Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Habari Wakuu!
January hii imeanza na mambo mengi lakini Mpaka sasa kwa humu JF kuna mambo Makuu mawili yaliyovuta usikivu wa wengi, Jambo la Kwanza ni Uchaguzi wa CHADEMA, na lile la Pili, ni Kitabu cha Kabendera.
Kwanza nikiri, Sina hicho kitabu, hivyo sijakisoma. Lakini kupitia utangulizi nilioupata kutokana na interview aliyofanyiwa Mwandishi wa kitabu hicho, Muhtasari alioutoa umetoa picha kuwa Kitabu hicho kinahusu nini na kina lenga nini.
Lengo kubwa kabisa la Kitabu hicho, ni kuonyesha Mabaya, ushenzi, na maovu ya Magufuli iwe yalikuwa yanajulikana au Yale ambayo yalikuwa hayajulikani.
Kwa lugha za mtaani, Kitabu hicho kimelenga kumuanika na kumkaanga vibaya Hayati JPM.
Mimi sina tatizo na Jambo hilo ikiwa yaliyoandikwa humo ni KWELI.
Ishu Ipo kwenye Matokeo, je Kitabu hicho kitakuwa na athari yoyote kwa Watu, hasa Tabaka la chini ambalo ndio kundi kubwa la Watanzania?
Hapa jibu ni Hapana.
Kitabu hiki hakitakuwa na athari zozote kwa Watanzania wengi. Kwa sababu zifuatazo;
1. Watanzania wengi sio wapenzi WA kusoma vitabu.
Hivyo kwenye Watanzania Milioni 60 Kitabu hicho hakiwezi kusomwa hata na Watanzania Laki Moja.
Na watakaofanikiwa kukisoma ni kundi la Tabaka Fulani la juu na lile la Wasomi.
2. Kitabu kipo kwa Lugha ya kingereza.
Kusoma vitabu ni changamoto kwa Watanzania. Sasa unapowaongezea Lugha ya kingereza Watanzania wengi waliochini ya Dola Moja ambao Lugha hiyo ni changamoto ni wazi hawatasoma.
3. Kitabu kinamsakama Magufuli ambaye ni wazi ni kipenzi cha Watanzania waliowengi.
Ingawaje Mimi Taikon Mtibeli sikufurahishwa na Mifumo na mienendo ya utawala wa Magufuli lakini hiyo haimaanishi kuwa sikuona jinsi Watanzania wengi walivyokuwa wanampenda Magufuli.
Nachelea kusema, Magufuli ndiye Rais aliyekuwa anapendwa zaidi na Watanzania kuliko Rais yeyote tangu nchi hii ipate Uhuru.
Kwa Watanzania, Magufuli ni kama Mtume wao. Hata ungemsema kwa ubaya gani wao wangemtetea, wasingekuamini.
Kabendera na Kitabu chake Hana namna yoyote hata angekuja na ushahidi WA video kuonyesha unyama wa Magufuli bado Watanzania wengi wangekataa katakata na kusema video hiyo ni AI.
4. Kabendera licha ya kuwa Watanzania wengi hawamjui lakini ikitokea wakamjua watamhusianisha na kibaraka wa Mabeberu.
Kwa nature ya Watanzania wengi walivyo, Kabendera hawezi kusema lolote la maana au kumsema vibaya Magufuli na Watanzania wakamuelewa.
Kabendera atakuwa labelled kama kibaraka tuu wa Mabeberu
Na Kitabu chake hakina maana yoyote kwa Jamii ya kitanzania.
Kitabu cha Kabendera ingawaje kwa Sisi Watibeli kinaweza kuwa kumbukumbu ya kihistoria, na kuonyesha madhaifu ya Mfumo wetu na Katiba yetu,
Lakini kwa Watanzania, Kitabu hicho hakitapewa uzito kihivyo.
Kwa upande wa Wazungu, Kitabu hicho hakina mambo yoyote mapya ya kutisha KW sababu mambo yote yaliyotajwa humo kwa Wazungu sio mageni pale waonapo viongozi wa Afrika au nchi zisizoendelea au zinazoendelea.
Haya!