Kabla hujaoa Usukumani, zingatia haya ili ndoa yako idumu

Mbona umefungua saana code,umejiweka wazi na umemuweka wazi mke wa Askari kujulikana

Jirani yako
Askari polisi
Mkewe unaetembea nae ni msukuma

Alishatembelewa na familia nzima
Askari akiiona hii,ameshapata mchoro
Hakuna ukweli wowote hapo hiyo ni kamba hakuna baba mkwe wa kisukuma akaenda kwa mkwilima kukaa zaidi ya mwezi. ndoa yangu ina miaka zaidi ya kumi lkn baba mkwe kaja mara moja na hakumaliza wiki. akija anasalimia anaondoka. mama mkwe huwa anakuja kila mtoto wake akiwa mimba hapo anaweza akakaa hata mwezi au
zaidi kama atakawia kujifungua na nilazima nimuombe mimi aje.
 
Mchele utoke wapi bro, ya kwao ni michembe tu.

Hilo la chale ni kiboko, mara ya kwanza nilishangaa sana ila uchawi ni utamaduni wao na hawaoni haibu

Mchele umekuwa ukilinwa sana Shinyanga kwa miaka mingi, tena mchele wao ni organic hawaweki mbolea za viwandani zenye kemikali , ukienda kununua masoko yenye hadhi kama Kisutu utakuta unaongoza kwa bei juu sababu ya ubora wake.
Mchele wa kurka ni jina tu lakini kwa utamu , kunukia na ubitą mchele wa Shinyanga ni nam Bari wani hauna mpinzani .
Kilo shilingi zaidi ya 4,500/- tena ni muda Sijui kwa Sasa .
Sema wasukuma wanalima kwa biashara na sio kwa matumizi ya chakula ,
Wao chakula chao kikuu ni ugali wa mahindi na viazi vitamu.
 
wanyamwezi na wasukuma tamaduni ni ile ile ni sawa na kusema wadakama na bhakiya sijui utaelewa.
kwanza michembe sio chakula kikuu huku hii pigaX
Mwaka jana mzee wangu pamoja na uzee wake katoa gunia 427. lakin usiku hawezi kula wali.

Uliza wazee watakwambia kuwa mpunga ulikuwa unaitwa chakula cha ndge kipindi hicho.
huku mpunga unalimwa sio kidogo vilevile kwa sababu unadhurula ukimaliza kuzurula muone bashe akupe takwimu
lazima kwenye kanda muhimu3 za wazalishaji wa mpunga kanda ya ziwa lazima imo.

mkuu kwa sasa zao la mpunga ndo linamatokeo chanya pamoja na mzee kutoa zaidi ya gunia 400 lakni mahidi kapata gunia hazizidi 20 imagine kwahiyo kauza mpunga na akanunua mahindi

Mi hata kesho wali siupendi huwa nakula kwenye sherehe tu.
 
Uko sawa mkuu. mpunga huku kwa sasa unalimwa sana nikweli hatuwezi ifikia mbeya, mbeya hata kwa mahindi tu inatuzidi mbali mno
 
Wanyamwezi wanapenda kurina asali na ni wavivu wa kulima.
Hupenda kutumia Warundi kwenye kilimo Cha Tumbaku.
Walozi hasa kwenye mapenzi

Wanyamwezi sio wafugaji ila Wasukuma ni wafugaji.
Walozi hata kwenye mamabo yasiyo ya msingi.
Yaani mpaka mna sikukuu ya kushindanisha wachawi.
BARIADI hufanyika kila mwezi wa Tano.
Tena Kuna mkuu wa wachawi na waganga kimkoa.

Hizi ni tamaduni zinazofanana?

Ninyi yenu ni michembe na udaga tusijilishe upepo
 
Hawa wakikaa wiki nafukuza mana watakua washanitua hasara ya gunia la Mchele...
Hahahaaaa mkuu ujio wao kwako ni baraka tupu

lazima waje gunia lililo kobolewa la mpunga
karanga
maharage na viazi vilivyo kaushwa almaalufu michembe. huwa wanabeba kama wanahama mkuu. hata wasipokuja
utatumiwa tu hata uwe dar au mbeya

wakija mikono mitupu fukuza sio wasukuma wale.
 
Hahaaaa mkuu unafurahisha sana. yaani hivyo vyote ulivyotaja wanyamwezi wanafanya nasisi vipo baadhi ya sehemu.
Sisi ndo wahusika unatubishia? Babu yangu mmoja wa wake zake alikuwa mnyamwezi nisijue kutofautisha? hadi leo baba wadogo wako hapo Tabaora huwa tunaenda na wao huwa wanakuja.

Kila kabila lina chakula chake pendwa mfano wazaramo na ubwabwa nani wa kuwatenganisha nao? je wanalima wapi wazaramo huo mpunga?

Sisi ni ugali mhogo huwa tunachanganya kwenye ugali wa mahindi ili uwe laini. udaga kavukavu huliwa mwambao wa ziwa hasa wavuvi na wengi wao sio wasukuma kuna wasubi,walongo,wasumva nk hawa ndo wanapenda udaga.


Sioni shida kabisa sisi kula ugali na viazi ni cahakula pendwa sana na kamwe huwezi kutubadirisha labda vizazi vya tiktok
 
Mchembe karanga na yoghurt ndiyo chakula pendwa kwao. Ila ni kabila linalo jali sana kwenye chakula hawana uchoyo kabisa kwenye msosi.
😂😂😂

Hivyo ni highly recommend in health isipokuwa ugali tu 👌👌
 
Hahahahahaha....!
 
Hivi mkuu kati ya wasukuma wa mwanza na shinyanga ni wapi kwenye wanawake wa kisukuma wenye tabia njema?
Kwa niaba tu.

shinyanga ni kubwa na sasa imegawanyika kuna simiyu pia yote hiyo ni shinyanga mwanza vile vile sasa kuna geita.

swali lako ni sawa na kubeti lakn kwa haraka haraka nenda vijijin huko shy utapata na uende kama msukuma ukienda kama bishoo utapewa bishoo mwenzio
 
HA!HA!HA

Kama wanafungasha hivyo inakua unyama sana ...!!
 
Shukrani mkuu ila mimi sio msukuma ila napenda nioe mwanamke wa kisukuma
 
Wasukuma ni kabila Mojawapo ambalo limebarikiwa sana.
Wasukuma ni ma-giants, ni majitu, yamepanda hewani kama Majerumani, kama wadachi, kama wacanada n.k
wengi wamenyooka mkikubaliana jambo ni hivyo hivyo Hawana kigeugeu.
Si Watu wa hila moyoni.
Si Watu wa ndimi mbili.
Si wanafiki.
Ukifanya nae kazi ofisini ujue uko salama hawezi kukufanyia ubaya wala fitina.

Nawapenda sana watani zangu lakini okokeni acheni uchawi na ushirikina.
Mwamini Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi.
Tubuni maana ufalme wa Mungu umekaribia.
Mwaminini na Robo Mtakatifu.
 
Sema kuna changamoto naziona kwa jamii ya wasukuma.
Ile identity yao ya u-giant huenda ikapotea na kubaki historia baada ya muda mfupi ujao.
Sababu siku hizi wanaoa wanazaa na makabila baki ambayo hayana vile vinasaba vya urefu ndani yake.
Unakuta mtu anakwambia ni Msukuma lakini mfupi kama Mpare wa thame au Mluguru wa mgeta/matombo ?!
Yaani zamani na wanawake wenu MashaAllah nao ni warefu mkija kutoa watoto ni majitu fulani yamenyoookaaa.

Breed ya aina yake kwa kweli.
 
Siku hizi kuna wasukuma wafupi hasa kuanzia kahama mpaka runzewe sababu wameoleana sana na waha
 
Nani aliyekwambia Wazaramo wanapenda wali?
Wandengereko na Wanyangalio ndio vipenzi vya wali.

Ninyi ni wazee wa udaga na michembe
 
Uko sahihi,kuanzia kahama mpaka runzewe kuna waha wengi sana na wameoana na wasukumu,waha wengi ni wafupi kwa hiyo kuna hybreed fulani haileweki kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…