Maana ya Neno Uislamu Kilugha
Kilugha, Uislamu unamaanisha kujisalimisha, kunyenyekea na kutii. Dini hii ndio inaitwa Uislamu kwa sababu ni dini yenye msingi wa kusalimu amri za Allah na kuzitii.
Maana Yake Kiistilahi
Ni njia ya maisha, mfumo wenye misingi ya imani na matendo ya kuwafanya watu wapate furaha kamili duniani na ahera, iliyotumwa na Allah na kufikishiwa watu kupitia kwa mitume. Uislamu ni sheria ya kiungu inayowaongoza watu wenye akili kuelekea mambo mazuri kulingana na hiari zao.
Yaliyomo katika Uislamu
Maana ya Uislamu ni kujisalimisha: kujisalimsha kwenye amri na makatazo ya Allah. Uislamu hautakuwepo bila ya kujisalimisha kwenye hukumu za Allah.
(Angalia al-An'am, 162 na an-Nisa, 65) Mwanadamu ni mja aliyeumbwa na Allah.
Kwa kuwa Allah amekizingira kila kitu kwa elimu Yake na kwa kuwa Yeye ana hekima, sharti la utumwa ni kujisalimisha Kwake. Sheria za uhai humshurutisha mwanadamu kujisalimisha kwa Allah kwa sababu Allah ndiye anayezijua zaidi sheria hizo na anamjua zaidi mwanadamu.
Ulimwengu na kila kilichomo ndani mwake hutii sheria za Muumbaji huyo. Kwa hivyo, dini ya ulimwengu wote ni Uislamu. Jua, mwezi na nyota, vyote hivyo vinafuata Uislamu. Kwa kuwa Uislamu unamaanisha kumtii Allah na kujisalimisha Kwake, tunaona kwamba viumbe vyote hivyo vinamtii Allah bila ya kuasi. Yaani, tunashuhudia kwamba vinajisalimisha na kwamba vyote vinafuata Uislamu.
Soma zaidi:
Uislamu ni nini? Unaweza kutoa maelezo ya kina kuhusu Uislamu? | Maswali juu ya Uislamu