WanaJF Salaam
Ni siku nyingine muhimu kabisa katika historia ya chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA.
Baraza Kuu jipya la Chadema linakutana leo maalum kuichagua sekretariati mpya ya chama hicho itakayokivusha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho Mwenyekiti wa Taifa atapaswa kupendekeza majina kwa nafasi tatu za Katibu Mkuu na Manaibu wake wawili wa Tangsnyika na Zanzibar.Kisha Baraza Kuu litapigia kura mapendekezo ya Mwenyekiti na kuwachagua rasmi watendaji hao.
Kwa sasa habari kuu hapa katika viwanja vya Mlimani City ni kuhusu jina la Katibu Mkuu mpya.Huku majina kadhaa yakitajwa na wajumbe kwa kubashiri.
Majina yaliyoko vinywani vya wajumbe na kuonekana kutajwa sana ni John Mnyika,John Heche,Salum Mwalim,Lazaro Nyalandu na Vicent Mashinji ambaye ni Katibu Mkuu anayemaliza muda wake.
Tunatarajia kuwaletea taarifa kamili ya uteuzi utakaofanywa na Mwenyekiti na tunawaahidi wasomaji wetu wa Jamii Forum kuwa wa kwanza kupata taarifa.
Asanteni sana
Wasalaam
Molemo wa JF