Jokate Mwegelo ateuliwa na CCM kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Kwamba baada ya uteuzi huu, Jokate hatendelea kuwa mkuu wa Wilaya au mwandishi wa taarifa hiyo hana uelewa wa lugha ya Kiswahili...

Najaribu kuelewa kama uteuzi wa kichama unaweza mvua mtu madaraka ya uteuzi aliyopewa na Rais...
Inawezekana asiendelee,maana ata Katibu Mwenezi Sophia Mjema alikuwa RC wa Shinyanga na ata Naibu Katibu Mkuu wa CCM taifa Bwana Macha alikuwa DC Kahama, lakini baada ya kuitwa kwenye chama wakatema nafasi zao.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Nilishaandika humu jukwaani miezi michache iliyopita juu ya mh jokate mwegelo kuwa ni kiongozi mwenye uwezo,bidii ya kazi,uchapa kazi na maarifa ya uongozi. Na nilipendekeza kuwa uchaguzi ujao achukue Fomu ya ubunge. Kwa hakika namtaka kila la heri mh jokate katika majukumu yake mapya ndani ya chama. Ni kiongozi mchapa kazi sana na kijana mbunifu na mwenye uwezo mkubwa sana kiuongozi
Wewe chawa ulikimbia umande nini?

Majina ya watu unaanza na herufi ndogo, katikati ya sentensi unaweka herufi kubwa kiufupi kanuni za uandishi huzijui.

Hivi UVCCM ndio imeishiwa hivi wanaokoteza mabumunda kuja kusifia humu kwa elfu 7.
 
Sema tu CV yake kwenye mahusiano haijakaa sawa hata kidogo.

Imagine amedate na wasanii wawili maarufu wa Bongo fleva kwa nyakati tofauti!! Kuna yule tall aliyecheza mpira wa kikapu Marekani!! Stone naye nasikia aliweka kambi! Kuna yule Das aliyetumbuliwa na Stone kipindi kile!!! Bado kuna huyo kada mwenzake aliyemzalisha.

Nadhani kwa wale mabinti wote wenye malengo na ndoto za kufanya mambo makubwa hapo baadaye, wachukue tahadhari mapema za Kujilinda, na pia kujiheshimu. Mheshimiwa Katibu Mkuu anaweza kuwa role model wa mabinti/wanawake katika mambo mengi! Ila siyo kwenye kipengele cha mahusiano yake.
Dada huruma
 
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyokutana
katika kikao chake maalum, leo tarehe 1 Oktoba, 2023, jijini Dar es Salaam, imefanya uteuzi wa makatibu wakuu wa Jumuiya za Umoja wa Wanawake (UWT) na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Kiaina pia CCM ilitaka Chama Cha Walimu Tanzania - CWT nacho kiwe moja ya jumuiya zake kama UVCCM, UWT, WAZAZI na kuichagulia CWT katibu mkuu ambaye chama dola kongwe kinamtaka

TOKA MAKTABA:

Walimu wamtetea katibu wao wa CWT mwalimu Japhet Maganga, waimba solidarity forever waalimu


View: https://m.youtube.com/watch?v=fy5yBs65RHc
 
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Taifa, iliyokutana katika kikao chake maalum, leo tarehe 1 Oktoba, 2023, jijini Dar es Salaam, imefanya uteuzi wa makatibu wakuu wa Jumuiya za Umoja wa Wanawake (UWT) na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Katika kikao hicho, Kamati Kuu imemteua Ndugu Jokate Mwegelo, kuwa Katibu Mkuu wa UWT, kabla ya uteuzi huo Ndugu Mwegelo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga.

** Taarifa Kwa Umma ***

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyokutana
katika kikao chake maalum, leo tarehe 1 Oktoba, 2023, jijini Dar es Salaam, imefanya uteuzi wa makatibu wakuu wa Jumuiya za Umoja wa Wanawake (UWT) na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Katika kikao hicho, Kamati Kuu kimemteua Ndugu Jokate Mwegelo, kuwa Katibu Mkuu wa UWT, kabla ya uteuzi huo Ndugu Mwegelo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga.

Pia, Kamati Kuu imemteua Ndugu Fakii Raphael Lulandala kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM, kabla ya uteuzi huo Ndugu Lulandala alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, mkoani Songwe.

Katika hatua nyingine, Kamati Kuu imemteua Ndugu Hamad Khamis Hamad, kuwa mgombea wa CCM wa nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo la Matembwe.

Aidha, Kamati Kuu imewashukuru na kuwapongeza wanachama wote wa CCM na wananchi kwa ujumla katika Jimbo la Mbarali kwa kumchagua mgombea wa CCM Ndugu Bahati Kenneth Ndingo, kuwa Mbunge wao katika
uchaguzi mdogo uliofanyika Septemba 20, 2023.

Pia, Kamati Kuu imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na ziara aliyoifanya katika mikoa ya Lindi na Mtwara, ambayo ilikuwa ya mafanikio makubwa sana . Katika ziara hiyo pamoja na mambo mengine, Rais alikagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2025, kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi changamoto za wananchi.

Pia, Kamati Kuu kimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa namna anavyoiongoza serikali katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Sophia Edward Mjema
Katibu Wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi

1 Oktoba, 2023

View attachment 2768443

View attachment 2768422
Kidumu CCM [emoji23][emoji7][emoji2788][emoji2788][emoji109][emoji1720][emoji1732][emoji120][emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom