Kabla hatuja wafundisha "Wasiomini Mungu" juu ya uwepo wake, basi inafaa sisi "Tunaoamini Mungu" tumalize tofauti zetu

Ukiona mtu anakujibu vile husingaike nae uwezo wake wa kufikiri ndio ulipoishia
 
Hapo mkuu nina maswali rukuki. Kuhusu tamaduni yetu pia Africa. Kwa sasa ngoja nisome comments za watu
 
Wewe huiamini Biblia, nimeinukuu kwa sababu ya watu kama wewe, mnaoamini maandiko ya watu mnasema ya Mungu.

Biblia hata Yesu mwenyewe hajawahi kuiona wala kuisikia. Na sisi tunawanukulia hiyo hiyo mjisute wenyewe.
Biblia ni kitabu Cha vitabu sasa wewe useme ni vitabu gani Yesu hakuwahi kuviona ,

Hujajibu kwa nini Allah alisaidiwa mpaka na majini kutengeneza quran
 

Mungu anataratibu zake za jinsi ya kuwafikia wanadamu. Biblia Agano la Kale ilikuwa njia aliyoamua kuitumia hapo awali kuwafikia watu baadaye Agano Jipya ambalo ni muendelezo wa yaliyotabriwa katika Agano la Kale. Agano la Kale linafanana kwa kiasi kikubwa na Kitabu cha dini ya kiyahudi ambacho kimsingi ndio asili yake. Dini ya Kiyahudi ilianzia naTaifa la Israeli ambalo ndilo Mungu aliliteua kuwafikishia watu wake ujumbe kwa kuanzia na Ibrahim hii ilikuwa muda si mrefu baada ya gharika ya Nuhu. Ibrahim alitengwa kutoka waabudu mizimu na miungu mawe, miti, milima, nyota, jua na vya aina hiyo.
 



Al fadl ndio kitu gani??---- labda ungesema katika jarida la Al fadhl hapo kidogo ningekuelewa kwani jarida la Al fadhl limeanza kuchapisha katika jumuiya ya Waisilamu wa Ahmadiyya tangu mwaka 1913 katika lugha ya kiurdu kabla ya jarida la hilo kuanza pia kuchapishwa katika lugha ya kiarabu, nukuu ya tafsiri katika kiswahili uliyoweka hapa bado inatia mashaka kwani katika miaka hiyo jarida hilo lilikuwa linaandikwa kwa lugha ya kiurdu bila shaka wewe utakuwa umetafsiri hiyo nukuu kutoka katika tafsiri ya kiingereza ya maadui wa Ahmadiyya!!---- hivi ni lini adui yako anaweza kuandika jema kutoka kwako ikizingatiwa uadui wenyewe ndio unatokana na jambo hilo hilo analolitolea tafsiri??!!.

Sasa ili usije sutwa uongo fanya hivi; tuletee hapa nukuu original ya kiurdu na ukurasa wa hiyo nukuu yako kutoka kwenye hilo jarida Al fadhl na sio kutuwekea tafsiri ama za kiingereza au kiswahili ili tuondoke na Shaka, mimi sijui Kiurdu lakini ninao watu wanaojua vyema kiurdu na Kiswahili ambao watatusaidia kutoa tafsiri lakini lazima tafsiri iwe sambamba na maandiko yake katika lugha original ya kiurdu ili kuondoa ubishi na ushindani.

Nashukuru umeuliza maswali haya:-

(1) Utume unaendelea au umekoma katika uisilamu??
(2) Yesu amekufa au yupo hai??
(3) Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad ni nani??
(4) Asiyekuwa kadiani kwenu nyinyi ni nani??


Maswali haya hayahitaji majibu ya short cut bali mjadala mpana wa swali moja baada ya jingine kwani nukuu za Qur'an na hadithi ni muhimu katika majibu. Kama upo tayari katika mjadala kwa masharti ya kuwa na hulka za kiislamu katika mjadala mimi nipo tayari na tuanze mada moja baada ya nyingine na rejea iwe ni Qur'an na hadithi za Mtume wetu mtukufu Muhammad (saw).

Na kabla ya yote unapaswa ufafanue kadiani ni nani???
 

Naandika kwa kifupi sana kwasababu kwa haya maswali yako wewe unajua tayari kwa kiasi kikubwa.

Ni kweli Kaini na Abel walikuwa ndugu. Vilevile ni kweli kulikuwa na Sadaka za kuteketezwa. Kwa mujibu wa Biblia Takatifu ndugu hawa wawili walipotoa Sadaka ya kuteketezwa kwa Mungu ya Kaini ilikataliwa na ya Abel ikakubaliwa na Mungu.

Umesema vizuri kuhusu moyo wa Kaini na Mungu kwa Neema yake alimpa njia ya kufuata ili na yeye sadaka yake ikubaliwe. Akaamua kukaidi na matokeo akatenda dhambi ya kumuua Abeli. Hii roho ya Kaini ni dhahiri ndio iliyo kuwa ya lusifa/ shetani kule mbinguni. Na ikamfanya afukuzwe Mbinguni na akatupiwa duniani baada ya kuasi. Ukitulia utaona hiyo roho ilimuingia Ismaili na ikasababisha watimuliwe na mama yake kutoka kwa bayake Ibrahim. Ukienda kwa Essau utaiona hiyo roho ikionesha vimelea vyake pia.

Sadaka ya kafara/ kuteketezwa ndio ilikuwepo. Ni kweli hata Ibarihim alikuwa akiitoa hadi Mungu alimjaribu akitaka amtoe mwanae wa pekee wa Agano na Mungu aiitwaye Isihaka. Zingatia sana maneno haya "Mwanae wa Pekee wa Agano na Mungu."

Sadaka hii ya kafara ilitolewa kwa ajili ya mwandamu kupatana na Mungu aka kusamehewa dhambi. Na ndio maana ilihusisha kumwagika kwa damu za wanyama . Kwenye damu kuna uhai na uhai huo wa wanyama ulitolewa baada ya toba ili uchukue nafasi ya uhai wa mwanadamu mdhambi ambaye angeliupozea kama asinge tubu.

Ni muhimu kujua kuwa Ibrahim aliamriwa na Mungu wakati flani badala ya wanyama wa kafara alitakiwa kumtoa mwanawe wa pekee Isihaka na Mungu alimzuia baadaya ya kuwa kesha mfunga na kumlaza kwenye madhabahu ya kafara ilibakia tu kumchinja lakini Mungu akampa Ibrahim mwanakondoo kwa njia ya mujiza aliyetolewa mahali pa Isaka.

Ikumbukwe kuwa hii sadaka ya Ibrahim kujaribiwa na Mungu kupitia kumtoa Isaka kama sadaka ya kafara/ kuteketezwa ilikuwa ni UNABII makhususi kabisa wa Mungu kwa wanadamu. Unabii huo ulikuja kutimia kwa Mungu kutoa Mwanae wa Pekee Yesu Kristo wa Nazareti Aliye Hai kusulubishwa Msalabani ili Damu Yake ya Thamani kuu itumike kama mbadala wa Sadaka ya damu ya Kafara ya wanyama once and for all. Ndiposa jibu la kukoma kwa sadaka ya kafara kwa Mungu lilipo. Hakuna damu ya myama yoyote yule awaye, hata iwe ya binadamu, nyangumi, tembo nini ngamia bana itakayo tolewa izidi Damu ya Mwana pekee wa Mungu( Bwana Yesu). Wanaotoa sadaka za kafara hii leo kama wameshasikia Habari Njema Kwa Watu Wote ya Bwana Yesu ni kuwa Neema ya Mungu imewapitia pembeni. Wamemua kuukataa huu ukweli kama Kaini na ni kwa hasara yao ya milele yote.
 
Mtume hasemi uongo.
Jua lipo moja Kwa mujibu wa Muhammad alafu anasema tusipo liona linakuwa limeenda kwa Allah kusujudu , tukiliona inamaana limesujudu na Allah kaliruhusu kutokea tena ,

Embu tueleze tofauti ya mda inatokeaje? Mfano unakuta sisi tz tunaliona Jua ila marekani hawalioni
 

Wakati huo ambao wamarekani hawalioni jua taweza kusema Allah yuko Afrika. Kwa maneno mengine Allah is not omnipresence kwa hiyo imani husika.
 
Nimecheka sana, naona unakimbia kivuli chako, ila hapa utanyoosha maelezo.

Nakusudia Jarida hilo hilo la Al-Fadhl. Hayo ya kuanza lini hapa hayana nafasi, unachotakiwa ukosoe hicho nilicho kiweka na uweke kilicho sahihi kwa ushahidi.

Nyinyi si mna Khalifa una kataa hilo ? Kilichonukuliwa sahihi au siyo sahihi ? Upi usahihi wake ?

Nakuuliza swali hamna majarida yenu mliyo yafanyia tarjama katika lugha nyingine ? Sasa kwanini hii hoja dhaifu unataka kuisimamia ?

Wapo maadui waadilifu ndiyo maana tunanukuu toka kwenye majarida yenu.
Hapa usikimbie hoja kijana, kosoa nilicho kiweka hapa, mimi sina nakala ya Kiurdu wala sikijui kiurdu, wewe mwenye nayo tuwekee hapa na uende kwenye nukta ya mzozo moja kwa moja. Ila kijana unachekesha sana hata kukimbia hoja unaikimbia kizembe sana.


Kijana acha uongo hakuna hata swali moja hapo lenye kuhitaji maelezo sababu kila kitu kipo wazi. Wala hakuna swali lenye kuhitaji mjadala mpana.

Haina shida kabisa kwa masharti hayo, ila naongezea hapa sharti lazima iwe kwa ufahamu wa maswahaba. Siyo kwa ufahamu wa Mirza Ghulam Ahmad, kisha utatuambia mwishoni alikufaje kufaje Mirzah Ghulam Ahmad.

Kadiani ni wale wafuasi wa Mirzah Ghulam Ahmad na wamepewa jina kwa sababu Mirzah alitokea katika kijiji cha Kadian.
 
Mwezi uko mmoja au iko mingi ? Kuna nchi yenye kupishana masaa 24 na nchi nyingine ? Sasa kwanini unauliza maswali ya kitoto namna hii ?

Unauliza maswali ya kitoto sana ujue ? Jua lina tembea na lina chomoza mashariki na kuzama magharibi, kwahiyo kila mmoja ataliona kulingana na kituo chake.
 
Wewe ndio una akili za kitoto huelewi, umethibitisha Jua ni moja na ukasema tusipo liona Yani kama saa 12 hivi linakuwa limeenda kwa Allah kusujudu ,

Sasa mda huo huo hatulioni ila marekani wanaliona ndio unatakawa uelezee inakuwaje , linakuwa limeenda marekani au limeenda kwa Allah kusujudu
 
Embu thibitisha kisayansi Jua linatembea
 
Embu thibitisha kisayansi Jua linatembea
Jua linachomoza wapi na kuzama wapi ?

Pili, Sayansi siyo mizani ya majibu katika hili, sababu wanasayansi wameandika uongo juu ya hili japokuwa wapo walio jaribu kusema ukweli kama vile Kina Albert Michelson katika kadhia yake na Albert Einstein.

Tatu, katika ujinga ambao Wanasayansi wanawachezea akili watu ni huo.

Nne, mimi nakupa kazi wewe uthibitishe ya kuwa Jua halitembei Kisayansi ukiweza naacha kutumia jf leo hii rasmi.

JUA LINATEMBEA NA LINA VITUO VYAKE LILIVYO PANGIWA NA MOLA WAKE.
 
Mola wako anasema lisipo onekana saa 12 zote linakuwa limeenda kusujudu , sasa elezea marekani wanaliona na tz limeenda kusujudu inakuwaje?
 
Mola wako anasema lisipo onekana saa 12 zote linakuwa limeenda kusujudu , sasa elezea marekani wanaliona na tz limeenda kusujudu inakuwaje?
Jibu swali nililo kuuliza.

Maswali uliyo uliza nimeshakujibu. Jibu maswali yangu.
 
Jibu swali nililo kuuliza.

Maswali uliyo uliza nimeshakujibu. Jibu maswali yangu.
Hakuna maswali , inajulikana na sayansi kwamba Jua halitembei , ila Dunia ndio inajizungusha na inazunguka , na hii ndio inaweza jibu swali la tofauti wa mda

Ila swala la Allah kusema Jua linaondoka kwenda kusujudu kwa saa 12 halijibu tofauti ya mda Kati ya nchi na nchi
 
Mpaka mnakufa hakuna anae weza kuthibitisha ya kuwa Jua halitembei wala Dunia inazunguka kwenye Muhimili wake.

Soma tafiti za hao wanao jiita Wanasayansi, usilete uzembe na utoto.

Nasubiri majibu ya maswali yangu.
 
Biblia ni kitabu Cha vitabu sasa wewe useme ni vitabu gani Yesu hakuwahi kuviona ,

Hujajibu kwa nini Allah alisaidiwa mpaka na majini kutengeneza quran
Biblia yoyote ile uipendayo, iwe ya Roman Catholic, iwe ya Protestants, iwe ya Orthodox au iwe version yoypte uipendayo, Yesu hajawahi kuziona wala hazijuwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…