Kabendera, Kitabu pekee hakina nguvu ya kumfanyia Mtu Character Assassination kwenye nchi Maskini hasa za Afrika

Kabendera, Kitabu pekee hakina nguvu ya kumfanyia Mtu Character Assassination kwenye nchi Maskini hasa za Afrika

Watanzania kuwalaghai ni Jambo rahisi Sana. Hilo Magufuli alifanikiwa

..jambo lingine ni kwamba wananchi wa kawaida waliotendewa unyama wakati wa Magufuli hawajapata mahali pa kueleza dhuluma waliyopitia.

..so far waliozungumza kadhia zao ni wanaharakati, na hao kwa haiba zao ni wapambanaji. Sasa watu wa aina hiyo sio rahisi kupata huruma ya wanaowasikiliza na kubadilisha mtizamo wa jamii kuhusu utawala wa Magufuli.

..Kama unampenda sana Magufuli na hutaki achafuke basi endelea kuomba kwamba watu wa kawaida aliowadhulumu wasipate jukwaa la kueleza waliyopitia.
 
Robert amezungumza jambo halisi. Watanzania si watu wa hivyo hata ikitokea hao watu wameweka ushahidi wa video bado kuna watu wengi watakataa watasema za kutengeneza. Hata pia ikitokea kabendera amesema aliyoandika alikurupuka si ya kweli bado watu wengi watasema kabendera katishwa, alichoandika ni ukweli

Haya yote mnayobishana toka jana hakuna kundi litakubaliana na mwingine. Lissu amesema chadema Kuna rushwa ya abdul, wapo wanaoamini na wapo wasioamini, hata lissu akiweka ushahidi bado kuna ambao hawataamini. Ikitokea pia lissu akasema alikurupuka bado watasema lissu nae kalambishwa asali. Ukishaelewa hili huu ubishani haitakuwepo tena

Kuna mtu nilimpa mifano juzi kuwa kina lowassa, rostam, karamagi, chenge na wengine waliimbwa mafisadi kwa miaka nenda rudi. Je nani Leo anaimba tena hao Ni mafisadi? Nani anaamini tena hao Ni mafisadi? Ukijua jamii yetu ilivyo huwezi kupata nayo tabu ndio maana ccm wanafanya like wanachotaka
 
Una ubongo wa kufikiri vema.
 
Umeongea kweli kabisa mkuu Mtibeli, hicho kitabu kusema ukweli hakitasomwa na wengi na kitawahi kuchuja sana masikioni mwa watanzania kama tu ilivyokuwa kwa kitabu cha wale jamaa kina Meena na wenzake.

Suala la watanzania kumpenda Magu liko wazi sana sijajua watu wengine wanachangamana na watanzania kwa kiwango gani maana kila penye mikusanyiko ya watu huwezi kukuta Magu anasemwa kwa mabaya na mpaka kuna baadhi ya sehemu watu bado wanapiga mpunga kila wiki kwa kuweka tu mkusanyiko wa hotuba za jamaa na kuna siku maalumu ya kusikiliza na watu wanajaa ukumbini.

Magu ni rais pekee nchi hii ambaye ameonyesha uthubutu wa kusimamia rasilimali za nchi na zikaleta manufaa makubwa ndani ya muda mfupi, kwa watanzania Magu ni kielelezo cha maamuzi magumu.

Nenda mashuleni kote asilimia kubwa kunapokuwa na debate zinazohusu uzalendo mfano pekee inaotumika wa kuwaonyesha watanzania uzalendo ni jina la mwamba JPM. Na mpaka wanashauri viongozi wetu wawe wachapakazi, wathubutu na wazalendo kama Magu.

Ukiacha udhaifu mkubwa wa kuogopa challenge Magu alilitendea vyema sana taifa hili kuliko kiongozi mwingine yeyote nisijue sana kwa Nyerere ila ukipitia mitandaoni na mijadala mbalimbali Magu ni kama anakubalika kwa kiwango kikubwa sana. Na hata ikifanyika poll yoyote humu au popote bado Magu atawaacha mbali sana kina Mkwere na Samia. Kumbuka hata utafiti waliofanya gazeti la mwananchi ulitoa matokeo ya Magu kushinda japo watawala waliopo hawakuridhishwa nao ikabidi mwananchi waombe msamaha.

Magu hachafuki kwa vitabu labda itokee flyover za Dar zivunjwe zote, SGR ihujumiwe, bwawa la Nyerere lipotee mazingira ya kutatanisha, mahospitali aliyojenga tuamue kufugia kuku, stand na masoko makubwa aliyoyajenga tusiyatumie, ikulu ya chamwino tuichome moto, daraja la busisi lipigwe bomu liteketee, ukarabati mkubwa wa shule kongwe uliofanyika uharibiwe makusudi, barabara alizojenga zisipitike, ukuta wa mererani tuuvunje, watu waliowekewa umeme kwa gharama ya Tshs 27000 wahamishwe wote nchini iwekwe imani nyingine kwa wakazi wapya watakaoletwa, ndege alizonunua tuzihujumu zote na mengine mazuri mengi aliyofanya ndipo tunaweza tukamsahau huyu mtu mchapakazi ambaye hajawahi kutokea nchini mwetu.
Hizo madaraja au flyovers na Ikulu ya Chamwino inakusaidia nini? umeme wa REA siyo yeye aliyeanzisha kaka, ni Mkapa ndiye aliyeanzisha. Huongelei uwanja wa ndege wa Chato unaonekana sasa sehemu ya kuanikia mpunga. Ndiyo Magufuli amefanya nchi yetu imekuwa ya ovyo sana, uliza ndugu zake. Eti alijenga kanisa lake Chato, mbona Katoliki walikataa. Wewe unaona daraja la Busisi la maana, kwani wewe huoni shida zingine nchi hii iliyokuwa nayo? Daraja siyo tija kaka, kuna mambo mengi tu, watu wamekufa kwa Covid-19 yeye alidanganya ili watu wafe.
 
..jambo lingine ni kwamba wananchi wa kawaida waliotendewa unyama wakati wa Magufuli hawajapata mahali pa kueleza dhuluma waliyopitia.

..so far waliozungumza kadhia zao ni wanaharakati, na hao kwa haiba zao ni wapambanaji. Sasa watu wa aina hiyo sio rahisi kupata huruma ya wanaowasikiliza na kubadilisha mtizamo wa jamii kuhusu utawala wa Magufuli.

..Kama unampenda sana Magufuli na hutaki achafuke basi endelea kuomba kwamba watu wa kawaida aliowadhulumu wasipate jukwaa la kueleza waliyopitia.

Mkuu sizungumzii Kumpenda au kumchukia Magufuli Hapa.
Nafikiri umeleta Jambo jipya.

Nazungumzia impact ya Kitabu cha kabendera Kwa Watanzania wengi ni chini ya 1%
 
Ni sahihi Kabisa

Ila lengo la kitabu halitafikiwa ambalo ni ukweli wa kuharibu Legacy ya JPM na heshima aliyonayo kwa Watanzania waliowengi
Wewe mwenyewe una promote kitabu husika kisha unasema lengo halitafanikiwa???? Lengo lipi na kwanani?
 
Mkuu sizungumzii Kumpenda au kumchukia Magufuli Hapa.
Nafikiri umeleta Jambo jipya.

Nazungumzia impact ya Kitabu cha kabendera Kwa Watanzania wengi ni chini ya 1%

Kwani impact ya kitabu cha mzee Mwinyi kwa Watanzania ni kiasi gani?. Kwa hiyo ndo kitabu kisiandikwe?

Kitabu kikiandikwa maana yake kitasomwa na vizazi zaidi ya 1000 vijavyo, na hivyo ndivyo civilization inavyojengwa.

Wewe unadjani kwa kuwa watanzania wa leo hawapendi kusoma, hiyo ndo itakuwa excuse ya kutoandika vitabu?
 
Magufuli yupo kaburini mwaka wa pili ama wa mwaka wa tatu huu, bado watu waanahangaika Na kivuli chake.

Namna sahihi ya kumfuta Magufuli Ni kuua miradi yote aliyopigania kama SGR, Mwalimu Nyerere Hydroelectric Power, Kigongo-Busisi Bridge, Magufuli Bridge (Posta-Masaki), Flights kutaja miradi michache...ikiwa hii miradi itaendelea kuishi, hakuna andiko litamchafua Magufuli
Umemaliza kila kitu Kuna kenge watabisha ila ndo ukweli
 
Magufuli yupo kaburini mwaka wa pili ama wa mwaka wa tatu huu, bado watu waanahangaika Na kivuli chake.

Namna sahihi ya kumfuta Magufuli Ni kuua miradi yote aliyopigania kama SGR, Mwalimu Nyerere Hydroelectric Power, Kigongo-Busisi Bridge, Magufuli Bridge (Posta-Masaki), Flights kutaja miradi michache...ikiwa hii miradi itaendelea kuishi, hakuna andiko litamchafua Magufuli
Wakiifuta hii na Wao wanakua wamejifuta
 
..jambo lingine ni kwamba wananchi wa kawaida waliotendewa unyama wakati wa Magufuli hawajapata mahali pa kueleza dhuluma waliyopitia.

..so far waliozungumza kadhia zao ni wanaharakati, na hao kwa haiba zao ni wapambanaji. Sasa watu wa aina hiyo sio rahisi kupata huruma ya wanaowasikiliza na kubadilisha mtizamo wa jamii kuhusu utawala wa Magufuli.

..Kama unampenda sana Magufuli na hutaki achafuke basi endelea kuomba kwamba watu wa kawaida aliowadhulumu wasipate jukwaa la kueleza waliyopitia.
Mpk Leo hawajapata jukwaa ? Anavyochukiwa Magufuli huku watu wangekosa kuwatafutia jukwaa hao watu ? Miaka inaenda wanamsubiri jukwaa ?
 
Habari Wakuu!

January hii imeanza na mambo mengi lakini Mpaka sasa kwa humu JF kuna mambo Makuu mawili yaliyovuta usikivu wa wengi, Jambo la Kwanza ni Uchaguzi wa CHADEMA, na lile la Pili, ni Kitabu cha Kabendera.

Kwanza nikiri, Sina hicho kitabu, hivyo sijakisoma. Lakini kupitia utangulizi nilioupata kutokana na interview aliyofanyiwa Mwandishi wa kitabu hicho, Muhtasari alioutoa umetoa picha kuwa Kitabu hicho kinahusu nini na kina lenga nini.

Lengo kubwa kabisa la Kitabu hicho, ni kuonyesha Mabaya, ushenzi, na maovu ya Magufuli iwe yalikuwa yanajulikana au Yale ambayo yalikuwa hayajulikani.
Kwa lugha za mtaani, Kitabu hicho kimelenga kumuanika na kumkaanga vibaya Hayati JPM.

Mimi sina tatizo na Jambo hilo ikiwa yaliyoandikwa humo ni KWELI.

Ishu Ipo kwenye Matokeo, je Kitabu hicho kitakuwa na athari yoyote kwa Watu, hasa Tabaka la chini ambalo ndio kundi kubwa la Watanzania?
Hapa jibu ni Hapana.

Kitabu hiki hakitakuwa na athari zozote kwa Watanzania wengi. Kwa sababu zifuatazo;

1. Watanzania wengi sio wapenzi WA kusoma vitabu.
Hivyo kwenye Watanzania Milioni 60 Kitabu hicho hakiwezi kusomwa hata na Watanzania Laki Moja.
Na watakaofanikiwa kukisoma ni kundi la Tabaka Fulani la juu na lile la Wasomi.

2. Kitabu kipo kwa Lugha ya kingereza.
Kusoma vitabu ni changamoto kwa Watanzania. Sasa unapowaongezea Lugha ya kingereza Watanzania wengi waliochini ya Dola Moja ambao Lugha hiyo ni changamoto ni wazi hawatasoma.

3. Kitabu kinamsakama Magufuli ambaye ni wazi ni kipenzi cha Watanzania waliowengi.
Ingawaje Mimi Taikon Mtibeli sikufurahishwa na Mifumo na mienendo ya utawala wa Magufuli lakini hiyo haimaanishi kuwa sikuona jinsi Watanzania wengi walivyokuwa wanampenda Magufuli.

Nachelea kusema, Magufuli ndiye Rais aliyekuwa anapendwa zaidi na Watanzania kuliko Rais yeyote tangu nchi hii ipate Uhuru.

Kwa Watanzania, Magufuli ni kama Mtume wao. Hata ungemsema kwa ubaya gani wao wangemtetea, wasingekuamini.

Kabendera na Kitabu chake Hana namna yoyote hata angekuja na ushahidi WA video kuonyesha unyama wa Magufuli bado Watanzania wengi wangekataa katakata na kusema video hiyo ni AI.

4. Kabendera licha ya kuwa Watanzania wengi hawamjui lakini ikitokea wakamjua watamhusianisha na kibaraka wa Mabeberu.
Kwa nature ya Watanzania wengi walivyo, Kabendera hawezi kusema lolote la maana au kumsema vibaya Magufuli na Watanzania wakamuelewa.
Kabendera atakuwa labelled kama kibaraka tuu wa Mabeberu
Na Kitabu chake hakina maana yoyote kwa Jamii ya kitanzania.

Kitabu cha Kabendera ingawaje kwa Sisi Watibeli kinaweza kuwa kumbukumbu ya kihistoria, na kuonyesha madhaifu ya Mfumo wetu na Katiba yetu,
Lakini kwa Watanzania, Kitabu hicho hakitapewa uzito kihivyo.

Kwa upande wa Wazungu, Kitabu hicho hakina mambo yoyote mapya ya kutisha KW sababu mambo yote yaliyotajwa humo kwa Wazungu sio mageni pale waonapo viongozi wa Afrika au nchi zisizoendelea au zinazoendelea.

Haya!
Ni kweli kabisa hata Mimi Niko nusunusu,ila Jamaa kama ni kweli aliua mtu Ikulu,alitenda jambo baya sana!
 
Lengo siyo kufanya character assasination, lengo ni kuuhuhabarisha ulimwengu kuwa tulikuwa na mtu dhalimu kupindukia pale Ikulu ili kizazi kijacho kiwe makini.

Naamini kizazi kijacho kitatengeneza hata sinema kuhusu huyu mtu dhalimu.

R.I.P Ben Saanane
R.I.P Azory Gwanda
R.I.P wote waliowema waliouawa na wasiojulikana
Mkuu upo Safi kabisa!
 
Watanzania wengi waliishi kwa unafiki kwasababu ya mfumo aliouweka haikuwa rahisi watu ku reveal hisia zao hadharani.

Lakini bado naungana na wewe kuwa watu walikuwa wanampenda (ila napinga factor ya kusema walikuwa ni wengi)

Kuna watu wamepata kazi kwenye mifumo ambayo iliharibiwa na connection.

Kuna watu walidhurumiwa na watu wenye nguvu lakini kupitia yeye haki zao zililipwa.

Kiukweli amefanya mengi kuigusa jamii na hilo nitakuwa mjinga kama nitapinga.

Kama binadamu nakubali kuwa alikuwa na mapungufu yake na pia alikuwa na mazuri yake.

Lakini katika mapungufu ya binadamu kuna mzani ambao mapungufu hayo tunayapima na kuangalia ni kwa kiasi gani tunaweza kuya ignore na ku move on na mazuri.

Mfano tunaweza kutambua kuwa ndoa zina changamoto na hizo changamoto zinakuja kwa mapungufu ya binadamu.

Mume ambaye alikuwa anamjali sana mke wake kwa kufanya kila kitu cha kumridhisha ikiwemo kumnunulia zawadi mbalimbali ili awe na furaha.

Then siku ikatokea mke amezidisha chumvi kwenye chakula halafu reaction ya mume ikawa ni kumgombeza kwa ukali.

Wote tukisimuliwa hicho kisa basi katika mizani ya mapungufu ya binadamu tunaweza kuona hiyo kama ni sehemu ya weakness ya mwanaume na pengine tukamshauri mwanamke a-move on.

Lakini kama story hiyo ikawa mume kuishia kumchinja na kisu mke wake kwasababu ya kuzidisha chumvi, hatuwezi kusema ni mapungufu ya binadamu kwa kitendo hicho.

Na kwamba tunapaswa kuachana na mabaya hayo na kukumbuka mazuri ya huyo mwanaume kwa jinsi alivyompa zawadi mbalimbali mke wake hadi kwenye siku ya birthday yake.

Hiyo haiwezi kuwa sawa

Lazima tukubaliane kuna viwango vya ubaya ambavyo mtu ukivifanya unakuwa umevuka mstari. Watu hawawezi kuona thamani ya yale mazuri uliyoyafanya.

Magufuli kama kweli alihusika na hayo mauaji tena kwa mkono wake basi hoja ya kusema alisaidia sijui kupata lami itakuwa ni ujinga unless huyo aliyeuliwa ithibitishwe alikuwa jambazi aliyehatarisha maisha ya raisi kwa wakati huo.

Nje na hapo utabaki kuwa utetezi irrational tu. Na ukitaka kujua how it feels jiweke kwenye nafasi za familia za hao wahanga kisha pima hoja za kuonesha mazuri ya JPM kama zitakuwa valid kwako.
Hili la kujua kama ni kweli,imefumba mdomo wangu na Akili imehama!
 
Back
Top Bottom