Katibu mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amesisitiza kuwa ni lazima Rais Samia aondolewe madarakani katika Uchaguzi Mkuu ujao. Mnyika anasema kuwa Rais ameshindwa kusikiliza sauti za wananchi na Jumuiya za Kimataifa, ambao wamepaza sauti kuhusu tishio la amani nchini kufuatia kifo cha Ally Kibao, akiongeza kwamba mchakato wa kumuondoa Rais Samia lazima uanze na kuwaondoa CCM katika kila nyanja. Mnyika anaweka wazi kuwa kuna hitaji la mabadiliko ili kuhakikisha demokrasia na amani vinapatikana nchini.
Video: Jambo TV
Pia, Soma: