Kabla hatuja wafundisha "Wasiomini Mungu" juu ya uwepo wake, basi inafaa sisi "Tunaoamini Mungu" tumalize tofauti zetu

Kabla hatuja wafundisha "Wasiomini Mungu" juu ya uwepo wake, basi inafaa sisi "Tunaoamini Mungu" tumalize tofauti zetu

Utofauti wako haukuwa relevant kwasababu unaye mhusianisha na sisi hayupo kwenye atheism

Ila nyinyi mpo kwenye theism
Nimezungumzia kwa umoja watu wasioamini Mungu na huyo ni mmoja wapo lakini nimesema hata hao Atheists nao hutofautiana.
 
Nimezungumzia kwa umoja watu wasioamini Mungu na huyo ni mmoja wapo lakini nimesema hata hao Atheists nao hutofautiana.
Agnostic ni kundi tofauti hivyo huwezi ukawa weka kundi moja na atheist

Kama atheist yupi?
 
Mimi kuna ndugu yangu alitoka kujijini alikuja dar tukawa tunapiga stori akanidokezea kuhusu kushamiri kwa watu wa Ahmadiya kujijini hapo na wametengeneza himaya fulani na yeye muumini wa msikitini wao . Akaanza kunipa dondoo baadhi ya itikadi na ibada zao hao Ahmadiya anafuata ndugu Mokaze hapo nikabaki nashangaa kwa sababu taratibu nyingi ni ngeni na misingi tofauti na Uislamu unaofahamika kwa asilimia kubwa ulimwenguni mpk nikajisemea inakuaje mtu Muislamu kufuata itikadi kama hizo ?

Kama habari zile ningesikia mtaandaoni ningepinga kwa asilimia zote kwamba hakuna waislamu wa hivyo watu wanawasingizia nimeamini kwa vile ninethibitishiwa na watu wengi wa kiijini pale .


Mkuu, ingalikuwa vyema ukaainisha hizo itikadi unazosema za Waisilamu wa Ahmadiyya ambazo ni "tofauti " ili tuone je itikadi hizo hazifuati Qur'an na hadithi na Sunna za mtukufu mtume (saw)--- kwani msingi wa Mafundisho ya Uisilamu ni Qur'an na Sunna/Hadithi sahihi,

Tafadhali tuwekee hapa.
 
Scenario
Naomba ni declare interest "Mimi ni mkristo Tena Mlutheri".
Hivi lipokuja swala la kuwaaminisha hawa wasio amini Mungu yupo "Kwanini sisi Tunaoamini Mungu yupo TUSIWE NA SAUTI MOJA?"

Flash back
Nimekuwa nikisoma nyuzi nyingi tu juu ya wasio amini Mungu yupo wakitoa madini yao.
Lakini pia nimekuwa nikisoma juu ya wanaoamini Mungu yupo wakitoa madini yao pia.

The Problem
Ila mi binafsi nahisi Kuna tatizo kwa "Sisi Waamini Mungu"
We fungua Uzi wowote kwa wasioamini Mungu, utaona kila mwamini Mungu yupo anatoa ushahidi wake ambao ni tofauti na ushahidi wa mwengine.

Hebu soma ushahidi wa wakristo juu ya Mungu yupo?
Then soma ushahidi wa Waislamu juu ya Mungu yupo?

Utaona japo wote wanaoamini Mungu yupo ila kila side ina views zake na comments zake ambazo sometimes zinatofautiana kabisa yaani ZINAPINGANA.

We Waambie watoe view juu ya Mungu yupo kupitia Maandiko yaliyomtaja Yesu na Mtume Mohammed S.A.W utaona wako tofauti na kama hata wao ""Wanakinzana na kugombana kimawazo""

Sasa najiulizaga "Ikiwa kama sisi Tunaoamini Mungu yupo" tunazinguana..!! Tutawezaje kumuaminisha huyu ambae haamini Mungu yupo Akaamini?

The Paradox
Nina rafiki zangu wawili John (Mlokole - namwitaga baba Mchungaji) na Khadija (Sunni - huyu namwitaga ustadhati mzuri..!!!)

Hawa watu wawili kama wewe ukitaka kupata ""Confusion kichwani mwako"" we waulize swali kama ""ikiwa Imani ndio msingi mkuu wa kufata mafundisho ya Mungu ili twende peponi basi Motoni anaenda wa Imani gani?""

Atakachokujibu baba Mchungaji ni tofauti kabisaa na ustadhati wangu mzuri..!!!

What is Behind?
Sasa huwa najiuliza
1. Mungu hajui huu mkanganyiko alionao Khadija na John juu yake?

2. Huyu Mungu atawachoma wakina Khadija au wakina John kwasababu kati yao mmoja anatumia njia isiyofaa kumfata yeye (Haya ndio mawazo ya John na Khadija, huyu shika Biblia huyu shika Quran)...??

3. Huwa najiulizaga ""Kwanini Mungu asitoe tu one statement ili kutoa one truth true..!!""
Maana ukitaka kujua juu ya Habari za Mungu na Pepo, na Jehanamu basi John atakufundisha hivi na Khadija vile...!!!! Yaani tofauti Tena kwa kupingana kabisaaa.

Kwanini Mungu asiseme yeye mwenyewe "Kundi hili ndio lipo sahihi na nyie wotee nifateni kwa staili ya kundi hili"

Conclusion
Kama sisi " Waamini Mungu yupo" tumeshindwa kuelewana na wenyewe kuwa Mungu ni wa upande gani, Je kuwaaminisha ""Wasioamini Mungu yupo"" ya kwamba ""Mungu anataka Mafundisho ya kina John au Khadija"" Tutaweza kweli??

Mi nafikiria sisi Tunaoamini Mungu tukae kikao..!!! tuelewane kwanza then ndio tuwafate wasio amini Mungu ndio ""TUWAPE HABARI ZA MUNGU""


#YNWA
Mkuu hilo haliwezekani. Kulikuwa na migongano miongoni mwa mitume waliokuwa na Yesu, sembuse sisi. Mungu katupa free will ya kila mtu kufanya aonalo sawa machoni pake. Hakutufanya robot tuwe na mawazo sawa.
 
Mkuu hilo haliwezekani. Kulikuwa na migongano miongoni mwa mitume waliokuwa na Yesu, sembuse sisi. Mungu katupa free will ya kila mtu kufanya aonalo sawa machoni pake. Hakutufanya robot tuwe na mawazo sawa.
Ila pia "Kuna upande uko sawa na mwengine unakosea?"

#YNWA
 
Atheism na Angotism ni vitu viwili tofauti

Ila muislam kwa muislam wote mko kwenye group moja la theism
Atheist yupo kwenye group gani na agnostic yupo kwenye group gani?
 
Mi nafikiria tu Kwa sauti...

Hivi Kwa mfano Waarabu na Wamishenari wasingekuja Africa kututawala na kutuletea hizi dini, labda ingekuwa sie ndo tumepata maendeleo mapema tukawa tumeenda huko, Uislamu na Ukristo ungekuwepo Africa? Na sie si tungekuwa tumeweza kuwashawishi waache dini zao wafuate hizi za kwetu na wakakubali?
 
Mi nafikiria tu Kwa sauti...

Hivi Kwa mfano Waarabu na Wamishenari wasingekuja Africa kututawala na kutuletea hizi dini, labda ingekuwa sie ndo tumepata maendeleo mapema tukawa tumeenda huko, Uislamu na Ukristo ungekuwepo Africa? Na sie si tungekuwa tumeweza kuwashawishi waache dini zao wafuate hizi za kwetu na wakakubali?
Dini zetu zipi hizi mila na tamaduni za makabila yetu?
 
Back
Top Bottom