JWTZ badilikeni, dunia ya sasa hakuna vita ya kuvunja matofali kwa kichwa!

JWTZ badilikeni, dunia ya sasa hakuna vita ya kuvunja matofali kwa kichwa!

Mkuu inawezekana unapitia magumu sana. Pole sana kwa yanayo kusibu.
Kwa marekebisho tu Mkuu, Israeli ilipigana na nchi zaidi ya 4 kwa mpigo za jirani yake. Majibu uanfahamu kama sikosei.

Nia hayo tu, wako mpendwa katika kujenga Taifa na kuangalia matofali yakipasuliwa uwanja wa Taifa.[emoji23]
 
Ila tanzania sio siri wakubwa ukifikiria kwa makini unabaki kucheka tu tupo kama binadamu wa maonyesho[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa hyo mleta mada unadhan kuna siku TZ itaingia vita na ISRAELI au MAREKANI KWELI?

Adui wa kwanza ni jirani yako,hivyo lzm ujiimarishe kulingana na jirani yako alivyo ie Kenya,Uganda na Nchi nyngne zinazotuzunguka!!
Muondoe Kenya hatumuwezi maisha
 
We mpumbavu kweli wew ...

Hyo israel na parestina ni kama ilala na Temeke.... Town city center tuu!!

Uwez linganisha kwa ukubwa wa nch!!!

Halafu hizo rocket hazipigi zaid ya mail 50 .. . ni jiran mnoo!!!!

Kama uamin!!! Njoo chombon field tukuonyeshe vitu ambavo ujawah kuvifikilia!! M*MAE
Hahahahahahahaha field huko wapi mkuu? Mizinga siku hizi inatumika?
 
Technology ni mhimu ila ata mwili kuwa vizuri ni muhim pia kuna sehem uwez tumia risasi ya moto ili mwili wako unaweza kukuokoa.
Ila ulichokisema kina ukwel kias chake
 
Unawaza kama mimi na hakuna nimekuwa nikikidharau kama kuona wanaoitwa makomandoo wetu wakishindana kuvunja tofali pale taifa, na kuruka kwenye ndege kwa kutumia parachuti,
Unasema tu hiiiiiiiii unanyamaza. Vita leo hii ni sayansi tupu, vita kubwa haziganwi kwa SMG, AK 47 nk, leo hii watu wanacheza na computa Dude linakufata huko huko.
Vita ya bunduki ni kwa ajili ya kupambana na vikundu vya waasi lkn nchi kwa nchi taifa kwa taifa hatuhitaji askari wa kuvunja matofali kwa mikono wala kwa vichwa.
Mzee ni vikundii vya waaasi sio kama ulivyoandika ww apo 🤣🤣🤣🤣
 
Nimekua nikifuatilia vita ya Israel na Hamas huko ukanda wa gaza. Ninachoshangaa hamna ngumi wala kareti ni makombora yanavurumushwa angani kama mvua!

Hiyo ni moja, mbili..

Nimevutiwa jinsi Israel inavyotumia "engineering na science" kulinda nchi yake... kombora zinarushwa kutoka gaza ila zinazo tua ardhini chache sana kutokana na nguvu ya technolojia ya kulinda anga ya IRON DOME.

Yani kombora kabla halija tua lina maliziwa huko huko angani..

Sasa najiuliza hayo makombora yaliyo rushwa kwenda Israel na yakamalizwa kabla hayajatua ardhini je yangetua pale Magogoni au pale posta au pale kariakoo kuna Mtanzania hata mmoja angepona kweli?

Nadhani ni wakati sasa TISS na JWTZ wakaanza kuwekeza kwenye technolojia zaidi maana vita vya kisasa ni technolojia na sio mabavu!!

Unaweza pigwa na kanchi kadogo kisa tu kanatumia technolojia wakati wewe umewekeza kwenye mabavu na kuvunja matofali kwa kichwa!

Dunia ya sasa ni bora uwe na jeshi la watu 1000 wenye IQ kubwa na wenye kuweza kutumia technolojia kuliko uwe na jeshi la watu milioni moja ambao hawajui hata kuwasha kompyuta!

Ajirini vijana wenye IQ/Akili kubwa ili muwatumie katika technolojia na tafiti mbalimbali za kitechnolojia!!

Acheni kuangalia TBC kila saa washa Aljazeera mjifunze kichoendelea huko gaza na jinsi wenzetu wanavyowekeza kwenye technolojia!!

Zindukeni dunia imebadilika hii!!

Naomba kuwasilisha!
Wale ni komando na operarion za komando zinainclude kukutana na adui ana kwa ana hapo ukiwa legelege unapoteza. Inapotokea vita ipo mtaani(mjini) comando huingia kazini ili kukwepa kuumiza wasiohusika.


Jeshi watu 1000 wenye IQ kubwa ni sawa lakini jeshi la israel kanchi kadogo lina watu wengi kuliko jeshi Tz ambayo ni kubwa sana kwa Israel.

Lakini si kwamba majeshi yetu hayahitaji hizi technolojia, tatizo ni hela mdogo wangu(budget)
Hayo makombora unayosikia Israel wanatumia bei zake usiombe, acha bei matunzo yake pia ni ghali sana.

Nakushauri uhimize vijana wenzio kufanya kazi kwa bidii ili nchi yetu ifike huko.
 
Kuna kitu is missing kwenu kuhusu jeshi. Yani mkisikia jeshi mnawaza vita tu, tena vya kumiminiana risasi au kuvurumishiana makombora tu basi

Jeshi ni taasisi mazee...

Wale unaoona wanavunja tofali kwa kichwa usichukulie lelemama mzee inawasaidia kwenye baadhi ya mazingira mfano special mission

Kuna vitengo vingi mule; intelijensia mizinga anga mawasiliano nk kwahiyo hata hao unaosema wa kuwasha kompyuta wapo wengi tu tena wengine serikali inagharamia kabisa kuwapeleka nje kusomea hayo mambo unayoyataja

Kuhusu maonesho huwezi kuonesha mambo ya cyber na maswala mengine ya kiintelijensia kwahiyo muendelee tu kuwa wavumilivu kwani mtaendelea kuona mazoezi ya ukakamavu yakiwemo kubeba mtu kwa meno na kujipigiza chini kwa kichwa

Mwisho kabisa nisikushangae wala kukulaumu kwani nyinyi ndio wale mnaosababisha mtu ajitume zaidi au akate tamaa kabisa. Hamthamini (mnadharau) vya kwenu. Naomba nikuache na swali pia ukipenda unijibu je hizo nchi unazoona wamewekeza zaidi kwenye teknolojia katika majeshi yao hakuna watu/vitengo/maonesho ya kuvunja matofali kwa kichwa?
 
Fact Kama wanataka jesh Bora wakubari kuinvest kwenye modern warfare waache propaganda na majigambo yakumpiga idd Amini saiv watu hawaitumii physical muscles
Muscles bado zina kazi nyingi za kufanya vitani au kwenye operation.
Kuinvest kwenye modern warfare si budget ndogo rafiki yangu.
Kununua ndege za kisasa, meli za kisasa na mizinga na vifaru vya kisasa ni mkwanja ambao si wa kitoto.

A well trained and equiped soldier gharama ya mavazi na vifaa vyake vya kisasa ni zaidi 200m. ( hao wa wa kupasua tofali)

Bado gharama za kutunza ndege, mizinga, meli na huyo soldier.
 
Mleta mada hujui usemacho chulia watu wamekuteka nyara wamekunyanganya silaha utapigana kwa teknolojia ipi zaidi ya kutumia ngumi mateke karate na kichwa chako?

Chukulia watu wanaleta vurugu eneo kama kariakoo ,gari haiwezi ingia je utatumia bunduki kuwapiga risasi wote kwenye vichochoro na mitaa iliyobanana ambayo ina vichochoro vingi?

Vita za ardhini mbali na kutumia silaha zinatuimia ngumi ,mateke na vichwa na karate.Wewe unawaza vita tu ya teknolojia utakuja tekwa mjini ulambwe makofi ubaki unalia tu kama bwege usiyeweza hata kujitetea kwa vichwa ,ngumi na mateke
Mfano wako ni mzuri ila sio relevant sana siku hizi kuna drones zinafika kila mahali na zinauwezo wa kugeuka silaha na kueliminate target ndio maana zimetungiwa sheria ya matumizi

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Dunia ya sasa ni bora uwe na jeshi la watu 1000 wenye IQ kubwa na wenye kuweza kutumia technolojia kuliko uwe na jeshi la watu milioni moja ambao hawajui hata kuwasha kompyuta!

MTU ANAAJIRIWA HADI KUSTAAFU HAJUI KUWASHA COMPUTER, HAKIKA KUNA SHIDA KUBWA SANA
Mzee wa ibara naona unashuka na kifungu kabisa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Kaweke akili charge. Battery low.

Kwa hilo Boko ulilolitoa kama akili zako zingekua zinaCharge a bit......

America wasingekua na wale jamaa wa NAVY SEALS au MARINES ambao wao wanavunja nazi kwa ugoko.

Kacharge akili izo au battery haikai na chaji??????

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Ila kaongea point sana. Sema tu uwasilishaji wake ndo kidogo,tenge. Amesema ni kama analinanga jeshi bila kujua kuwa kila kinachofanyoka jeshini kina umuhimu mkubwa sana.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Ila kaongea point sana. Sema tu uwasilishaji wake ndo kidogo,tenge. Amesema ni kama analinanga jeshi bila kujua kuwa kila kinachofanyoka jeshini kina umuhimu mkubwa sana.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Ndio maana nikamshauri akachaji betri ya akili yawezakana battery low au haikai na chaji.

Unajua madhara ya battery ya akili kutokaa na chaji unakua huna commomsense au inakua haikai sana everytime pia upeo wa kung'amua mambo unakua mdogo

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
maana yangu ni kuwa hata kama una teknolojia kubwaa kiasi gani bado kuna matukio hayahitaji teknolojia kwa mfano japo Marekani ina teknolojia kubwa ila mission ya kumkamata na kumuua Osama ilihitaji special force ili kutoathiri nchi nyingine hali ambayo ingepelekea vita ndo maana Marekani haikutumia drone, missile au kitu chochote zaidi ya hao makomandoo

umepuyanga sana kwenye suala la mission ya marekani kumkamata/kumuua osama bin laden. rudi kwenye makabrasha yako kasome vizuri.

ktk mission hii, teknolojia ilitumika kwa ufanisi wa hali juu sana.

kwa mda mrefu makazi ya osama yalikuwa kwenye surveillance ya setelite za jeshi la marekani. hii ilisaidia jeshi la marekani kufanya covert analysis na kupanga mikakati ya kuvamia eneo lile.

it's through technology, marekani iliweza ku monitor mienendo yote ya wakaazi wa ile nyumba.

chopper iliyowabeba navy seal ilikuwa na teknolojia ya hali ya juu sana ndio maana jeshi la pakistani halikuweza kui-detect kwenye rada yao ndani ya anga la pakistani.

walikuja kushtuka baada ya mission kukamilika. kitendo hiki kilikuwa ni kama dharau kubwa kwa jeshi la pakistan.
Pakistan's army ridiculed after Bin Laden raid

kumbuka mda wote wakati mission hii inaendelea pakistani, rais obama na washauri wake wa masuala ya ulinzi na usalama walikuwa zao white house kwenye chumba kinachofahamika kama situation room wakifatilia hatua kwa hatua kupitia tv screen. haya yote ni matokeo ya uwekezaji mkubwa wa teknolojia. sio mambo ya kuvunja matofali.






IMG_20210519_105713.jpg
 
Back
Top Bottom