Katika jambo ambalo umekosea ni kuniita mimi MUONGO.
Ngoja ninukuu, kisha utakanusha haya nayo yanukuu :
Hotuba ya Khalifa wa Kadiani iliyochapishwa katika Al-Fadl, Agosti 21, 1927 chini ya kichwa Advice for Students’ kinawafafanulia wafuwasi wake tofauti kati ya Ahmadiya na wasio Ahmadia. Anasema “... Kwa kuwa Kristo aliyeahidiwa alisema kuwa. Uislamu wao, Allaah wao na hija yao nitofauti na zetu, daima tunatofautiana nao kwa killa kitu.”
Nanukuu :
"Mnamo Julai 30,1931 Al-Fadl likachapisha hotuba nyingine ya Khalifa wa Kadiani ambapo alielezea ugomvi uliotokea baina ya Makundu mawili. Moja likatowa hoja kuwa kwa vile tofauti kati ya Makadiani na Waislamu zinajulikana, na Kristo aliyeahidiwa amekwishazifafanuwa hakuna haja ya kuanzisha shule binafsi za kadiani: tunaweza kuyasoma yale mambo yote yasiyo na ubishani katika shule za Waislamu. Makundi mengine yakakataa. Huku bado wakibishana, Kristo mwenyewe aliyeahidiwa akaingia na kusikiliza mabishano yao. Kisha akatowa hukumu hii, akisema: “Ni makosa kusema kuwa tunatofautiana na Waislamu katika suala la kifo cha Yesu tu. Tunapingana nao katika yote; Allaah, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), Qurian, sala, hija na zaka. Kwa kifupi aliwafafanulia kuwa tunatofautiana kabisa na Waislamu kwa mambo yote yanayohusiana na dini”.
Mwisho wa kunukuu.
Haya ni madai tu kama madai mengine. Unatakiwa uthibitishe hili, mimi nakuuliza swali au maswali yafuatayo :
1. Utume unaendelea au umekoma ?
2. Yesu amekufa au yuko hai ?
3. Mirza Ghulam Ahmad ni nani ?
4. Asiyekuwa Kadiani kwenu nyinyi ni nani ?
Ukithibitisha ya kuwa Ukadiani ni Uislamu mimi nakuwa Kadiani.
Najua huwezi kuonyesha uongo wangu hata chembe.
Twende taratibu, Mirza Gulam Ahmad ni nani ni muumini kama ulivyo wewe au ni mtume au nabii ?
Usilete malalamiko, na uwe mkweli.
Haya unayasema wewe ila uhalisia hauko hivyo. Kinachonena kwa kasi sana siku hizi ni elimu sahihi juu ya UISLAMU.