Sahihi sana mkuu, vita kuu ya pili ya dunia boats za raia zaidi ya 850 zilikwenda kuokoa askari wa Uingereza na allies ambao tayari walikuwa wamezungukwa,
Zaidi ya skari 336,000 waliokolewa, Operation Dynamo, inaitwa Miracle of Dunkirk, yalikuwa ni maajabu, jeshi la Hitler tayari lilikuwa karibu kuwamaliza askari hao na hawakuwa na mahala pakutokea, lakini kwa upendo wa wananchi waliamua kujitolea kwenda kuwakomboa askari hao, hata hivyo jeshi la Hitler lilijitahidi kuzuia uokozi huo lakini ndio hivyo kwa moyo waliokuwa nao wananchi wakashirikiana na jeshi hatimaye wakafanikisha operation hio ambayo haiwezi kusahaulika Miracle of Dunkirk.
Mfano mwingine tena, jeshi la Marekani wakati linafanya recruitment ya wanajeshi wa kupigana vita ya pili ya dunia kuna vijana wengi walikuwa na miaka 17 na 16 wako under age walidanganya umri wao, idadi yao ni kama 200,000.
Jeshi la Marekani muda wote hushawishi raia kwamba ni sehemu muhimu ya nchi, ni wajibu wa kila mwananchi kulinda nchi yake na jeshi ni kwa ajili yao. Watoto shule za Marekani wakitaka kutembelea kambi ya jeshi wanapokelewa na uongozi wanatembezwa kama kuonyeshwa silaha na kazi zake. Kuna career days wanajeshi wanaenda shule wanauliza nani anataka kuwa mwanajeshi na kufafanua branches za jeshi na kazi zake
Hii ni Youth Army ya Urusi
Uko Israel na South Korea ndio usiseme maana almost kila mwenye afya aliwahi pitia jeshini. Kukutana na fundi seremala ambaye ni Sergeant ndani ya Israel ni kawaida, nchi ina watu wachache na maadui kila kona hivyo raia wote wanajua kupigana. Humtishii mtu na mabuti yako.
Nchi kama hizo zikivamiwa raia hujiona ni wanajeshi na wanajua cha kufanya sio kuanza kufundishana muda huo. Na sio kuanza kuogopa na kuona jeshi ni sehemu ya ukorofi, fujo, ugomvi na uonevu.
Tafsiri ya kuwa mwanajeshi kwa nchi nyingine maana yake discipline yako iko juu, utu wako uko juu, uelewa wako wa kisheria uko juu. Ukienda club ukajitambulisha mwanajeshi hakuna anayekuwa na wasiwasi kwamba utafanya fujo. Hakuna anayekutegemea utachukua sheria mkononi.
Njoo huku sasa mtu akikosa kazi ndio analazimisha kujiunga jeshi, uko akivaa buti anarudi kibanda umiza kulazimisha ugomvi. Sisi mwanajeshi kwa haraka haraka honestly tuna wasiwasi ni mlevi, mzinzi, hana financial discipline, mapenzi yanamtesa hajui kuchagua mke wa kuoa. Tafrani tu