Kabla hujanunua Azam TV pitia hapa; Usije kujuta

mkuu Fanya utafiti wa kina kabla ya kununua usije nunua Azam kwa mategemeo makubwa ukaambulia patupu! Jaribu kuangalia Zuku maana wana afadhali! ila jiridhishe kwanza

kabla ya kununua zuku akae akijua kua mwisho wa mwezi ukifika wanakomba channel zote hakuna cha locals wala loko
 
Mvua ikinyesha kidogo chanel zote zinakata hazionyeshi
 
Hivi haiwezekani kuangalia TV yoyote duniani through internet?. Natamani sana hii kitu, sema internet yenyewe TZ bado sio stable.
 
Kwa kuiondoa ETV Africa kunanifanya nirudi kwenye Startimes ambako nitawaona kina Roman Reign na Dean Ambrose na WWE yao,

Kwa heri Azam TV
 
Mimi nina mawazo tofauti kidogo, sijaona king'amuzi ambacho kinakurudishia thamani ya pesa yako kama cha azam, kwanza kiko unlocked na uwezo wa kufungua FTA channels japo si zile zenye BISS kEYS etc, na kama ukichoka huduma za azam unabadilisha tu uelekeo wa dish na kunasa zingine, kina kidhi thamani ya pesa zako
 
Azam TV wanaboa sana,hata presenters wao wanaboa sana, sidhani kama wote ni professionals
 
Mi nimefunga geto na nalipia Azam Sport Hd ili niwe namuona Mess tu maana ndie anayenifanya niangalie kila game anayocheza Barca ila lasi yeye HD wasingeniona…

Mipira imenifanya nitumoe Azam tv nikiangalia LIGA BBVA na VPL kwa Yanga yangu basi nabirudika sana lakini hawako fair kwenye bei kwa maana ile elfu 15 ya Azam Sport HD haina maana kutuwekea chanel ya Azam sport Hd na zile za Manchester Unt, Liverpool na Real Madrid tu pale ilitakiwa Ukilipia kile chanel zote za.michezo zifunguliwe kama Kombat Sport, Fox zote na etc yaani kulipia 15 elfu kwa Azam Sport Hd sawa umenunua Chanel moja tu maana zile nyingie na Man u, Liverpool na Madrid hazina maana huwa hazionyeshi ata mipira live
 
sasa mbona mnatuchanganya. anyway ni angalizo zuri
 

kweli mkuu zile channel za Man U ,Liverpool na Madrid hazina maana! ni kutangaza timu zao tuu!!!!hakuna mech ya live labda za watoto
 
Kwa kuiondoa ETV Africa kunanifanya nirudi kwenye Startimes ambako nitawaona kina Roman Reign na Dean Ambrose na WWE yao,

Kwa heri Azam TV

tupo pamoja
 
Kuhusu wauzaji, Tanzania tuna shida sana eneo la custommer care
 
kwa hela unayolipa unastahili kupata chaneli hizo, elfu 15! unataka kuona epl, la liga, vpl da wewe umezidi bana! kwa hela hiyo labda ufunge cable. Watu hawana shukurani badala ya kuwashukuru azam mnawashutumu, njooni huku dstv kwenye ubora mnaoutaka.
 
dstv mambo yote hapa utapoteza muda tu kujua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…