Kabendera, Kitabu pekee hakina nguvu ya kumfanyia Mtu Character Assassination kwenye nchi Maskini hasa za Afrika

Tatizo la nchi hii illiteracy ni kubwa sana, uamuzi wa kuandika Kiingereza ni wa mwandhishi, ingawa umefunga macho aliposema atatafsiri kwa Kiswahili. Naona bado unayo mentality za kijamaa bado, kwani lazima watanzania wote wakisome? Pili Kabendera ameandika kwa lugha ya Kiingereza ambayo ni pamoja na lugha ya Kiswahili ni lugha zinazotumika kwa mawasiliano na businesses, sasa wewe kama tu lugha inakushinda na inafundishwa tangu darasa la kwanza basi una shida ya uelewa mdogo sana., narudia tena, umedanganywa na ujamaa wa kijinga, unasema hakuna tabaka nchi hii? Nani anaendelea kukudanganya? Wanaoishi Oysterbay , Masaki, Mikocheni ni sawa na wanaoishi Manzese, Tandika na Gogo la Mboto? Tanua akili yako kaka, hata China na Russia matabaka yapo, ukijitahidi ukatoboa utakuwa na maisha mazuri ila wewe kadanganye wenzako kuwa unajua sana Kiswahili...Utabaki tabaka la kutawaliwa.....Jipe moyo.
To sum up, acha kudanganya watanzania, Siyo kweli kuwa Magufuli ni rais aliyependwa nchi hii kuliko yeyote, kwa lipi? Ulifanya utafiti upi? Nafuu ungesema mashirika ya Pew na mengine yalimpa alama kidogo, yakafungiwa.....Hayo ndiyo ya ukweli. Hakuna rais aliyewahi kupendwa sana nchi hii...wote walikuwa na matatizo mengi sana. Uwe unasema ukweli.
 
Lengo siyo kufanya character assasination, lengo ni kuuhuhabarisha ulimwengu kuwa tulikuwa na mtu dhalimu kupindukia pale Ikulu ili kizazi kijacho kiwe makini.

Naamini kizazi kijacho kitatengeneza hata sinema kuhusu huyu mtu dhalimu.

R.I.P Ben Saanane
R.I.P Azory Gwanda
R.I.P wote waliowema waliouawa na wasiojulikana
 
Na wewe ni wale wale tu kama kabendera,Hakuna tofauti ya wewe na yeye

Umejaa mambo ya hearsay

Umehoji kundi la wasukuma halafu unatoa hitimisho watanzania kumbe umehoji kundi la wasukuma wa kabila lake
Wapi nimehoji Wasukuma?
Wasukuma umewatolea wapi kwenye post hii?

Takwimu kuwa magufuli alipendwa sana umezitoa wapi ?
Hilo hata ungekuwa kipofu usingeshindwa kuona kwenye akili yako kuwa Magufuli alikuwa anapendwa Sana na Watanzania wengi.

Kama kitabu hujakisoma unatoa wapi nguvu ya kuandika vitu ambavyo unavisikia bila uhakika huo ni umbea tu
Soma maelezo, kwenye uzi wangu utaelewa nguvu ya kuandika nimetolea wapi.
Kabendera mwenyewe ndiye katoa muhtasari wa kile alichoandika. Huo muhtasari kwa Sisi watunzi na waandishi inatosha kujua Kitabu kinaujumbe gani na kimelenga nini hasa

Unapoongelea Tanzania kwani Magufuli alikuwa ana mamlaka zanzibar? Umewahi uliza wanzibar kama walimpenda Magufuli?

Unaposema Tanzania unazungumzia Watanzania wote. Hiyo ya kusema Zanzibar ni yako
 
Ukweli ukikataliwa hugeuka uongo na uongo ukikubaliwa huwa ni UKWELI [emoji28][emoji28]
Ukweli upi umekataliwa ?

Umeshasema kitabu cha kabendera hujakisoma ,Sasa mbona unageuka mchambuzi

Kama hujakisoma kitabu acha waliokisoma waandike

Vitabu vya dini kuna watu wameacha legacy kwenye bibilia na quran lakini watu bado wanawajadili kwa maovu yao kila wakati

Yuda Iskarioti kila Pasaka anajadiliwa

Mfalme Suleiman kila wakati watu wanamsem na wake na masulia yake

Legacy haitetewi ,inajitetea yenyewe
 

Unazungumzia mambo usiyoyaelewa.

Watanzania hivyo vitabu vya Kiswahili vyenyewe hawasomi sembuse vya kingereza?

Hayo Mengine ya Matabaka nafikiri ubongo wako umejigusa baadhi ya nerves, zikatoa kitu kingine ambacho Mimi Wala sijakisema
 

Unaishi Tanzania?
Nimekuambia Kwa Watanzania wengi Magufuli ni Nabii
 
Takwimu umezitoa wapi kuwa watanzania walimpenda Magufuli?

Huna authority ya kuanzisha hii mada wakati kitabu umekiri hujakisoma.

Usipende kujadili mambo ambayo huyafahamu na hauna takwimu
 
Mkuu
Kama unajua watanzania hawapendi kusoma

Jaribu na wewe ku summirize maandishi yako

Unaandika maelezo mengi unneccessary huku ukitambua watanzania hawapendi kusoma
Kumbe naye creche wa uwasilishaji
 
Takwimu umezitoa wapi kuwa watanzania walimpenda Magufuli?
Sio kila Jambo linahitaji Takwimu. Ninyi wenye Elimu za kukariri ndio maana hata mambo madogo yanawashinda.

Huna authority ya kuanzisha hii mada wakati kitabu umekiri hujakisoma.
Unazungumzia authority ipi?

Usipende kujadili mambo ambayo huyafahamu na hauna takwimu
Wewe unapojadili hapa unanifahamu?
 
Umechambua vizuri Ila kuhusu Magufuli kupendwa sana hii sio kweli

Magufuli ndo rais Pekee alipokufa watu walikesha bar kunywa na kula .

Japo Mimi nilikuwa namkubali Ila watz wengi walikuwa hawampendi .
Acha uongo wa Tz wasiye mpenda labda wewe na ukoo wenu
 
Muhimu ujumbe umefika na umezingatia. Kunaweza kusiwe na impact leo lakini kuna siku itatumika kufanya marejeo mabadiliko yatapohitajika.

Tanzania au mabadiliko wapi?

Unauhakika nchi hii itakuwepo Miaka miatatu ijayo?
 
Kuna mambo hayahitaji takwimu wala Tafiti.
Magufuli ni habari nyingine kwa Watanzania waliowengi. Kwao ni kama Nabii.

Sisemi kishabiki nazungumzia ukweli uliopo
Usipende kuandika mambo kwa ujumla jumla hapa JF

Una uhakika watanzania wengi ni maskini au wewe ndiwe maskini?

Unaposema watanzania hawajui kiingereza ,Usiandike kwa ujumla jumla .labda watu wako wa karibu ndio hawajui kiingereza

Dunia ya teknolojia leo unaweza tafsiri kichina ,kijerumani kwa lugha yako.Wewe hutumii AI ?Hicho kitabu ndani ya AI ni siku ngapi unasoma kwa kiswahili?

Kwa mujibu wa wizara ya elimu ,Elimu ni bure na watoto wanajifunza kiingereza toka shule ya msingi au ule mtihani wa kiingereza wanafunzi wanajibu kwa kiswahili
 
Umechambua vizuri Ila kuhusu Magufuli kupendwa sana hii sio kweli

Magufuli ndo rais Pekee alipokufa watu walikesha bar kunywa na kula .

Japo Mimi nilikuwa namkubali Ila watz wengi walikuwa hawampendi .

Mkuu, hata viongozi Wakubwa wa nchi wanajua wananchi wakawaida walimkubali Sana JPM.

JPM aliweza kuwa-manipulate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…