Kabla ya kuja watu weupe waafrika tuliamini uwepo wa Mungu ila hatukuamini uwepo wa shetani

Kabla ya kuja watu weupe waafrika tuliamini uwepo wa Mungu ila hatukuamini uwepo wa shetani

Kama unamuamini Mungu wa kweli, sasa kabuli la babu yako nila nini?? unaenda kutafuta nn??
mtu aliyekufa anaweza kukusaidia kitu..? wakati yupo huko na yeye anasubr hukumu yake.

NAONA UNAFANYA OPOTOSHAJI TU
Unapomuomba Yesu na Bikira Maria wakusamehe dhambi zako je unatofauti gani na hao wanaowaomba wapendwa wao??

Tenaa wewe unawaomba watu wasiokua na nasaba ya ukoo wako
 
Umepotea ndugu.

Historia uliochimba wewe nichamtoto..

Kuna jamaa kafundisha, video ipo YouTube

kaelezea tangu jinsi gani watu waliingia ardhi ya Tanzania..
Makabila kama wanyamwezi, wahehe, wapare, wahiraki yalianzishwa vipi na kwa maana zipi,.
imani hizo za mizimu zilianza vipi tulizitoa wap...

Shule ya maana.

na Hitimisho ni.. Sisi watu wa mataifa nje na Israel mwanzo wote hatukumjua Mungu wa kweli tulifanya ibada za Sanamu na kuabudu miungu pasipo kujua (Tunaita ni zama za ujinga)

lakini sasa tupo ambao tumeijua kweli, Tunamuabudu Mungu tunae mjua, Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo.
Vipi ambao walikufa bila kuijua iyo kweli Mungu anawajibika nao vipi mkuu? Atawaacha wale bata mbinguni kwa sababu hawakuwa na taarifa au atawatupa motoni maana hawakumfata?
 
Unapomuomba Yesu na Bikira la Maria wakusamehe dhambi zako je unatofauti gani na hao wanaowamba wapendwa wao??

Tenaa wewe unawaomba watu wasiokua na nasaba ya ukoo wako
Futa hiyo Maria kwanza ndio twende sawa.
 
Mungu (nguvu kuu) kila jamii ilikuwa na namna yake yakumfikia mungu (nguvu kuu) katika dunia nzima, kwetu afrika tulikuwa na njia zetu za kumfikia mungu na kutusaidia

Mizimu ni watu wema au mababu zetu waliokufa lakini katika uhai wao walikuwa watu wema walikuwa machifu,waaguzi,walinzi wa ukoo,watabiri n.k hawa watu roho zao hubaki katika ulimwengu kusaidia jamii zao husaidia kwakuwa wapo karibu sana na nguvu kuu( mungu) ndomana wakiombwa na kukumbukwa na jamii zao husaidia bila shaka lolote

Lakini pia kuna mizimu mibaya mababu zetu waliokuwa wachawi,wasaliti,walozi nao pia roho zao hua zinabaki duniani kuendeleza mambo yao waliowaachia mikoba huwaomba wawasaidie kazi zao za uchawi na ulozi na huwasaidia pia

Note: kila jamiii ina namna yake yakumfikia mungu (nguvu kuu) maamuzi ni yako kufata jamii yako ili umfikie mungu au kufata jamii nyingine wazungu,waarabu,wachina,waizraeli n.k ili umfkkie mungu(nguvu kuu)

_mzoma
 
Samahani mkuu.

Unamzungumzia huyu Mungu alieshindwa Kujua walipo Adam na Hawa baada ya kuasi hadi akaita ADAMUUU UPO WAPI???

unamzungumzia huyu Mungu mwenye wivu??

Unamzungumzia huyu Mungu ambae alimtaka Ibrahim amchinje mwanae Isaka Ili ajue kama ana imani thabiti kwake???

Unamzungumzia huyu Mungu alieua wazawa wa kwanza wa Wana wa Israel waliokataa kupaka damu Milangoni???

Kama ndo huyo huyo, basi Mungu wenu ni FARA
Amini nakwambia SIKU UTAKaYOKUFA HUKO UENDAKO UTAKUTANA NA WATU ULIO WAACHA DUNIANI, Utajua Mungu alioo uliza adam uko wapi ilikuwa na maana ipi.
PILI nikumbe mm halafu ukaabudu miungu mingine huyo utaratibu hata kwa mdudu mwenye hekima ndogo kama ya nyuki HAKUBALI.Christ mwenyewe alipimwa imani na ni pure God blood sasa Ibrahim ni Nani!?

Huo uzao wa kwanxa kasome vizur(Angel of Death,Among of the First order angels of God) ulivo mnafik huuliz kifo cha mtoto wa farau
 
Bikra maria bado yupo hai au sio???

Halafu anakuwaje bikra wakati alikwisha zaa???
Kuhusu Kuabudu bikira maria ilo mbona liko wazi ni Ni ufedhuli unao fanywa na makanisa ya kiroma wabudu sanamu.
pili aliitwa bikira keasababu alibeba mimba bira kumjua mwanaume
 
Mungu (nguvu kuu) kila jamii ilikuwa na namna yake yakumfikia mungu (nguvu kuu) katika dunia nzima, kwetu afrika tulikuwa na njia zetu za kumfikia mungu na kutusaidia

Mizimu ni watu wema au mababu zetu waliokufa lakini katika uhai wao walikuwa watu wema walikuwa machifu,waaguzi,walinzi wa ukoo,watabiri n.k hawa watu roho zao hubaki katika ulimwengu kusaidia jamii zao husaidia kwakuwa wapo karibu sana na nguvu kuu( mungu) ndomana wakiombwa na kukumbukwa na jamii zao husaidia bila shaka lolote

Lakini pia kuna mizimu mibaya mababu zetu waliokuwa wachawi,wasaliti,walozi nao pia roho zao hua zinabaki duniani kuendeleza mambo yao waliowaachia mikoba huwaomba wawasaidie kazi zao za uchawi na ulozi na huwasaidia pia

Note: kila jamiii ina namna yake yakumfikia mungu (nguvu kuu) maamuzi ni yako kufata jamii yako ili umfikie mungu au kufata jamii nyingine wazungu,waarabu,wachina,waizraeli n.k ili umfkkie mungu(nguvu kuu)

_mzoma
Yan umetulia kabisa una andika mizimu ni watu wema kwel??! Mizimu si watu tena ni nafsi za wafu uwe mwema uwe mbaya. Na haiwez kusaidia chochote
 
Waliwezaje kuwasaidia mababu zetu..? Wazungu wameshakuloga
Wazungu wameshimamisha SANAMU ya mbuzi, sasa huoni mm na hao ni tofati.
Nikwambie jambo rafiki, ambayo kwa sasa hata mitaani kwenu utayaona. Familia zote zenye asili uganga wa kienyeji au uchawi ndo hua zina sumbuliwa na pepo walio weka magano na marehemu kipindi akiwa hai na Mtu agano lake lilipo ndo mauti yake ilipo,na kizazi cha kwake hadi za nne ni mali ya mkuu wa pepo na muhusi juu,
Sasa kinacho tokea pepo wanachukua sura na sauti ya mareheru kukutaka ww ufanye au uendeleze alicho kuwa anafanya marehem sasa utasema Huu ni mzimu wa marehemu.?Hahafu zamani jamii nzima itafuata kila kitu chief atacho taka usidhani mababu wote walikuwa wanapenda kwa hiyo ukitaja mababu walikuwa hivi usijumuishe wote,Amini na kwambia tungepata story za miiko na sheria za kafara za kila kabila na chief na miungu yao nakwambi kwa free will ww unge kimbia, Kazome kwenye Miti mikubwa na mapango kuna nn waulize waganga na wachawi wanajua, kuwa makin
 
Vipi ambao walikufa bila kuijua iyo kweli Mungu anawajibika nao vipi mkuu? Atawaacha wale bata mbinguni kwa sababu hawakuwa na taarifa au atawatupa motoni maana hawakumfata?
Ni jukumu la kwanza na la juu kabisa la kila kiumbe mwenye akili kujifunza
kutoka katika Maandiko ukweli ni nini, na kisha kutembea katika nuru na
watie moyo wengine wafuate mfano wake. Tunapaswa kujifunza siku baada ya siku
Biblia kwa bidii, ikipima kila wazo na kulinganisha andiko pamoja na maandiko. Kwa msaada wa Mungu tunapaswa kuunda maoni yetu
sisi wenyewe kama ambavyo tunapaswa kujibu wenyewe mbele za Mungu. - E .G White ( The Great Controversy)

Kitafute hiki kitabu, kitakusaidia sana katika maswali mengi yanayohusu imani yako na Mungu.
 
Kuhusu Kuabudu bikira maria ilo mbona liko wazi ni Ni ufedhuli unao fanywa na makanisa ya kiroma wabudu sanamu.
pili aliitwa bikira keasababu alibeba mimba bira kumjua mwanaume
Na wewe unaamini alibeba mimba bila kuto*bw*??
 
Jana nilibahatika kufanya maongezi na mzee moja wa zamani sana age inakimbilia kama miaka 90 now.

nilimuuliza maswali mengi sana yanayohusu imani ila tukaenda mpaka miaka ya nyuma kidogo kutokana na maelezo yake niligundua aya.

kuwa waafrika kabla ya kuja waarabu, wareno , waingereza, waberigiji, wafaransa, wahindi na wachina. waliamini uwepo wa mungu ila swala lilikuja pale kumuabudia huyo mungu.

Nini maana halisi ya neno "Mzimu"?

Mzimu ni marehemu, ambapo Kiafrika kiasili tuliamini kuwa wafu wapo karibu na Mungu hivyo tulikuwa tunaomba mizimu utusaidie maana wao wapo karibu na Mungu. Ni sawa na Wakatoliki wanavyoamini katika saints.

lakini kwenye dunia ya leo tunaamini

"Maana ya neno "Mzimu", ni Mashetani ambao ndio humuongoza kufanya maasi, wakati mtu anakata roho hao Mashetani hutoka, hao ndio "Mizimu". Mizimu ni Mashetani walio toka kwa WAFU, kutii Mizimu ni kutii Mashetani, na si kutii WAFU."

ila ukweli wa mambo ni kuwa neno SHETANI sio neno lenye asili ya kiafrica . Concept ya shetani imeletwa afrika. waafrika walikuwa hawaamini uwepo wa shetani.

Mzimu imefananishwa na shetani baada ya dini za kigeni kufika afrika ila
imani ya uwepo wa shetani imeletwa hapo mwanzo haikuwepo.

Waafrika wengi wanaamini mababu zetu hawakuamini Mungu bali mizimu. Kumbe sio kweli Mungu alikuwepo ila tuliamini ndugu zetu waliokufa walikuwa wanatuunganisha sisi na Mungu, hivyo ili maombi yako yafanikiwe unaongea na mizimu (marehemu wa ukoo wenu).

Waafrika tuliamini Mungu, ila tukaamini Mungu yuko karibu na wafu (mizimu/mababu na ndugu walokufa) ambao tuliamini wanaishi katika mibuyu na miti nk. Sio kwamba tuliabudu miti

Ndio maana dini za Kiafrika hazikuwa na wamisionari wa kusambaza kwasababu, kila mtu aliomba Mungu kupitia mizimu ya ukoo wao. Mizimu ya ukoo wa mwezako ulikuwa hakusaidii hivyo hakukuwa haja ya kusambaza dini za asili, kila mtu aliomba kikwao.

Ila watu weupe ndio wakatufunza kuwa Mungu kwa imani zetu sio sahihi. Kwahiyo wasingekuwa wao bado tungeamini Mungu kinamna yetu.

nakualika kaka Mshana Jr katika kutoa mawazo yako katika hili andiko

Back
Top Bottom