Kabla haujakopa milioni nne kwaajili ya Ada ya mwanao, tuliosoma Cuba tuna ujumbe wako hapa


Nitafutie aliyesoma international school alafu nikutafutie aliyesoma Kayumba alafu tuwalete sehemu moja uone kuwa kusoma shule kubwa haimaanishi uta- achieve Sana tofauti na waliosoma Kayumba.

Kinachowagharimu wakayumba ni mazingira kuanzia ya nyumba mpaka shuleni.
Sisi wengine tumesoma Kayumba lakini tupo vizuri
 
Mm najipanga mwanangu degree ya kwanza akasome ulaya huko
Atengeneze maisha huko huko after graduation

Huko Ulaya labda ni ili akimaliza atokomee hukohuko afanye kazi na kutafuta Pesa HUKOHUKO.
Lakini wapo wamesoma Ulaya kuanzia SEKONDARI mpaka chuo na tupo NAO hapa mjini na Hawana maajabu
 
Umeongea ukweli apa home kuna dogo anazingua sana anataka vitu vikubwa wakati uwezo wa atuna pia ata yeye kichwani hovyo kaka ake apa 3 yrs sina mishe za kueleweka na vyeti vipo ndani ananiona nimefeli maisha .Anataka akasome Redioology sijui

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Achana naye. Akikua atakuelewa
 
Ujuaji ujuaji ujuaji!!

Sio Kila muda utoe andiko

Nenda PWC na divishen 3 na mwenzio Ana one uone kaama utapata kazi...Kwanza hata hiyo PWC hujui nini.

Wewe unajua maana ya DCL?
Haya ndio Matokeo ya MTU unapeleka shule Kwa gharama kubwa alafu kuandika abbreviations ya maneno ndio anaona ni Jambo kuubwaπŸ˜‚πŸ˜‚


Wabongo oneni madhara ya kupeleka mitoto shule ili ikakariri
 
Ujuaji ujuaji ujuaji!!

Sio Kila muda utoe andiko

Nenda PWC na divishen 3 na mwenzio Ana one uone kaama utapata kazi...Kwanza hata hiyo PWC hujui nini.

Mdogo wangu anafanya kazi PWC ameajiriwa mwaka jana.

Alikuwa best student udsm mwaka 2021.

Mdogo wangu amesoma shule za serikali kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu.

Anaitwa Irene msengi.

Amesoma kayumba ila bado udsm kaburuza chuo kizima.
 
Kuna mtu Fulani

Kasomesha watoto wake kuanzia vidudu hadi form $ix private tena zile za gharama.

Chuo kawalipia ada na kuwapa Hela ya matumizi madogo hawakuomba bodi ya mkopo.

Baada kumaliza Chuo madogo wanatembea na bahasha kuomba kazi[emoji1]WTF

Sijawahi ielewa hii logic yaani wanasaga soli kama waliosoma st kayumba.

Dingi yupo Wala hastuki sio kwamba Hana uwezo kuwapusb wafanye biashara.

Ni vile mbinafsi tu. Au ni wale wazee wenye mentality za kizamani waaoamini kazi tu.

Na mbaya zaidi watoto wenyewe nao wanachagua aina za kazi.

Kuvunja vicious cycle ya umasikini ni kazi ngumu.
 
Mdogo wangu anafanya kazi PWC ameajiriwa mwaka jana.

Alikuwa best student udsm mwaka 2021.

Mdogo wangu amesoma shule za serikali kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu.

Anaitwa Irene msengi.

Amesoma kayumba ila bado udsm kaburuza chuo kizima
sasa huyo jamaa yako anasema kwenye ajira sio lazima kupata divisheni one.

Hata Mimi nimesoma kayumba na nilifaulu vizuri vi-Necta vya ndalichako

Pia mdogo wako kusoma kayumba na kufaulu Haina maana kwmba watu wasisomeshe watoto shule zinazotoa elimu bora
 
Wewe unajua maana ya DCL?
Haya ndio Matokeo ya MTU unapeleka shule Kwa gharama kubwa alafu kuandika abbreviations ya maneno ndio anaona ni Jambo kuubwa[emoji23][emoji23]


Wabongo oneni madhara ya kupeleka mitoto shule ili ikakariri
Huna akili.
 
Kama unataka mwanao awe na akili kubwa awe anaangalia movi za kisayans hahaha, elimu elimu, elimu,
 

Mleta uzi alichomaanisha somesha mtoto kwenye shule ambazo una afford. Sio uingie madeni ya mamilioni kisa mtoto asome shule nzuri wakati shule za bei nafuu zipo za serikali.

Kama wewe una ni tajiri somesha shule za gharama ila kama unaunga unga maisha peleka goverment. Sio ujipe madeni kisa elimu
 
Kusomesha watoto shule nzuri ni jambo la muhimu sana.Sikupingi mleta maada ni vile tu wewe umeiangalia elimu itakua na return zipi kwa mwanao financially AND YOU ARE VERY CORRECT kwa ulimwengu sasa.
Kama uwezo unao peleka mtoto shule nzuri. Kama uwezo wa kawaida peleka mtoto shule za kawaida.

mbali na atakuja kupata nini hapo baadae, kuna factors nyingi zinafanya watoto tuwapeleke shule za kulipia

Mfano.
Mimi ni mtu wa bara nyanda za juu kusin magharib huko lakin maisha harakati niko mkoa wa pwani.Tamaduni nilizokua lelewa nazo na ambazo nataman kuwaona wanangu pia wanakua nazo ni tofaut sana na mfumo wa maisha ya hapa nilipo sasa. Mifumo na taratibu za kimalezi kwa wenyeji / wazawa wa ukanda huu ni tofaut sana.Na mimi siupendelei hata kidogo japo siwalaumu maana kila eneo na mila na desturi zake..
Kwahiyo watoto mitaani mpaka shuleni wanakuzwa katika taratib zao hizo na
Kwangu hii ndio sababu kubwa ya kutopeleka mtoto shule za serikali kwenye changanyikeni.
Watoto wengi darada moja kias kwamba ni ngumu kuwa monitor.

Kwangu Moral values ndio kinanifanya bora nijinyime nikawalipie tuu .
 
Mbona umeandika kwa jazba sana mkuu, kulikoni?
 
Point ya msingi niliyoipata hapa ni moja tu, " somesha kulingana na uwezo wako".
 
Mkuu si umeona effect ya elimu yetu ya kukariri, jamaa hata contents za mtoa mada hajaelewa ,Kisha anaenda kufanya direct confrontation na mtoa mada ,mkuu Kwa harakaharaka unapata Nini na msingi wa elimu yetu?,je mtu huyu anaweza kujireason kwenye changamoto ngumu?,hii ni cancer Kwa taifa
 

Hapo sio ajabu zaidi ya milioni 10 zimetumika kumsomesha. Ndio utajua kusoma sio kuwa na Akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…