Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante kwa ushauri
Naona angalau wewe umeona nini kazi ya Katibu Mkuu. Ukifuatilia mikutano hii ya chadema wametoka kwenye the so called mechanical politics. Sasa nashangaa baadhi ya fans wao humu wanataja majina ya aina hiyo ya siasa. Ile nafasi ina hitaji mtu wa mipango sana na seraWe need a focused diplomatic person, ukimuweka mtu mechanical kunaweza kuwa na shida kidogo. Heche is mechanical anafaa sana kwenye uhamasishaji, mikutano, campaign etc
ana kelele tu hamna kituHuyu Mzee anafaa sana, ni msomi, anajiamin , NA mwenye misimamo yako.
Sema aliwah sema yeye sio mwanasiasa.
Easter Bulaya.........anatosha!
vyeo vyote vikubwa chadema mnagawia wabunge .Tatizo la ajira gumu kwisha mtu mbunge .halafu tena katibu mkuu mishahara yote abebe yeye ya ubunge na ukatibu mkuu .Wapeni wengine igeni CCm sio mnazungusha hao hao kakundi kadogo ka wabunge
Hili ni swali tu ndugu zangu ambalo nimelileta kwenu na wala sina lengo lingine zaidi ya kutaka kujua maono na utabiri wenu tu.
Ikumbukwe kwamba hii ni nafasi nyeti sana ndani ya chama, inahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa sana anayeweza kuunganisha viongozi na wanachama, mwenye uwezo wa kufuta makundi yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huko kwenye kanda na kwenye Mabaraza, mbunifu na asiye muoga.
Ndio siasa iyo...siasa inahitaji uongeaji... Wakat ambao watu wanahisi chama kimekoswa MTU..ana kelele tu hamna kitu
John Heche, Peter Msigwa, Mnyika, Halima Mdee na Kigaila Bensoni. Mmojawapo anafaa japo watatu wamwanzo are the bestWanaJF Salaam
Ni siku nyingine muhimu kabisa katika historia ya chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA.
Baraza Kuu jipya la Chadema linakutana leo maalum kuichagua sekretariati mpya ya chama hicho itakayokivusha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho Mwenyekiti wa Taifa atapaswa kupendekeza majina kwa nafasi tatu za Katibu Mkuu na Manaibu wake wawili wa Tanganyika na Zanzibar.Kisha Baraza Kuu litapigia kura mapendekezo ya Mwenyekiti na kuwachagua rasmi watendaji hao.
Kwa sasa habari kuu hapa katika viwanja vya Mlimani City ni kuhusu jina la Katibu Mkuu mpya.Huku majina kadhaa yakitajwa na wajumbe kwa kubashiri.
Majina yaliyoko vinywani vya wajumbe na kuonekana kutajwa sana ni John Mnyika,John Heche,Salum Mwalim,Lazaro Nyalandu na Vicent Mashinji ambaye ni Katibu Mkuu anayemaliza muda wake.
Tunatarajia kuwaletea taarifa kamili ya uteuzi utakaofanywa na Mwenyekiti na tunawaahidi wasomaji wetu wa Jamii Forum kuwa wa kwanza kupata taarifa.
Asanteni sana
Wasalaam
Molemo wa JF
Hao maccm wanajielewaga basi kasahau vyeo mwenyekiti wao. Wakati anapewa wenyekiti alikuwa tayari na vyeo vingapi? Pumbavu sana.Hao mawaziri walioko ccm wanaacha ubunge?
Kwangu mimi yeyote kati ya hawa anafaa:
1. JOHN HECHE (MB) Tarime Vijijini
2. MARCOS ALBANIE (Mwanasheria na mwanaharakati mbobevu)
John Mnyika abaki kuwa naibu (Tanganyika) na Mwalimu Salumu (Zanzibar)