Tunajadiliwa sana kwa mabaya sisi wasukuma! Nadhani hatuna jema kwa ninyi makabila mengi hapa Tanzania.
Chuki mliyonayo dhidi yetu ni kubwa mno kiasi Cha kuanzisha mijadala hasi dhidi ya jamii yetu.
Hoja ya haya yote ni Mila na desturi! Tuko tofauti na hatufanani.
*Nimeishi maeneo mengi katika ujana wangu huu na nimekuwa na marafiki wengi wa kusaidiana katika shida na Raha hasa walipojua kuwa Mimi ni msukuma. Of course Mimi ni mcheshi na tunaishi kwa kupendana sana.
- Wanawake wengi wanapenda hili kabila la "washamba" sijui kwanini ila mimi nime date na wanawake ( wadada) wengi wa makabila mengine kuliko hata wasukuma. Nipo humble na najiamini.
- Huwa naishia kuwahurumia baadhi ya watu wanaofuata mkumbo kutusema vibaya ilihali ni watu duni na fukara wa nguvu na kiuchumi.
- Hatujali hayo, tuna Ari ya kazi na ustahimilivu wa kimkakati. Kamwe tutabaki kuwa jamii inayojituma na kujiboresha kwa kutumia raslimali ardhi.
- Chuki za wapumbavu si kitu kwetu.
- Tuko wengi na ndiyo alama ya amani na uchapakazi, utu na ukarimu.
Mwisho: Hakuna kabila lilitimamu, tamaduni zinatupa kasumba ya kunyosheana vidole kwa kuwa hatuwezi kufanana. Furahia na wale mnaoendana, oana nao na uchangamane nao.
Chale za wasukuma zinatofauti Gani na alama za makabila kama datooga, wamakonde na wamasai?
Chuki huzaa mitazamo yenye ubaguzi na migogoro.