Kabla haujakopa milioni nne kwaajili ya Ada ya mwanao, tuliosoma Cuba tuna ujumbe wako hapa

Kabla haujakopa milioni nne kwaajili ya Ada ya mwanao, tuliosoma Cuba tuna ujumbe wako hapa

Watoto wayajue magumu pia.Sio soft soft sisi kusini apata na.elimu kwa vitendo marenda mirenda haipo.Tokea anasoma anakaa kwenye mraba na shule.Hapo akishinfwa kuajirika snajiajiri katika lilimo anaoa au kuolea poa ka isa
Kama kuandika kwenyewe ni shida hivi acha wanangu niwasomeshe ata kwa mkopo
 
Nyie mnaoponda elimu sijui mkiwa mnaandika Huwa mnazingatia vitu gani, Nani aliyekuambia ukisoma lazima UWE tajiri. Lengo la elimu siyo kutajirisha watu Bali inawezesha kupambana na mazingira Yetu.

Binafsi MTU yeyote nayeponda elimu namwoma kamatahira , MTU aliyechanganyikiwa na kukata tamaa. Dunia ya leo unaanzaje kuponda elimu Bora, exposure utapataje..

Kama fikra zako ni kuishi na kuinterract na watu wa tandale na mpanda Sawa, lakini Dunia ya leo ni kijiji huwezi ku undermine elimu Bora Hata kidogo

Angalia wakenya wanatupiga gape kubwa sana Kwa sababu elimu Yao ni Bora kuliko Sisi. Ivi mnaosema mtoto wako ajue na kuandika tu.

1. Madaktari watapatika wapi.
2. Engineers watapatikana wapi.
3. Wachumi na wanasheria watapatikana wapi.
4. IT guys tutawapata wapi.

Etc etc.

Kutokujali elimu ni kukubali utumwa. Tumetawaliwa Kwa sababu tu wajinga. Ulitakiwa ulete suluhisho nini kifanyike ili elimu yetu iwasaidie vijana lakini siyo kusema wajue kusoma na kuandika tu .

Kama MTU Hana uwezo wakusomesha shule nzuri atumie MDA WA ziada kuhakikisha watoto wake wanakuwa na uelewa mzuri WA mambo la sivyo tutaendelea kudanganyana eti watoto Bora wawe wafanya biashara.

Huwezi kuwa na matajiri wajinga wajinga wachuuzi afu nchi ikasonga mbele. Lazima uwe na matajiri wenye akili pevu wanaoweza kuwekeza Katika viwanda na technology

Najiuliza mara mbili mbili u great thinkers baadhi ya watu hapa ndani elimu Bora ni muhimu kuliko kitu chochote hapa Duniani acha kudanganya watu..

Shule Za kayumba za Sasa si sawa na Za miaka ya 80 utatesa watoto bure

THINK TWICE BRO
Jf ni kama kijiweni tu kanuni moja wapo ya kijiweni ni kwamba unayoyasikia pale huyachukui yote unachukua ya muhimu mengine unayaacha palepale.
Unaweza ukakuta anayeandika hapa mwanawe yupo the heaven of peace pale mbuyuni kunduchi anasoma na wazungu.
Though sometimes inatokana na kukatishwa tamaa kwa watu waliosoma wakilinganisha na mafanikio walio nayo vs wasiosoma na mafanikio waliyo nayo kama msukuma
 
Ww mbona umesoma? Acha upotoshaji kama wewe umesoma na kuishi bila kaz bac aiko ivyo kila mtu na bahat yake
Hamna Cha bahati ilikuwa zamani ukimsomesha inabidi uanze andaa connection za kazi na hapo lazima utumie pesa na unaweza ukatumia pesa na ukafeli

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nikipata pesa watoto wangu watasoma shule nzuri za bei mbaya...wale maisha..Mimi kama mzazi nitakua nimetekeleza wajibu wangu.
Mambo ya kazi ni mambo ya riziki na riziki Kila mtu ana yake
 
Nikipata pesa watoto wangu watasoma shule nzuri za bei mbaya...wale maisha..Mimi kama mzazi nitakua nimetekeleza wajibu wangu.
Mambo ya kazi ni mambo ya riziki na riziki Kila mtu ana yake

Ndio mpaka upate SASA hizo Pesa.
Pesa sio ndoto za alinacha
 
Watoto wayajue magumu pia.Sio soft soft sisi kusini apata na.elimu kwa vitendo marenda mirenda haipo.Tokea anasoma anakaa kwenye mraba na shule.Hapo akishinfwa kuajirika snajiajiri katika lilimo anaoa au kuolea poa ka isa

Noma Sana
 
Utakuja kusikia nimekusomesha kwa tabu sna😂😂

Wanakuwa wakwanza kupiga Mayowe.
Wakati unasomesha Kwa shida na kuuza viwanja, na magharama makuubwa, mpaka anamaliza kidato cha sita mtoto kamaliza milioni 20.
Kuna wenzako wametumia Chini ya milioni moja From kindergarten to Form six.
 
Elimu imekosa maana kabisa siku hizi ila sio kutokusomesha watoto shule nzuri eti kwa sababu hamna ajira, kimsingi elimu inamkomboa mtoto aje kujiendeshea maisha yake mwenyewe akiwa na akili sawasawa, wasipopata elimu ya kutosha wataishia kwenda kutafuta miujiza feki kule wanakokanyagishwa wese na kupeleka nywele ili wapate utajiri na hela , elimu ndio mpango mzima hasa elimu za kuwasanua kwamba hakuna ajira wanatakiwa kuwa wajasiriamali. Kuna mjadala nilitaka kuingia mkenge eti musukuma na kishimba hawajasoma ila wanamihela jaribu kufuatilia kwa makini uone kama hizo hela ni za mbanga za halali kweli unaweza kukimbia, bora hela ndogo ya halali kuliko hela nyingi ya magumashi.
 
Somesha shule ya hadhi yako. Hiyo ndio Hoja.
 
Somesha shule ya hadhi yako. Hiyo ndio Hoja.
kayumba usijaribu kaka wala usimshauri mtu ambaye ana kauwezo kake apeleke mtoto kule ,kwanza hao walimu wenyewe tiamaji tiamaji, nimeshuhudia mwalimu hata ku construct sentensi moja ya kiswahili iliyonyooka hawezi KISWAHILI wala sio kizungu, unategemea huyo atamfundisha mwanao?
 
Kwema Wakuu!

Leo sina mbambamba, short and clear sitaki kuchosha nguvu kazi ya taifa nisijeitwa mhujumu uchumi.

Siku hizi wala usijitese kusomesha Watoto wako. Somesha Kwa ku-relax kulingana na uwezo wako. Sio uingie madeni kisa kusomesha. Huo ni ushamba na matumizi Mabaya ya Pesa na Akili.

Sisi wengine tumeshasoma,😀😀 tunajua MTU mwenye Elimu anakuwaje, anafursa gani na anachangamoto zipi. Sisi ndio unatakiwa utusikilize, hutaki Acha.

Usidanganywe na matangazo ya shule 😂😂 ooh! Atapata divisheni one blah blah blah! Mlete mwanao, wekeza kwenye Elimu na blahblahblah zingine. Hivyo jinyime ili msomeshe mwanao, Ada milioni mbili Wakati uwezo wako ni laki tatu.
Ada milioni Tano Wakati uwezo wako milioni Moja. Alafu Kwa vile nawe ni hamnazo unajitutumua kama tukutuku!

Anayeandika hapa anahizo divisheni one, nimeshakaa na watu wenye hizo divisheni one. Hakuna maajabu yoyote ya divisheni one nje ya mfumo wa elimu.

Wakati unampeleka mtoto wako Kwa kujipinda haswa mpaka unashindwa kul vizuri elewa mambo haya;

1. Kusomesha Kwa kujipinda ilikuwa biashara inayolipa zamani na sio sasa.
Zamani mtoto uliyemsomesha akimaliza anapata kazi, Pesa zote zinarudi, lakini usithubutu kujimaliza kisa Elimu sasa hivi utalia kama mbuzi mee! Huku ukiuza karanga.
Kusomesha sasa hivihakulipi. Usijiumize.
Kama huna pesa peleka mtoto shule za serikali. Mbona Sisi tumesoma hizo shule na tumefaulu Kwa Daraja la Kwanza tuu.
Usijitesewal kujipa stress kama mpumbavu.

2. Elimu inayotolewa haiendani na Pesa utakayoitoa.
Unajikakamua wee kupeleka Watoto shule kubwa ukitegemea utaona mabadiliko ya kitabia na Kiakili Kwa Watoto. Lakini mitoto inarudi haina inachojua, imezoea kukariri tuu. Ukiipa maswali ya kutafakari haina uwezo wa kuchambua mambo.
Mbaya zaidi inashindwana wale wanaosomea shule za Bure.

Elewa kuwa Akili ya mtoto ndio kitu kikubwa kuliko kile anachokifuata shuleni.

3. Mtoto hataajiriwa kisa kapata division one au two. Bali ataajiriwa ikiwa anacheti hata kama nichakuunga unga factors zingine zikizingatiwa.
Hiyo milioni tano unayomlipia Kwa kujipinda nibora uitumie kujichanga na kutafuta connection ili mtoto akimaliza apate kazi, au utumie hizo Pesa kumuwekea Akiba akimaliza shule umpe mtaji afanye biashara.

Sasa unatumia mapesa meeengi alafu akimaliza shule unamtelekeza,😂😂 endelea kutoa Pesa mpaka apate kazi.au lengo lako lilikuwa asome tuu iliiwe nini? Lengo ni ili apate taaluma Fulani kisha afanye kazi.

Sasa mzazi unatoa mahela meengi kusomesha ili baadaye umlaumu mtoto hapati kazi. Kama lengo lilikuwa nikazi mpe kazi.

4. Waliosoma siku hizi kuburuzwa na wasiosoma ni kitu cha kàwaida.
Unasomesha mtoto Kwa gharama kubwa ukijtesa ili baadaye aje aajiriwe na mhindi ambaye hajasoma kabisa, au ili aongozwe na mbunge au diwani ambaye kaishia darasa la Saba.

Hayo mapesa uliyopoteza Kwa kujibana na kujitesa(zingatia Sana Hii kauli) ni Bora ungenunua zako nguo ukavaa au Kula bata.

Wewe unasomesha mtoto ambaye anafikiri akiongea kingereza ndio ataonekana Msomi bado uone hapo uliweka Pesa. Hapo umepoteza na kujitesa Bure tuu!

5. Unasomesha Kwa kujitesa ili mitoto yako baadaye ije Ione Mila na desturi zenu ni Mavimavi.
Hapo watachanganya ni kingereza utadhani wanaakili kumbe ni matope.

Kumbe nilisema sina mengi. Mniwie Radhi.
Zingatia, kama unauwezo wa kusomesha shule za gharama someshe kulingana na kipato chako. Lakini kamwe usithubutu kujitesa kisa hizi Elimu za kikoloni.
Sisi ndio tumesoma tunakuambia,
Sisi ndio tulipata ufaulu wa Daraja la juu ambao unataka mtoto wako aupate ndio tunakuambia. Sasa kuwa mbishi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Nilishawahi kusema hapa, uwekezaji wa elimu kwa sasa haulipi. Unasoma na kwenda kufanya kazi za wasiosoma.
Shule standard zipo ada
 
Nilishawahi kusema hapa, uwekezaji wa elimu kwa sasa haulipi. Unasoma na kwenda kufanya kazi za wasiosoma.

Sasa ndio nini hiyo Mkuu.
Hizo Pesa zilizotumika kusomesha Kwa gharama ungempeleka shule za kawaida alafu akimaliza unampa mtaji mtoto akafanye biashara
 
kayumba usijaribu kaka wala usimshauri mtu ambaye ana kauwezo kake apeleke mtoto kule ,kwanza hao walimu wenyewe tiamaji tiamaji, nimeshuhudia mwalimu hata ku construct sentensi moja ya kiswahili iliyonyooka hawezi KISWAHILI wala sio kizungu, unategemea huyo atamfundisha mwanao?

😂😂😂
Unamfundisha Mwenyewe mtoto nyumbani.

Sisi wengine tulijua kusoma, kuandika, kuhesabu na kidogo kingereza nyumbani. Kila tukirudi jioni tunapigwa msasa
 
Back
Top Bottom