Joseph Mbiliyi (Sugu) awaumbua CHADEMA, akiri walichelewa Uwanjani kumuaga Mzee Mkapa

Image

Leo, ilikuwa ni siku ya kuuaga Kitaifa mwili wa Rais wa Awamu ya 3, Benjamin Mkapa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar na viongozi mbalimbali walikuwa wakienda kutoa salamu zao za mwisho

Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe walienda uwanjani hapo na baadaye kudai kuwa walizuiwa kuingia Uwanjani kwa ajili ya kuuaga mwili wa Mkapa

Katika Ufafanuzi wao CHADEMA huku wakiitaka Serikali itoe ufafanuzi kwa kuzuiwa kwao wamesema wao wamefuata ratiba waliyopelekewa ikionesha tarehe, muda, siku tukio na muhusika

Hata hivyo, Jana Msemaji wa Serikali aliweka bayana ratiba ya kufika uwanjani hapo ambapo Serikali iliwataka Viongozi wote wa Kitaifa na Viongozi wa Kisiasa kufika katika Uwanja wa Karimjee na kuacha magari yao hapo kukiwa na gari maalum la kuwapeleka uwanjani ambapo la mwisho liliondoka saa 1:30 asubuhi
 
Laumu inapobidi, kiri unapokosea, omba msamaha unapoharibu. Tunataka kufuta siasa za uwongo, hila na unafiki.

Viongozi wa CHADEMA kama walichelewa, wakiri kosa, wajisahihishe na waombe msamaha. Kama viongozi, walistahili kuzingatia ratiba na muda.

Kwenye tukio hili la msiba, kiserikali mfiwa wa kwanza ni Rais na mke wa marehemu. Lakini zaidi ya hayo, Magufuli ni Rais, ndiye mgeni rasmi - huwezi kumtanguliza yeye halafu wewe ukafuata baadaye.

Makosa haya CHADEMA huwa wanayafanya mpaka kwenye uchaguzi. Wanachelewa kurudisha fomu au hurudisha dakika za mwisho. Wanakosea kujaza fomu, n.k.

Japo huwa kunakuwa na hila na figisu nyingi lakini pia kuna upungufu wa umakini. Unakosa umakini, unakimbilia kulalamika na kuwaonesha watu kuwa umeonewa.

Kwenye tukio hili.la msiba, CHADEMA walenge maombolezo ya msiba tu. Nothing else.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naamini sana kuwa hapa duniani bado hakuna mwanadamu aliye sahihi kwa 100%.

Kama yule kamishina wa jeshi la magereza alichelewa kuingia kwenye kikao cha waziri wa mambo ya ndani chini ya Lugola itakuwa sisi raia?
sawa mkuu ila akili zetu hazijadukuliwa.
viongozi wasingiweza kuingia uwanjani baada ya rais kuingia as kiprotokali sio sawa.
Pia tushukuru wameishia getini huenda humo ndani kuna mengine wameepushwa nayo.
 
SAFI SANA JOSEPH MBILINYI.
MWAMBIE MWENYEKITI AOMBE RADHI WATANZANIA.
 
Mkuu naamini sana kuwa hapa duniani bado hakuna mwanadamu aliye sahihi kwa 100%.

Kama yule kamishina wa jeshi la magereza alichelewa kuingia kwenye kikao cha waziri wa mambo ya ndani chini ya Lugola itakuwa sisi raia?
ni kweli tumeumbwa kukosea.
 
Leo, ilikuwa ni siku ya kuuaga Kitaifa mwili wa Rais wa Awamu ya 3, Benjamin Mkapa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar na viongozi mbalimbali walikuwa wakienda kutoa salamu zao za mwisho

Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe walienda uwanjani hapo na baadaye kudai kuwa walizuiwa kuingia Uwanjani kwa ajili ya kuuaga mwili wa Mkapa

Katika Ufafanuzi wao CHADEMA huku wakiitaka Serikali itoe ufafanuzi kwa kuzuiwa kwao wamesema wao wamefuata ratiba waliyopelekewa ikionesha tarehe, muda, siku tukio na muhusika

Hata hivyo, Jana Msemaji wa Serikali aliweka bayana ratiba ya kufika uwanjani hapo ambapo Serikali iliwataka Viongozi wote wa Kitaifa na Viongozi wa Kisiasa kufika katika Uwanja wa Karimjee na kuacha magari yao hapo kukiwa na gari maalum la kuwapeleka uwanjani ambapo la mwisho liliondoka saa 1:30 asubuhi
MATAGA baada ya kudukua akaunti wanaanza kujitekenya! Mtu kashasema ukweli wote mbona
 
Hasa hasa Mwenyekiti, itakuwa yeye ndiyo kawachelewesha wenzake, maana mkubwa huwa haamshwi
Nyinyi mbona mlishindwa kwenda Nairobi hospital kumjulia hali mh Lissu? Kuna mtu alisha omba radhi kwa hilo?
 
Wewe unao ushahidi kuwa walipewa ratiba sahihi? Kunamabadiliko yaliyofanyika kwenye ratiba ya awali.
Baada ya hilo tukio unsonekana moyo wako umefarijika, huo ni ujinga.

Unamaanisha nini walipewa ratiba sio? Umeelewa kwanza nilichoandika? Jana jioni Serikali iliweka wazi kabisa ratiba kwa viongozi wote kwa namna ya kuafuata. Viongozi waliofuata ratiba si wajinga.....
 
Kuna uwezekano mkubwa baadhi ya viongozi wa Chadema wako kwenye system haiwezekani kila mara wanafanya makosa ambayo yako wazi.
Nyinyi mbona mliwakataza hata wabunge wenu kwenda hospital Nairobi kumjulia hali mh Lissu?
 
Leo, ilikuwa ni siku ya kuuaga Kitaifa mwili wa Rais wa Awamu ya 3, Benjamin Mkapa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar na viongozi mbalimbali walikuwa wakienda kutoa salamu zao za mwisho

Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe walienda uwanjani hapo na baadaye kudai kuwa walizuiwa kuingia Uwanjani kwa ajili ya kuuaga mwili wa Mkapa

Katika Ufafanuzi wao CHADEMA huku wakiitaka Serikali itoe ufafanuzi kwa kuzuiwa kwao wamedai wao wamefuata ratiba waliyopelekewa ikionesha tarehe, muda, siku tukio na muhusika

Hata hivyo, Jana Msemaji wa Serikali aliweka bayana ratiba ya kufika uwanjani hapo ambapo Serikali iliwataka Viongozi wote wa Kitaifa na Viongozi wa Kisiasa kufika katika Uwanja wa Karimjee na kuacha magari yao hapo kukiwa na gari maalum la kuwapeleka uwanjani ambapo la mwisho liliondoka saa 1:30 asubuhi
Lakini amesoma maelezo ya afisa habari wake ambaye anaeleza ya kuwa palikuwa na mawasiliano kati yao na Msajili wa vyama.
Ninachohisi ni kuwa Chadema walikuwa wanatarajia VIP treatment lakini kwa maelezo ya Makene waliambiwa "wapange foleni.
Bado wingu halijaondoka!!!
 
Back
Top Bottom