Kabendera, Kitabu pekee hakina nguvu ya kumfanyia Mtu Character Assassination kwenye nchi Maskini hasa za Afrika

Habari Wakuu!

January hii imeanza na mambo mengi lakini Mpaka sasa kwa humu JF kuna mambo Makuu mawili yaliyovuta usikivu wa wengi, Jambo la Kwanza ni Uchaguzi wa CHADEMA, na lile la Pili, ni Kitabu cha Kabendera.

Kwanza nikiri, Sina hicho kitabu, hivyo sijakisoma. Lakini kupitia utangulizi nilioupata kutokana na interview aliyofanyiwa Mwandishi wa kitabu hicho, Muhtasari alioutoa umetoa picha kuwa Kitabu hicho kinahusu nini na kina lenga nini.

Lengo kubwa kabisa la Kitabu hicho, ni kuonyesha Mabaya, ushenzi, na maovu ya Magufuli iwe yalikuwa yanajulikana au Yale ambayo yalikuwa hayajulikani.
Kwa lugha za mtaani, Kitabu hicho kimelenga kumuanika na kumkaanga vibaya Hayati JPM.

Mimi sina tatizo na Jambo hilo ikiwa yaliyoandikwa humo ni KWELI.

Ishu Ipo kwenye Matokeo, je Kitabu hicho kitakuwa na athari yoyote kwa Watu, hasa Tabaka la chini ambalo ndio kundi kubwa la Watanzania?
Hapa jibu ni Hapana.

Kitabu hiki hakitakuwa na athari zozote kwa Watanzania wengi. Kwa sababu zifuatazo;

1. Watanzania wengi sio wapenzi WA kusoma vitabu.
Hivyo kwenye Watanzania Milioni 60 Kitabu hicho hakiwezi kusomwa hata na Watanzania Laki Moja.
Na watakaofanikiwa kukisoma ni kundi la Tabaka Fulani la juu na lile la Wasomi.

2. Kitabu kipo kwa Lugha ya kingereza.
Kusoma vitabu ni changamoto kwa Watanzania. Sasa unapowaongezea Lugha ya kingereza Watanzania wengi waliochini ya Dola Moja ambao Lugha hiyo ni changamoto ni wazi hawatasoma.

3. Kitabu kinamsakama Magufuli ambaye ni wazi ni kipenzi cha Watanzania waliowengi.
Ingawaje Mimi Taikon Mtibeli sikufurahishwa na Mifumo na mienendo ya utawala wa Magufuli lakini hiyo haimaanishi kuwa sikuona jinsi Watanzania wengi walivyokuwa wanampenda Magufuli.

Nachelea kusema, Magufuli ndiye Rais aliyekuwa anapendwa zaidi na Watanzania kuliko Rais yeyote tangu nchi hii ipate Uhuru.

Kwa Watanzania, Magufuli ni kama Mtume wao. Hata ungemsema kwa ubaya gani wao wangemtetea, wasingekuamini.

Kabendera na Kitabu chake Hana namna yoyote hata angekuja na ushahidi WA video kuonyesha unyama wa Magufuli bado Watanzania wengi wangekataa katakata na kusema video hiyo ni AI.

4. Kabendera licha ya kuwa Watanzania wengi hawamjui lakini ikitokea wakamjua watamhusianisha na kibaraka wa Mabeberu.
Kwa nature ya Watanzania wengi walivyo, Kabendera hawezi kusema lolote la maana au kumsema vibaya Magufuli na Watanzania wakamuelewa.
Kabendera atakuwa labelled kama kibaraka tuu wa Mabeberu
Na Kitabu chake hakina maana yoyote kwa Jamii ya kitanzania.

Kitabu cha Kabendera ingawaje kwa Sisi Watibeli kinaweza kuwa kumbukumbu ya kihistoria, na kuonyesha madhaifu ya Mfumo wetu na Katiba yetu,
Lakini kwa Watanzania, Kitabu hicho hakitapewa uzito kihivyo.

Kwa upande wa Wazungu, Kitabu hicho hakina mambo yoyote mapya ya kutisha KW sababu mambo yote yaliyotajwa humo kwa Wazungu sio mageni pale waonapo viongozi wa Afrika au nchi zisizoendelea au zinazoendelea.

Haya!
Kijitabu chenyewe kimeandikwa kwa kimombo. Maybe, amewalenga akina nshomile wenzake.
 
Mjitahidi mkisome chote, Hajaandikwa Magufuli pekee, ila ni ishara nzuri ya kuweka vitu kwenye vitabu hata kama jamii haipendi kusoma. Hii ni njia moja wapo kwa kuelekea kuwa na jamii bora baadae.
 
MAREHEMU WA KWANZA KUITAWALA TANGANYIKA.HONGERA MZILANKENDE,,Kabendera kametumwa katachanika na upepo.
 
..jambo la msingi ni UKWELI kuwekwa wazi.

..vilevile WAHANGA waliopotezwa wakati wa Magufuli kuwekewa kumbukumbu sahihi.
Na hawa wanaopotezwa sasa je? Ni Magufuli.

Tufikiri kwa kuchwa badala ya mkundu. Njaa zisitubadilishe akili.

Na uninga wa kabendera ukilelewa, Samia ajiandae kuchafuliwa vilevile.

Haiwezekani iandikwe alitaka kubakwa halafu mwandishi hakanywi na usalama wa taifa wananeng'eneka badala ya kuchukua hatua.
 
..unashauri nini kifanyike ili vitendo vya utekaji, utesaji, na mauaji, vikome?
 
Walikuja na kile sijui the state ikabuma leo wako na hii nayo chaliii kesho watakuja na filamu ila ndani ya nafsi zao dhamira inawasuta pamoja na madhaifu ambayo kila binadamu anayo ukweli ni kwamba Magufuli aliipenda sana Tanzania kutoka moyoni na aliidhihirisha kwa vitendo,kitu ambacho hawajui ni kwamba wanamuongezea umaarufu kila uchwao na hata sasa kuelekea oktoba 2025 wamejiharibia saaanaaa sababu Samia na Kikwete hawauziki kwa wapiga kura.

Ccm imerudi zama za JK ukivaa vazi lao uku mtaani wanazomewa km mafisadi na watekaji/wauaji na hao Mafisadi wasifikiri wapo salama au wameshinda vita kuna kitu kinakuja hakika yule wanayemuita Mhutu wa Chato atawanyamazisha huko huko kaburini alipo.

Na hii mbegu Tiss wanaiyopanda ndanj ya Taifa hili teule inazidi kumea na kwa hakika hata vizazi vyao haviko salama kwani Tanzania siyo ya kwao peke yao Karma itarudi kwa kishindo kikuu.JPM hakuna msafi nchi hii anayeweza kumchafua zaidi ya kumuongezea umaarufu kwa Watanzania 75% kumbuka zile kura za maoni zilizosababisha gazeti la mwananchi kupewa onyo na baadaye kufungiwa kwa kisingizio cha kibonzo.

Kama kuuwa nao wanaua uchaguzi wamechafua ufisadi umerudi kwa kasi nyongeza ya mishahara hakuna pesa za mikopo za Tanganyika zinajenga kizimkazi na Zenji Mkataba wao wa Korea Kusini Rais wa kule anaandamwa na Tiss ya kule kwa ufisadi mkubwa how come mtu mmoja ajimilikishe hili Taifa na kisha kuwafanya Watanzania wote maiti kama alivyosema Mzee Kenyatta.
days are numbered.
TANGANYIKA FC DRC.
 
Attachments

  • 1736094254889.jpg
    1736094254889.jpg
    234 KB · Views: 2
  • 1736094229895.jpg
    1736094229895.jpg
    149.2 KB · Views: 2
Habari Wakuu!

January hii imeanza na mambo mengi lakini Mpaka sasa kwa humu JF kuna mambo Makuu mawili yaliyovuta usikivu wa wengi, Jambo la Kwanza ni Uchaguzi wa CHADEMA, na lile la Pili, ni Kitabu cha Kabendera.

Kwanza nikiri, Sina hicho kitabu, hivyo sijakisoma. Lakini kupitia utangulizi nilioupata kutokana na interview aliyofanyiwa Mwandishi wa kitabu hicho, Muhtasari alioutoa umetoa picha kuwa Kitabu hicho kinahusu nini na kina lenga nini.

Lengo kubwa kabisa la Kitabu hicho, ni kuonyesha Mabaya, ushenzi, na maovu ya Magufuli iwe yalikuwa yanajulikana au Yale ambayo yalikuwa hayajulikani.
Kwa lugha za mtaani, Kitabu hicho kimelenga kumuanika na kumkaanga vibaya Hayati JPM.

Mimi sina tatizo na Jambo hilo ikiwa yaliyoandikwa humo ni KWELI.

Ishu Ipo kwenye Matokeo, je Kitabu hicho kitakuwa na athari yoyote kwa Watu, hasa Tabaka la chini ambalo ndio kundi kubwa la Watanzania?
Hapa jibu ni Hapana.

Kitabu hiki hakitakuwa na athari zozote kwa Watanzania wengi. Kwa sababu zifuatazo;

1. Watanzania wengi sio wapenzi WA kusoma vitabu.
Hivyo kwenye Watanzania Milioni 60 Kitabu hicho hakiwezi kusomwa hata na Watanzania Laki Moja.
Na watakaofanikiwa kukisoma ni kundi la Tabaka Fulani la juu na lile la Wasomi.

2. Kitabu kipo kwa Lugha ya kingereza.
Kusoma vitabu ni changamoto kwa Watanzania. Sasa unapowaongezea Lugha ya kingereza Watanzania wengi waliochini ya Dola Moja ambao Lugha hiyo ni changamoto ni wazi hawatasoma.

3. Kitabu kinamsakama Magufuli ambaye ni wazi ni kipenzi cha Watanzania waliowengi.
Ingawaje Mimi Taikon Mtibeli sikufurahishwa na Mifumo na mienendo ya utawala wa Magufuli lakini hiyo haimaanishi kuwa sikuona jinsi Watanzania wengi walivyokuwa wanampenda Magufuli.

Nachelea kusema, Magufuli ndiye Rais aliyekuwa anapendwa zaidi na Watanzania kuliko Rais yeyote tangu nchi hii ipate Uhuru.

Kwa Watanzania, Magufuli ni kama Mtume wao. Hata ungemsema kwa ubaya gani wao wangemtetea, wasingekuamini.

Kabendera na Kitabu chake Hana namna yoyote hata angekuja na ushahidi WA video kuonyesha unyama wa Magufuli bado Watanzania wengi wangekataa katakata na kusema video hiyo ni AI.

4. Kabendera licha ya kuwa Watanzania wengi hawamjui lakini ikitokea wakamjua watamhusianisha na kibaraka wa Mabeberu.
Kwa nature ya Watanzania wengi walivyo, Kabendera hawezi kusema lolote la maana au kumsema vibaya Magufuli na Watanzania wakamuelewa.
Kabendera atakuwa labelled kama kibaraka tuu wa Mabeberu
Na Kitabu chake hakina maana yoyote kwa Jamii ya kitanzania.

Kitabu cha Kabendera ingawaje kwa Sisi Watibeli kinaweza kuwa kumbukumbu ya kihistoria, na kuonyesha madhaifu ya Mfumo wetu na Katiba yetu,
Lakini kwa Watanzania, Kitabu hicho hakitapewa uzito kihivyo.

Kwa upande wa Wazungu, Kitabu hicho hakina mambo yoyote mapya ya kutisha KW sababu mambo yote yaliyotajwa humo kwa Wazungu sio mageni pale waonapo viongozi wa Afrika au nchi zisizoendelea au zinazoendelea.

Haya!
Shida ya watanzania ni uelewa mdogo na viwango vya chini na hawa wanamwona Magufuli kuwa nabii wao.
 
Tatizo la nchi hii illiteracy ni kubwa sana, uamuzi wa kuandika Kiingereza ni wa mwandhishi, ingawa umefunga macho aliposema atatafsiri kwa Kiswahili. Naona bado unayo mentality za kijamaa bado, kwani lazima watanzania wote wakisome? Pili Kabendera ameandika kwa lugha ya Kiingereza ambayo ni pamoja na lugha ya Kiswahili ni lugha zinazotumika kwa mawasiliano na businesses, sasa wewe kama tu lugha inakushinda na inafundishwa tangu darasa la kwanza basi una shida ya uelewa mdogo sana., narudia tena, umedanganywa na ujamaa wa kijinga, unasema hakuna tabaka nchi hii? Nani anaendelea kukudanganya? Wanaoishi Oysterbay , Masaki, Mikocheni ni sawa na wanaoishi Manzese, Tandika na Gogo la Mboto? Tanua akili yako kaka, hata China na Russia matabaka yapo, ukijitahidi ukatoboa utakuwa na maisha mazuri ila wewe kadanganye wenzako kuwa unajua sana Kiswahili...Utabaki tabaka la kutawaliwa.....Jipe moyo.
To sum up, acha kudanganya watanzania, Siyo kweli kuwa Magufuli ni rais aliyependwa nchi hii kuliko yeyote, kwa lipi? Ulifanya utafiti upi? Nafuu ungesema mashirika ya Pew na mengine yalimpa alama kidogo, yakafungiwa.....Hayo ndiyo ya ukweli. Hakuna rais aliyewahi kupendwa sana nchi hii...wote walikuwa na matatizo mengi sana. Uwe unasema ukweli.
Mkuu mhurumie huyo akili ndogo mwandishi Kanjanja
 
Kama watanzania wa sasa hawataelewa Kuna kizazi kitakuja kumuelewa na kifahamu magufuli aliokuwa ni kiongozi wa namna Gani kwahiyo itawasaidia kuwa makini pindi watakapo takiwa kuchagua kiongozi hasa katika ngazi ya urais kutokana na kumba maandisi yanadumu kwa vizazi vingi kwahiyo kwasasa unaweza usione impact ya kitabu hiki
 
Hata hivyo kuna kitabu kingine cha yule prof wa zambia kinachomsifia Magu kitasomwa pia kwahiyo tusichukulie hivi vya kumkashifu pekee ndivyo vitasomwa baada ya miaka 200
 
Umechambua vizuri Ila kuhusu Magufuli kupendwa sana hii sio kweli

Magufuli ndo rais Pekee alipokufa watu walikesha bar kunywa na kula .

Japo Mimi nilikuwa namkubali Ila watz wengi walikuwa hawampendi .
Watanzania wa level gani unaowazungumzia?..
Tembea Tanzania ukiwa na free mind na uulize watu,utapata majibu..
Magufuli amefariki lkn ndie Rais anayetajwa kila siku kuliko hata Nyerere .
Nguvu kubwa inayoweza kutumika kujaribu kumfifisha,ndio inazidi kumpandisha juu zaidi.
Kama wewe ni mmoja wa watu waliokuwa wanapigwa pini na Magu..lazima ulikesha bar kusherehekea..
 
Back
Top Bottom