Kabla hatuja wafundisha "Wasiomini Mungu" juu ya uwepo wake, basi inafaa sisi "Tunaoamini Mungu" tumalize tofauti zetu

Waulize wale wanazuoni wa Kiislam/ masheikh wabobezi wa ukosoaji wa Ukristo jinsi wanavyohangaika kutumia Biblia kuonesha ya kwamba Bwana Yesu alitabiri /aliwaahidi wafuasi wake ujio wa Roho Mtakatifu ambaye ndiye mtume Muhamad SAW.
Niwaulize nini ?
 
Natumaini mpaka muda huu utakuwa umeshiba, sasa karibu tufanye mjadala kibusara.

Tuliishia pale ambapo ulisema unaweza kuthibitisha wewe ni muislam
Nilishathibitisha hilo tayari.

Kingine unakubali kama wewe ni mjinga tena mpumbavu juu ya UISLAMU ?
 
Thibitisha haya maneno yako uliyobwabwaja hapa.
 
Mzee nithibitishie mimi apa kuwa islamic ni dini pekee Mungu alithibitisha
 
Kwa hiyo Mokaze anapingana na maneno ya muhamad?
Unaniuliza mimi tena, si umesema yeye ni Muislamu na Ukadiani huujui. Nilikuuliza unakubali kama wewe ni Mjinga na huujui UISLAMU ? Hivi ndivyo nilimaanisha. Utakataa tena kama siyo MJINGA.

Yaani mtu kama wewe haiwezi kuwa ajabu kusema Mola hayupo kwa sababu hayupo au ukatumia Logic wakati haina uwezo huo.
 
Nakuuliza wewe uliyesema Mokaze sio muislamu, tena ikiwezekana uniambie na hayo maneno anayoyapinga
 


Ndugu zangu Kisai na Scars mimi sikutaka kujihusisha na hii mada aslan lakini kwakuwa mmenitaja nadhani watu wangependa kusikia kutoka kwangu majibu ya; Muisilamu ni nani ???.

Mimi nitajibu swali Muisilamu ni nani?? Kwa mujibu wa Qur'an tukufu na hadithi za Mtukufu kipenzi chetu Mtume wetu Muhammad (saw).

Qur'an:-

Katika Qur'an (49:14) Waarabu waliojiunga katika dini ya Uislamu walisema:-

قلت العراب امنا

Yaani: Waarabu hao walisema tumeamini. Allah anamwambia mtukufu mtume awajibu hao waarabu:-

قل لم تومنوا و لكن قولوا اسلمنا و لما يدخل الامان في قلوبكم

Yaani:- waambie bado hamjaamini isipokuwa semeni mmekuwa waisilamu (mmesilimu) kwakuwa imani bado haijaingia nyoyoni mwenu.

Hapo sasa utaona kuna vitu viwili vinazungumzwa; 1-- Imani, 2-Kusilimu (mtu kuwa muisilamu), yaani mtu anaweza kujiita Muisilamu na sio kosa ila mtu kujiita muumini hapo inaweza kuwa ni kosa kwani inategemeana na jinsi imani ilivyoingia moyoni mwake na yule anayeweza kujua imani ya moyoni mwa mtu ni Allah na mtume aliyefunuliwa tu, hivyo hakuna mtu anayeweza kumtoa mtu mwenzake katika Uisilamu mtu ambaye anajiita yeye ni Muisilamu.

------Hadithi #1,

Wakati fulani Mtukufu mtume Muhammad (saw) aliwaagiza masahaba zake kufanya sensa ya waisilamu Katika mji wa Madina, masahaba wakamuuliza tutamjuaje Muisilamu?? Yeye akawajibu:-

قال اكتبوا لي من تلفظ بالاسلام

Yaani: aliwaambia muorodhesheni yule anayejiita Muisilamu.

Na hao Masahaba (watu wa sensa) wakasema:

فكتبنا له الفا خمسمانة رجل

Yaani: basi tukaorodhesha wanaume1500.

Sahih Bukhari , kitabu jihad, Babul kitabul immami nas 56/265.

Hapo sasa utaona Mtukufu mtume (saw) anawaagiza watu wa sensa wamuhesabu mtu yeyote anayejiita MUISILAMU, wala mtu hapo hakuukizwa imani yake bali akijiita Muisilamu tu ilitosha kuhesabiwa kwenye sensa kwamba yeye ni Muisilamu.

------Hadithi #2, yafunga mchezo.

Mtume mtukufu Muhammad (saw) akimueleza Muisilamu nin nani alisema:--

من صلى صلاتنا و استقبل قبتنا و اكل ذبيتنا فذالكم المسلم

Yaani; yule anayeswali jinsi tunavyoswali, anayeelekea qibla chetu na anakula dhabihu zetu huyo ni Muisilamu.

Sunan Nasai kitabul iman wa sharaih Bab sifatul Muslim 47/13.

Sasa ni nani anayeweza kuwa na jeuri ya kumtoa mtu yeyote katika uisilamu yule anayetekeleza hayo mambo yaliyoainishwa na mtukufu mtume wetu kipenzi chetu (saw)??!!.

Ni ujinga mkubwa mtu kujipa wadhifa wa kuwatoa watu kwenye uisilamu kwa ujinga huo ipo siku mtu atajipa wadhifa wa kujua nani ataingia motoni au peponi, utadhani dini ya Uisilamu ni mirathi waliorithi kutoka kwa Babu na Baba zao na hivyo kujipa mamlaka ya kuwatoa na kuwaingiza watu kwenye Uisilamu.

Shame on them.
 
Nakuuliza wewe uliyesema Mokaze sio muislamu, tena ikiwezekana uniambie na hayo maneno anayoyapinga
Umekubali kwamba wewe ni MJINGA katika hili ?

Unawajua MAKADIANI ?

Huo muda sina, mpaka ukiri hilo. Hatulei wajuaji sisi.
 
Huyo jamaa kwa namna ambavyo anataka sisi tumuone anaweza fanya chochote ili tuamini yeye ndio muislamu pekee humu.
 
Umekubali kwamba wewe ni MJINGA katika hili ?

Unawajua MAKADIANI ?

Huo muda sina, mpaka ukiri hilo. Hatulei wajuaji sisi.
Kuonesha kuwa mtu ni mjinga kuna hitaji consent?

Btw jamaa amejibu hapo juu na ameonesha namna gani ulivyo snitch
 
Kuonesha kuwa mtu ni mjinga kuna hitaji consent?

Btw jamaa amejibu hapo juu na ameonesha namna gani ulivyo snitch
Unaendelea kuonyesha wazi kabisa UISLAMU huujui, maelezo yake yote aliyo yatoa hayajibu swali langu. Kwanini sijamjibu ? Kwasababu ametumia Hadithi sehemu ambayo si yake na hii ndiyo kawaida yao. Mfano Hadithi ya sensa ile ilikuwa kwa ajili ya tukio maalumu katika masuala ya vita, ili kuwajua nani wa kuwaua na nani wakuwaacha.

Kingine akatumia hadithi ya kuhusu kuwa Muislamu ni usali kama alivyo sali mtume, lakini wenyewe makadiani katika vitabu vyao na magazeti yao wanasema hawafanani katika ibada na Waislamu wengine. Sasa watu waongo hakuna haja ya kupoteza muda kujadiliana nao.

Kingine kwa upande wako ndiyo maana nakuita MJINGA, na huujui Uislamu aichokiandika ukashindwa kukihoji na kujua dosari yake.

Makadiani siyo Waislamu kwanza kulingana na maana ya Uislamu. Hao alio waongelea tayari walikuwa wameshamkubali mtume, kwa maana ya kukubali alichokuja nacho, lakini Makadiani wanapingana na Qur'aan na mafundisho ya Mtume, vipi uwe Muislamu na huku unapingana na mafundisho ya Uislamu ?
 
Mokaze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…