kama chizi.
 
Hakuna kitu kinaitwa Nshumata! Sweden hakuna vitumbua, napajua mno na hakuna nhicho wasema Bora ungesema anauza mikate ilo okwa ningekubaliana na wewe!

Tuje kwenye hoja kuna mambo mengi nyuma ya mambo anachosema Dr slaa na kwakuwa wengi hapa mpo kiushabiki you won’t understand me until it is your turn !!

Unajua ya Chacha!! ? Ya Baregu walichokuwa wamepanga dhidi yake na Kitila?

Anyway ya CHADEMA hayanihusu ila I was crosschecking facts ….

SIKU UKIJUA KWANINI DEREVA AKUTAKA KUJITOKEZA NDO UTAELEWA

Britanicca
DEREVA ALIKATAZWA NA GAIDI MBOWE
 
Hebu pitia link hiyo hapo chini. Ndipo utagundua Slaa kasema uongo au ukwel Joseph Yona Mwenyekiti wa chadema wilaya Temeke na Mjumbe wa Baraza kuu aliyetwkwa ameeleza waliomteka. Halafu wewe unaleta poroja ana assumptions wakati kuna facts!!!
Nawashauri vijana mkae kimya msimbagaze huyo Slaa.
Alikuwa SG CHADEMA
Anajua mengi ya chadema enzi zake kuliko yeyote humu jukwaani msimfanye akalazimika kujitetea ataropoka sana
1. Huo hauwezi kuwa ukweli iwapo wahusika wa tendo hilo wako huru..

2. Hoja ya msingi hapa ni kuwa, kesi ya kutekwa na kuumizwa huyo ndugu iliripotiwa polisi. Ni zaidi ya miaka 15 sasa, hakuna uchunguzi wala taarifa yoyote kutoka polisi ambao ndiyo wenye wajibu wa kutegua kitendawili hiki..

Unasemaje kuhusu hili? Nani anafanya porojo kati yetu sisi tunaojiuliza maswali haya na kulitupia lawama polisi na wewe/nyie ambao mnasema mambo ya hewani tu yasiyo na uthibitisho..?

By the way ndugu artch2311 kama kweli ndiyo CHADEMA wanahusika na shida hizi kuna ugumu gani kwa polisi kuwakamata wote na kuwafungulia mashitaka mahakamani kisha wafungwe na ikibidi chama kifutwe kabisa..?

Oooh, huna jibu, 😎😎😎!!

Mimi nitakusaidia kujibu; Kwamba sababu ni mbili tu;

1. Polisi hawana cha kuwashitakia CHADEMA au mwanachama yeyote wa CHADEMA in connection na matukio haya kwa sababu hakuna ushahidi wa kuwa - incriminate...!

2. Polisi wanawajua wahusika wa matendo haya machafu na ya kijinai. Wanaofanya haya ni wana CCM wenyewe (Ole Sabaya, Paulo Makonda na timu zao) wakishirikiana na baadhi ya maafisa wakubwa na mafisadi ndani ya serikali wakiwatumia UWT na polisi...

Wanajitahidi kwa kila namna wayatendayo wayape sura ya "KUTENDWA NA CHADEMA" lakini mpango huo kwa miongo kadhaa ulishashindikana na hauwezekaniki tena daima na milele mpaka wao wote na chama chao wapokee hukumu yao...!

Rejea matukio haya yaliyosukwa na wao wenyewe na kisha yakawaumbua mbele ya safari;

✓Ugaidi wa Rwakatare..

✓Mauji ya bomu ktk mkutano wa CHADEMA 2013 Arusha yaliyoratibiwa na Mwigulu Nchemba na wenzake CCM by then akiwa ni Naibu katibu CCM Tanzania bara (kama sijakosea)

✓mauji ya Aqulline Aqullina mwaka 2018 yaliyofanywa na polisi katikati ya kusanyiko la CHADEMA

✓ Jaribio la kuuwawa kwa Tundu Lissu [mbunge, mwanaharakati na mwanasheria nguli na makamu mwenyekiti taifa CHADEMA], mchana kweupe na katikati ya mji wa Dodoma..

✓ And recently, ni kesi ya ugaidi wa Freeman Mbowe, na;

✓ Matukio mengine mengi madogo dogo nchi nzima..!

CCM wakitumia advantage ya kuwa ni "chama dola" hutumia mbinu mbali mbali hususani ya kuwatumia baadhi maafisa wa UWT na POLISI wasio na maadili na kazi yao kuwasadia kupigana vita yao ya kisiasa dhidi ya mpinzani wao mkuu CHADEMA..

Wakati mwingine wanajiingiza ktk chama hiki, wanavalisha sare za CHADEMA watu wao ili wafanye uhalifu kwa jina la CHADEMA na baadaye wapate sababu ya kuishitaki...

Very unfortunately for them is that, their evil strategies & plans have spectacularly failed all the times...!!

Mpaka hapo huelewi tu mchezo huu wa kisiasa unavyochezwa wewe artch2311 ili ufungue akili na ufahamu wako? Unadhani Dr Slaa atakuja ni jambo gani jipya linaloweza kuwa incriminate CHADEMA? Nakuhakikishia, NOTHING.... absolutely NOTHING..!!
 
Back
Top Bottom