Wewe elimu yako ni ya ajabu sana, unaponukuu kitu ni lazima useme kwamba hiyo ni tafsiri ya maandiko fulani original na maandiko hayo ni lazima uyaambatanishe ili tuone kama ulichotafsiri ni sahihi, mfano kama tafsiri zote za Qur'an tukufu duniani zingekuwa haziambatanishwi na aya halisi za Qur'an katika lugha yake ya asili ya kiarabu unadhani leo hii Qur'an ingekuaje???--- si ingekuwa kama Biblia ambayo haina maandiko ya uasilia wake kiasi kwamba kila mtu au kanisa linayotafsiri yake na idadi ya vitabu vyao katika Biblia kiasi kwamba ni vurugu tupu.
Unapotoa nukuu ya tafsiri ni lazima useme imepatikanaje, kwa suala la Alfadhl kama nilivyosema, ni jarida lilikuwa likitokewa katika miaka hiyo kwa lugha ya kiurdu, sasa tuambie hiyo tafsiri yako kutoka katika hiyo Alfadhl umeitafsiri kutoka kiurdu, kiingereza au kutoka katika lugha ipi??? au umekopi hiyo tafsiri???, toa majibu mkuu!!!.
Ipo hivi; Ahmadiyya tunavyo vitabu vingi sana, majarida, Magazeti, makala.mbalimbaki nk, na umekuwepo mchezo wa wapinzani wa Ahmadiyya kuchukua maandiko yetu na kuyabadilisha au kuyaweka katika tafsiri zao ili tu kupotosha ukweli ili jumuiyya yetu ionekane si chochote bali jumuiyya inayokwenda kinyume na mafundisho ya Uisilamu sasa ili kuepusha jambo hilo ndio maana kwanza ninataka ORIGINAL URDU SCRIPTS ZA HIYO TAFSIRI YAKO ULIYOTUWEKEA ili kuondoa utata na baada ya hapo mambo mengine yatafuata, kama wewe.ni mkweli na huna hila chafu kwanini unashindwa kutuwekea hiyo Alfadhl ulimochukua hiyo tafsiri yako????.
"Leo tutajua kafiri ni nani kati yako na mimi"
Ni husuda dhidi ya hii jumuiya ya Waisilamu wa Ahmadiyya ndio inawatafuna sio kitu kingine.
Kipenzi chetu Mtukufu mtume Muhammad (saw) alipata kusema juu ya husuda:-
اياكم و الحسد فان الحسد ياكل الحسنات كما تاكل النار الحطب
Yaani; "Jiepusheni na hasadi kwani hakika hasadi inakula wema (wa mtu) kama jinsi moto unavyokula kuni"
Sasa tunaona jinsi hasadi inavyokula wema wenu hadi mnashindwa kuleta ushahidi wa kashfa zenu dhidi yetu bali mmebaki kutukana na kulalama tu.
Msikie Shk Amri Abeid Kaluta anavyosema juuu ya matukano na uongo:-
Usemapo neno;
Pasi ujuzi mtimilifu;
Utauma meno;
Ujaposutwa udanganyifu;
Nayo matukano;
Mtukanayo na kukashifu;
Ndiyo msumeno;
Utakereza zenu sharafu.