Juma Nature ndio best storyteller wa muda wote Bongo. Wasanii wachanga mnao-rap jifunzeni kwa Juma Nature

Mkuu sanaa ni pana sana, haiko hivyo unavyofikiria... Huo uandishi na uwasilishaji wa Dizasta una hadhira yake na ndio maana mpaka leo bado anafanya hicho anachokifanya... Dizasta ni moja kati ya MCs wachache ambao uwasilishaji wao umebaki vilevile bila kuyumbishwa na kelele za akina nyie ambao mnapiga mayowe kuwa wasanii wa hivyo wabadirike kufuata soko.

Hoja yako ya kusema ngoma zake zina part 1 mpaka 8 ukimsikiliza kama unaperuzi kurasa... Kuna ubaya gani kufanya hivyo? Au ubongo wako mdogo hupendi kuperuzi kurasa? Kwanza inabidi ujue kuwa mziki wa HipHop una nguzo zake, na mojawapo ya nguzo muhimu zaidi ni "Knowledge" nguzo ambayo siku hizi imekua underrated sana kutokana na mziki kuingiliwa na watoto waimba ngono, pombe na mademu sana kuliko maarifa, Dizasta kaamua kubaki huko.

Hiyo style ya kufanya ngoma kwa series sio ngeni kwenye fasihi, asili yake ni Medieval Literature (ya Ulaya) ila kwenye rap game bongo imekua introduced na Dizasta na wadogo zake katika game hawajaiona hiyo kuwa ni mbaya na ndomana Maarifa akatoa series ya MAARIFA YA MAARIFA, Rapcha akatoa series ya LISSA, Young Killer SINAGA SWAGA baada ya kuwa inspired na Dizasta.
 
Mstari wako wa kwanza na wa pili, With all due respect I beg to differ kaka mkubwa... Dizasta na underground MCs wengine uliowa mention(nafikiri kwamba unaelewa maana ya underground Hip hop na tofauti kati yake na mainstream Hip hop) wana audience zao kama ambavyo kila aina ya mziki una audience zake.

Dizasta na underground rappers wengine wana watu wao ambao wakitoa bidhaa zao (Albums, T shirts, EPs) wanawasapoti na shows zao wanahudhuria.

Audience ya underground MCs ni ndogo mno hivyo hata hivyo hata sapoti wanayopata haiwezi kuwa sawa na mainstream hip hop artists. Kwa sababu hiyo kumekua na wimbi la wasanii wa huku underground wanaoitamani mainstream na kujikuta wakijaribu ku 'switch' na pia mashabiki ambao wanawalazimisha wasanii wa huko wa switch. Dizasta ni moja wa wasanii ambao wame maintain uhalisia wao kuanzia uandishi na uwasilishaji na huku handakini tunamsikiliza na ku enjoy anachofanya, sisi ndio hadhira yake.
 
Msukuma msukume arudi kwao mwanza/narusha stone liwapate wanaojibanza... ukishaumiza kichwa kwa mstari kama huu unagundua nini? πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Umeiweka vizuri sana kiongozi, awa jamaa watunza misingi hawataki kabisa kupewa ushauri.

Lakini kwa lawama sasa ooh hatupewi airtime hatupewi shows.

Ndio maana One the incredible kaamua kuwa baba lishe
 
[emoji441][emoji441][emoji443][emoji443]nashangaa!! Nashangaa!! Nikimuonaaaa[emoji443][emoji443][emoji441][emoji441]

Nakumbuka kibwagizo cha nyimbo hii ya juma nature
Lakini nyimbo siikumbuki.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Nashangaa nashangaa mimi kuona
Kuona mshikaji wangu wa karibu ananichukia
Na kila nikipita maskani ananiharibia
Nikimuuliza naambiwa sina msaada nae ktk maisha
Ndio maana hivi sasa ameamua kutangaza vita
Chaajabu ni kwamba ameniambia nisione maskani nikipita
Nikitia maguu tu nitakuwa maisha yangu nayahatarisha
Naomba msamaha sana kama nitakuwa nimekukosea
Na sidhani kama kuna mtu akazaliwa akawa hana kosa
Msela acha hasira ya kuniharibia
Kwani sisi sote binadamu tunapita njia
Nashangaa nashangaa mimi kuona
Mshikaji ananichukia na vitu kuchukulia
Nikifikiria mm sijamkosea ila vita tu ananifanyia
Naona azidishe moyo sisi tuishi kwa amani
Apate ya sasa yote ya thamani
Niaje hatupatani kuna msela ana hasira na mm
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
KILA ZAMA NA MFALME WAKE, SIKU HIZI WAMEUFANYA MZIKI RAHIS SANA

ETI WE MPELEKEE MOTO, UNAUA VIBE, SIJUI NIKAGONGEE NYAGI, SPONSOR NIACHIE MY WANGU, MARA PWAA PWAA PWA
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
nashangaa DIZASTA VINA NA MPOTO WAPI NA WAPI
 
Naomba A LIST YA HIPHOP ARTISTE IN TANZANIA RIGHT NOW
 
That is prime Juma Nature πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯

Watoto wa sasa Nature ni shule ya bure, tengenezeni local content msiigize uniga andikeni stories
 
Shukrani sana

Sent from my Moto C using JamiiForums mobile app
 
yani alipojibu tu hapo nikajua hapa hamna kitu hapa.... dizasta hakuna wa kumfananisha nae hapa bongo ...
 
Haha! Yani upige chibuku alafu usikiliz muscular feminist/ tattoo ya asili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…