The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
- Thread starter
- #101
Binafsi sijaelewa unatetea au kupinga kitu gani..Itachikua muda Sana kupata watu wenye kufikiri mantiki
Tatizo la Kuwa bias katika kufikiri na kutoa hukumu litatutafuna Kwa muda mrefu Sana.
Katika hoja hii hakuna ubishi kwamba Kuna matukio ya udhalimu yamekuwa yakitokea kwenye vyama,Serikalini na kwenye jamii.
Sehemu inayotakiwa kufanyiwa utafiti wa kina ni je,katika mipango ya kutekeleza uovu inaratibiwa na taasisi yote au ni kundi dogo katika taasisi husika lililowekwa maalumu Kwa KAZI husika?
Viongozi wa taasisi wanaporatibu umafia wanashirikisha taasisi yote?
Kama jibu ni hapana je,kitendo kiovu kinakuwa kosa la taasisi yote au ni Wale WACHACHE ambao wametumia koti la taasisi kutekeleza mambo ambayo siyo makusudio ya kitaasisi.
Mfano KAZI za Polisi au vyama vya kisiasa vimeainishwa kwenye sheria hivyo kama itatokea kundi dogo limekiuka sheria na taratibu hizo basi KUWEPO na mechanism ya kuwachomoa waliokiuka sheria wao kama wao kama ilivyo Kwa wahalifu wengine.
Kwa mujibu wa Circumstancial evidence CHACHA wangwe,Tundu Lisu NK Kuna makundi kutoka taasisi wametekeleza uhalifu Kwa mwanvuli wa taasisi na wamejificha ndani ya taasisi kujustify uovu wao.
Uhalifu ni uhalifu tu hakuna taasisi inayoweza Kuwa na Common intension ya kuua Bali watu kadhaa wanaweza kufanya hivyo na kujifanya wamepewa baraka na taasisi.
Hapo ni pagumu Sana itachukua muda mrefu kupaelewa kwasasa wacha tuendelee kuwaficha waovu mmoja akiharibu wote wanastahili lawama.
Hata hivyo nikuulize maswali kadhaa na tafadhali, be hosest to give us the honest answers..
1. Kwani kazi ya Jeshi la polisi ni nini kwa uelewa wako?
2. Je, siyo kulinda usalama wa raia na mali zao?
3. Je, siyo kuzuia uhalifu?
4. Je, siyo kuchunguza makosa ya uhalifu/jinai na kukamata wahalifu na kuwapeleka mahakamani na sheria kuchukua mkondo wake..?
5. Je, polisi wana mipaka au wanazuiwa kuchukua au kuchunguza baadhi ya watu/taasisi zinazoripotiwa kuwa zimefanya uhalifu/jinai..?
NOTE:
##Ukijibu maswali hayo yote, sasa unaweza kujibu swali hili muhimu na ambalo ndilo MSINGI WA HOJA YA MADA HII, kwamba;
1. MOSI; Ni sababu gani sensible zimelifanya Jeshi la polisi kushindwa kuchunguza tukio la kutekwa na kupigwa hadi karibu ya kufa kwa m/kiti huyo wa CHADEMA (w) lililo ripotiwa na yeye mwenyewe Dr W. P. Slaa [by then akiwa Katibu Mkuu - CHADEMA] na inasemekana kuwa ni CHADEMA wenyewe kuhusika..?
2. MBILI, ni sababu gani sensible ambazo zinaeleweka kwa wenye akili timamu zinazolifanya Jeshi la polisi kushindwa kuchunguza assassination attempt ya Tundu Lissu mwaka 2017...?
3. TATU, Je huoni kuwa kama ni INSIDE JOB ndani ya CHADEMA wenyewe ndiyo ilikuwa fursa ya kutumia matukio haya mawili makuu kuwachunguza na kuwa - pin-point wahusika kuweka mambo hadharani kukiwa na vivid evidences...?
4. NNE, watu wachache ndani ya taasisi mathalani vyama vya siasa, jeshi la polisi, UWT nk nk kutumiwa kufanya uhalifu/jinai na kuichafua taasisi, kwa mujibu kujieleza kwako hapo juu, Je hiyo yaweza kuwa justification ya polisi kushindwa kufanya uchunguzi ktk taasisi hizo ili kuikomesha tabia hiyo...?
##Kama mpaka hapa hujailewa hoja yangu, basi kalaghabhaho...!!