Kabla ya mwezi Julai 2025, kuna jambo zito mno! Giza nene

Hata akiondoka hakuna, kitakachobadirika,
Shida iko kwenye system.
Aliondoka yule, kaingia huyu, ambae watu wengi walimuona mpole, ana huruma na kadhalika.
Lakini baada ya hapo "system" ikaanza kafanya yake.

labda tuombe Mungu tupate ambae hatopenda nguvu na mamlaka aliyopewa na Katiba. Na ni nani huyo.
 
Hizo ni ramli chonganishi. Hujui kuwa sikuhizi makanisani pia kuna uganga na ramli?
 
Wakati wa Mungu kuleta ukombozi kwa watu wake hakuna cha tahadhari wala nini.
Kapeace labda atakuwa amesahau historia....

Watawala wajinga waliokwisha kuota jeuri na kiburi cha madaraka hata kama wakichukua tahadhari zote ikiwemo kulindwa na madege kulia, kushoto, nyuma, mbele na angani pamoja na wachawi, huwa haisaidii chochote iwapi wakati wa Mungu Yehova kuwatoa ukifika, basi unakuwa umeshafika tu...

Hivi kuna mtawala gani jeuri, mwenye kiburi na aliyekuwa anajiona kuwa yeye ndiye mwanzo na mwisho (Alfa & Omega) aliyewahi kutokea ktk ulimwengu huu kumlinganisha na Farao wa Misri ya wakati wa nabii Musa..?

Huyu jamaa alikuwa jeuri eti si mchezo...

Huyu jamaa alikuwa na kiburi eti si mchezo...

Alizungukwa na majeshi ya kila aina yenye kila aina ya silaha na zana za kivita pande zote mpaka angani ktk kujilinda kwake..

Huyu jamaa alizungukwa na wachawi wa kila dizaini ili kumsaidia kushindana na Mungu...

LAKINI, hebu angalia mwisho wake ulivyokuwa mbaya na wa aibu...

Yeye na wanajeshi wake, silaha zake za kivita, na wachawi wake walizikwa chini ya maji ya bahari ya Shamu mpaka leo...!
 

Tumefika kubaya sasa kama nchi. Yaani imefikia hatua ya kushangilia "parapanda italia"!! Aloo!!!

Kumbe sisi sote ni sawa. Maana anayeshindwq kukemea ya Mdude na kusema "kifo ni kifo" huyo nae ni pacha na hata tofauti ya anayelilia na kupiga ramla za "parapanda italia"...

Halafu maisha yalivyo bhana unaweza kuta akaja mwingine mbaya zaidi hadi ukamkumbuka marehemu. Jamaa 1 mwalimu wa Sec ile night ya 17.03.21 alishangilia na kunywa bia sana parapanda kulia coz anasema for 6yrs hakuwahi kuongezewa salary. Siku hizi kila nikikutana nae nikimkumbusha anasema alibugi big time coz mwendazake alikuwa machine,mtu na nusu.
 
Tunahitaji mabadiliko na road map ya hayo mabadiliko imeshawekwa mezani .. Je kwanini kuna hofu ya mabadiliko? Na kwanini wenye hofu ni hao waliovimbiwa?
 
NINI KINATOKEA!!
 
Kama itakua ni bibi chaudere anafanyiwa sub na sir God basi itakua ni kitu bora sana kuwahi kutokea tangu dunia kuumbwa, ngoja niandae bajeti ya kitimoto mzima kabisa
Hahaha we jamaa
 
Kwani mfaji kanena lolote hata sasa?,hakika mtwaaji atakuwa ameifanyia wepesi nchi
 
Angekuwa kajipanga, asingekubali pawe na ushidi wa 99% serikali za mitaa, ushindi huo ndio chanzo Cha NO REFORMS NO ELECTION.

Alipaswa aache uwanja huru wapate hata 50% ili wajue uchaguzi mkuu wanashinda, halafu wahujumiwe wakati wa uchaguzi mkuu.

NO REFORMS NO ELECTION, ni zao la MIMBA YA UCHAGUZI WA SERKALI ZA MITAA 2024, angekuwa kajipanga asingekubali ujinga ulofanyika!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…