Julai 31, Rais Samia kuzindua bandari kavu ya Kwala, malori kuingia mjini sasa basi

Kimara unapajua lakini.
 
Nani huwa anahujumu mipango?
 
Mama yenu mnamtwika mambo ambayo hata hana uwezo naye na so far raia na chama chake wamemkataa.

Ngoja kwanza nianze na kuuliza, hivi masuala yake na kujipitisha kuwa mgombea pekee kashayamaliza ama bado?

Na jingine kelele Za wanachama wenzie akina Lusinde na co amezisikia ama bado kashupalia?

Sasa twende kwenye hoja.
Mama hana la kufanya kuhusu si kwala tu bali hata ishu nzima ya SGR haiwezi na daily liko wazi. Ramani ya SGR ilikuwa ya JPM na aliondoka nayo ramani yake.

Ukitaka kujua hilo rudi nyuma tafuta clip za JPM akiwa anaongea juu ya SGR, malengo na umuhimu wake kwanzia kwa wananchi mpaka kwa Taifa alafu vitafute leo unambie viko wapi. JPM aliagiza viwanja maeneo karibu na SGR vipimwe wauziwe watu Ili ikianza wakafanye biashara maeneo hayo ..vipi leo hari ikoje huko?

Angalia barabara zinazolisha hiyo reli na kama zimejengwa kama ilivyokuwa katika mkakati Ili kuwafikisha abiria vituoni, zipo, zimejengwa? Ukitoka Dar kuja Chalinze kuna barabara zaidi ya 10 zote ni trunkroads kuelekea kwenye vituo vya SGR lakini hajabu hakuna iliyo katika ubora wa kusafirisha abiria ukitoa hiyo ya kwenda kwala kwa ajiri ya malori. Zingine zote ni madongo kwinama na abiria hawana jinsi ya kwenda vituoni. Hilo ni zero ya zero.

Nenda hapo vituoni kwenyewe, ukifika pale ukaangalia pembeni ni kama umefika msibani. Hakuna heka heka, hakuna mzunguko wa watu hakuna mzunguko wa biashara. Ni kama kwamba pale abiria wako msibani ..wako wapi wafanyabiashara, ziko wapi biashara, pesa na ajira maeneo hayo viko wapi? Yako wapi yaliyokuwa maono na malengo ya muasisi JPM? Zero.

Natolea mfano, kile chuo cha uongozi cha Nyerere pale Kibaha wakati kinajengwa raia waliamasishwa wajiandae kufanya shughuri na kutoa huduma kwa wanafunzi watakaokuja kusoma. Watu kweli wakaenda wakanunua maeneo, wakaweka miundombinu, wakajenga majumba na ofisi wakisubiri chuo kije. Nenda kaone leo kinachoendelea na kama kuna hata hiyo dalili ya kuwa chuo na hizo pesa za watu ziko wapi, chuo ni kama msikitini na hakuna kinachoonekana cha kuwasaidia hao walowekeza hizo pesa zao, maana yake chuo kimeleta hasara kwao.

Kwahiyo tunaposema Sa100 nchi inampwelepweta mnatakiwa kuelewa, hana ramani na maarifa hamna. Hauwezi ukakaa unalia leo kama raisi watu wako hawana ajira, vijana hawana ajira alafu eti unazuia vituo vya SGR watu wasijenge, wasifanye biashara, wasitoe huduma. Fikiria wangeruhusiwa ni watu kiasi gani wangekuwa huko wanaifanya biashara zao kujiingizia kipato, lakini umewafungia alafu unajifanya unaona uchungu na ajira ...huku ni kushondwa kwa kiwango cha juu sana kama raisi. Anachokwenda kukifanya pia subirini kuona maajabu yajayo, uwezo wa yeye kushughulika na mambo makubwa kama haya jamani twende turudi ni wa chini mnoooo.
 
Sema kuna wakati ni kama tunaenda enda tu bila mwelekeo. Baada ya JPM kufariki jiji la Dar limelipuka kwa uwepo wa Bandari kavu kila kona ya jiji... Kuanzia Mbagala, Sinza, Kigamboni na kila kona. Hii yote ni hujuma tu kwa bandari kavu hii ya Kwala. Leo mnatuambia Mama anaenda kuizindua ili kupunguza foleni mjini, swali, hizi ambazo zimejengwa na kina GSM kila kona ya jiji zitafungwa????? Na kama zitabaki ikiwemo inayojengwa Mbagala Zakhem muda huu, je mizigo itapelekwa pale kwa Edikopta au Meli? Kama ni malori je hapo mmetibu tatizo gani au ni kampeni??
Ifike mahali tuwaombee sana viongozi wetu wawe na moyo thabiti kweli wa kutuongoza na sio siasa kila sehemu kwa manufaa ya wachache.

Ni hayo Tu!
 
Ili kulinda barabara zetu zidumu muda mrefu na kurahisisha usafiri wa barabara Malori yalitakiwa yawe Yana pokea Mzigo kutoka kwenye train kule kigoma kwenda Kongo, burundi na Rwanda maana kwa Zambia na kwingineko TAZaRa inafika.Kwa mizigo ya ndani Malori yatengenezewe bandari Karibu Karibu na staisheni za Reli.

Naweza kuwa naza ndani ya box anayewaza Nje ya box anisaidie na Mimi niwaze Nje ya box! Asante
 
Inasikitisha sana
 
Hapo angezindua hata Nick wa pili tu.

BTW: Isaka dry port nayo inastahili ufufuo na uzima ili wanyarwanda waishie hapo kama enzi zile.

Miundombinu mf matenki ya mafuta yapo hapo yamechakaa tu na ule mji umesinyaa baada WFP kutokuwa active kama zamani.
 
Mimi ndo nakuambia ukweli mdau, hapo hana kitu. Nchi hii inaendeshwa kihuni huni tu na mipango yote inaelekezwa kwenye watu kupiga ...it's for sale.
 
Una roho mbaya kama sehemu za siri zisizonyolewa muda mrefu
 
Hayo yataruhusiwa usiku tu mida maalum
 
Sasa kuna mji unaokosa malori mjini umeambiwa kupunguza sio kuondoa malori na huu mradi utahusu malori transit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…