JWTZ badilikeni, dunia ya sasa hakuna vita ya kuvunja matofali kwa kichwa!

Mbona umehamaki sana . Vile wanayembea kwenye wanakata mauno viwanjani ndio jeshi
 
Hiii kamba kaka kaivuta sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Watu hawapendi kuambiwa tuwadhaifu pande hizo. Ukipita makambini walevi watupu hadi aibu yaani
 
Unavyokiwazia chombo sivyo kabisa yani. Ningekwambia jambo ila najua utaniletea ubishi tu kuna integrated Air Defence System za maana najua huna unachokielewa.
 
Ukiwekeza kwenye teknologia jeshi la foot soldiers "milioni moja na malaki" la nini?
Jeshi la miguu kila nchi lipo( infantry solders) ni sehem ya kamandi ya jeshi.

Tuna kamandi ya jeshi la anga( Airforce)
Tuna kamandi ya jeshi la miguu( infantry)
Tuna kamand ya jeshi la maji( Navy)

Jeshi la miguu la miguu la miguu limegawanyika,

1. Mizinga
2. Vifaru
3. Askari wa miguu au ardhini.

Kwenye uwanja wa medani, hizo kamandi zinaweza kushirikiana kutegemea but inategemea .

Mfn.. Wakati askari wa miguu wanasonga mbele , kumfwata adaui alipo, nyuma , wazee wa mizinga watoa msaada , kumfurusha adui, huku jeshi la miguu la miguu linasonga , na vifaru..

Kikosi cha mizinga kinapokea frequency kutoka kwa captain, au yule msoma Raman, zile frequency ndio zinaonesha maadui walipo , kikosi cha mizinga kinatuma mzinga unaenda kutua pale pale kwenye point walio pewa ..ambako maadui wapo.. Sasa captain ataoe direction tofauti..

Kama kamandi ya anga au Navy wataitajika, wanaingia mzigoni.
 
Kwahyo jeshi lazima liwepo, bila kujali wapo kiasi gani .

Alafu haya mambo ya majeshi, yana usiri sana, RAIA kama ww sio lazima ujue power tuliyo nayo... .
 
Duuuh
 
huna akili kabisa ndg.
acha tukueleweshe. utendaji kazi wa navy seal wanapokuwa ktk operation zao, asilimia kubwa unakuwa supported na zana za kiteknolojia.

huko angani kuna satellite ambazo mmarekani kaziweka ziweze kumsaidia ktk kuspy activities za maadui ili kuwarahisisha kazi navy seal kuvamia ngome ya adui.

katika masuala ya medani, ukusanyaji wa taarifa wa aina hii hufahamika kama imagery intelligence na signals intelligence. kwa asilimia 100 unakuwa supported na zana za kisasa zilizoundwa kwa teknolojia ya hali ya juu.

hoja ya mleta mada ina logic, usiibeze.
 
Kwahyo jeshi lazima liwepo, bila kujali wapo kiasi gani .

Alafu haya mambo ya majeshi, yana usiri sana, RAIA kama ww sio lazima ujue power tuliyo nayo... .
Sawa pamoja na usiri mambo ya jeshi, sote tulishuhudia jinsi jeshi la anga la marekani lilivyo
sambaratisha jeshi la miguu , kikosi cha vifaruu vya Saddam kwa kipindi kisichozidi miezi minne .Air power muhimu modern warfare. Chini ya miezi minne jeshi la footsoldier milioni moja hoi bin taaban .
 
Nilimsikia Kagame anataka kununua S-300 kutoka Russia
Hana hela hiyo, hana adui na wala hana jirani mwenye ndege za kupigwa na S-300 ambayo kwanza hawezi uziwa na Urusi wala hawezi ruhusiwa na US kuinunua.
 
Mleta mada uko very wrong kulinganisha nchi yenye defense budget ya $20 billion dhidi ya nchi yenye $1 billion na point. Bado hatulingani kwenye teknolojia na mambo kibao.

Hiyo Iron Dome unajua kuwa US ndio alifadhiri mradi huo, pamoja na ule mfumo mwingine mkubwa zaidi. Gharama za kufadhiri defense project ni kubwa mno Tanzania hatuwezi.

Kwanza nchi zote ununua silaha kulingana na uhitaji na maadui waliopo. Unanunua air defense nzito vile dhidi ya nani. Vipaumbele havioneshi kama tunahitaji air defense hata hiyo Israel ina silaha zinakoseana idadi kama submarines kwa vile sio kipaumbele na maadui wake hawapigwi kwa hizo wala hawatumii bahari kushambulia.

Nchi inayonunua panpasi na pedi nje ndio unataka itengeneze air defense system?
 
Pamoja na kwamba teknolojia ni muhimu, lakini bado tunahitaji askari wakakamavu.

Teknolojia ina mahala pake, na askari wana mahala pake.

Huwezi kuwa na jeshi la kutumia kompyuta tu. Unahitaji vijana wa kazi.

Halafu pia tunaangalia na mahitaji ya nchi pamoja na aina ya matishio ya kiusalama ambayo tunakabiliana nayo.

Sisi maadui zetu ni nani hasa? Hawa panya rodi na wajinga wajinga wa mpakani?

Ukishabaini aina ya matishio ya kiusalama tuliyonayo, utaona kwa kiasi kikubwa tunahitaji askari wakakamavu badala ya hizo kompyuta.

Bajeti ya nchi pia inazingatiwa. Hatuwezi kuacha kusambaza maji halafu turukie kununua teknolojia ambazo hazina matumizi ya msingi.

Tukombe bajeti yote tukanunue hiyo IRON DOME kwa ajili ya nani?
 
Mi nadhani tuna watu tu wanaovaa nguo za kijeshi lakini si wanajeshi

Dharau hizi
Au sio
Sawa Hamna shida
Kauli Kama hizo sio nzuri ukisikika mbele yao .
Shida utamuachia Mama ako Duniani.
 
Mada hii imekaa Kidharau dharau dhidi ya Jeshi letu la wananchi.. wanakulinda wale Lakini ukiwa Umelala Usingizi na kuendelea na mambo yako kwa Amani.
Mambo yao mengi ni ya Siri.
Na ndo taratibu zao kiutendaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…