Mama yenu mnamtwika mambo ambayo hata hana uwezo naye na so far raia na chama chake wamemkataa.
Ngoja kwanza nianze na kuuliza, hivi masuala yake na kujipitisha kuwa mgombea pekee kashayamaliza ama bado?
Na jingine kelele Za wanachama wenzie akina Lusinde na co amezisikia ama bado kashupalia?
Sasa twende kwenye hoja.
Mama hana la kufanya kuhusu si kwala tu bali hata ishu nzima ya SGR haiwezi na daily liko wazi. Ramani ya SGR ilikuwa ya JPM na aliondoka nayo ramani yake.
Ukitaka kujua hilo rudi nyuma tafuta clip za JPM akiwa anaongea juu ya SGR, malengo na umuhimu wake kwanzia kwa wananchi mpaka kwa Taifa alafu vitafute leo unambie viko wapi. JPM aliagiza viwanja maeneo karibu na SGR vipimwe wauziwe watu Ili ikianza wakafanye biashara maeneo hayo ..vipi leo hari ikoje huko?
Angalia barabara zinazolisha hiyo reli na kama zimejengwa kama ilivyokuwa katika mkakati Ili kuwafikisha abiria vituoni, zipo, zimejengwa? Ukitoka Dar kuja Chalinze kuna barabara zaidi ya 10 zote ni trunkroads kuelekea kwenye vituo vya SGR lakini hajabu hakuna iliyo katika ubora wa kusafirisha abiria ukitoa hiyo ya kwenda kwala kwa ajiri ya malori. Zingine zote ni madongo kwinama na abiria hawana jinsi ya kwenda vituoni. Hilo ni zero ya zero.
Nenda hapo vituoni kwenyewe, ukifika pale ukaangalia pembeni ni kama umefika msibani. Hakuna heka heka, hakuna mzunguko wa watu hakuna mzunguko wa biashara. Ni kama kwamba pale abiria wako msibani ..wako wapi wafanyabiashara, ziko wapi biashara, pesa na ajira maeneo hayo viko wapi? Yako wapi yaliyokuwa maono na malengo ya muasisi JPM? Zero.
Natolea mfano, kile chuo cha uongozi cha Nyerere pale Kibaha wakati kinajengwa raia waliamasishwa wajiandae kufanya shughuri na kutoa huduma kwa wanafunzi watakaokuja kusoma. Watu kweli wakaenda wakanunua maeneo, wakaweka miundombinu, wakajenga majumba na ofisi wakisubiri chuo kije. Nenda kaone leo kinachoendelea na kama kuna hata hiyo dalili ya kuwa chuo na hizo pesa za watu ziko wapi, chuo ni kama msikitini na hakuna kinachoonekana cha kuwasaidia hao walowekeza hizo pesa zao, maana yake chuo kimeleta hasara kwao.
Kwahiyo tunaposema Sa100 nchi inampwelepweta mnatakiwa kuelewa, hana ramani na maarifa hamna. Hauwezi ukakaa unalia leo kama raisi watu wako hawana ajira, vijana hawana ajira alafu eti unazuia vituo vya SGR watu wasijenge, wasifanye biashara, wasitoe huduma. Fikiria wangeruhusiwa ni watu kiasi gani wangekuwa huko wanaifanya biashara zao kujiingizia kipato, lakini umewafungia alafu unajifanya unaona uchungu na ajira ...huku ni kushondwa kwa kiwango cha juu sana kama raisi. Anachokwenda kukifanya pia subirini kuona maajabu yajayo, uwezo wa yeye kushughulika na mambo makubwa kama haya jamani twende turudi ni wa chini mnoooo.