Pre GE2025 John Mnyika: Rais Samia lazima aondolewe Madarakani Uchaguzi Mkuu ujao
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Katibu mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesisitiza kuwa ni lazima Rais Samia aondolewe madarakani katika Uchaguzi Mkuu ujao. Mnyika anasema kuwa Rais ameshindwa kusikiliza sauti za wananchi na Jumuiya za Kimataifa, ambao wamepaza sauti kuhusu tishio la amani nchini kufuatia kifo cha Ally Kibao, akiongeza kwamba mchakato wa kumuondoa Rais Samia lazima uanze na kuwaondoa CCM katika kila nyanja. Mnyika anaweka wazi kuwa kuna hitaji la mabadiliko ili kuhakikisha demokrasia na amani vinapatikana nchini.
Video: Jambo TV

Pia, Soma:
 
Sami, ameshapanik Tayari,( hajui baya lipi na zuri lipi)
1. Washauri wake ndo hivyo wanampeleka chaka kila kukicha, mbaya zaidi anayapokea maoni yao kama yalivyo bila kuyachambua.

2. Nguzo kuu anayotegemea kwa sasa ni mitutu kutoka kwa police..
 
Huyu Mama ni mzigo wa misumari kwa watanzania.
Sio kama Mzee Mbowe na genge lake la Wachagga pale ufipa aisee .Imagine leo hii John Mrema anayo sauti kuliko katibu mkuu wa chama 🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Katibu mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesisitiza kuwa ni lazima Rais Samia aondolewe madarakani katika Uchaguzi Mkuu ujao. Mnyika anasema kuwa...
Afadhali baada ya mkwara juzi mmejielewa kuwa ni uchaguzi tu ndio unatoa haki ya kumuondoa kiongozi madarakani na si vinginevyo.hongereni kwa kubadili gia angani🤣🤣
 
Muacheni huyu mama,mnaanza kutuaminisha Yale Yale ya J.K ni dhaifu,alivyokuja JPM a.k.a Chuma mkaanza kukimbia nchi.
Ni huyu huyu mnyika alianza maneno yake ya shombo and last akaufyata.
 
Back
Top Bottom