Bill
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 10,703
- 11,816
1. Kwani kakwambia anataka kuwa mtumishi wa kanisa?Mungu alisema ukioa umefungwa wewe ni wamwanamke mmoja ukiwa na wapili unatenda dhambi maana ulishaapa mbele za Mungu na mbele za watu wote kuwa wewe ni mme wa mkeo so wewe unazini kitu ambacho Mungu hapendi . So mahari isikudanganye kama wewe umeoa ni unazini na mtu mwingine ni dhambi
Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; 1.Timotheo 3:2
Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. 1.Timotheo 3:12
2. Hao Daud na Suleiman unadhani walikuwa hawamjui Mungu hadi wakawa na wake wengi?
3. Mwanaume oa kadri uwezavyo. Sharti ni moja tu kwa mke wa kwanza, soma hapa👇
Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia.
Kutoka 21:10